Makazi ya Wananchi 500 Ubungo - Kisiwani (Dar) yapo hatarini, tunaomba Serikali itujengee mifereji ya kusafirisha maji ya mvua kutoka Barabara Kuu

Makazi ya Wananchi 500 Ubungo - Kisiwani (Dar) yapo hatarini, tunaomba Serikali itujengee mifereji ya kusafirisha maji ya mvua kutoka Barabara Kuu

Poleni sana.kizimkazi yeye anajua kulipa magoli ya mpira milioni kumi Kila Moja lakini hayo ya kuzuia kingo za moto anasema hayamuhusu.
 
Taarifa imewasilishwa vizuri na inaeleweka.

Ushauri: Msisubiri tena ahadi kutoka kwa yeyote, fanyeni maamuzi magumu ya kuhama hilo eneo.
Maji yana nguvu hasa kwenye njia yake.
Najua uchumi mgumu, kuhama ni njia ya uhakika zaidi
 
Kwa mtazamo wangu sioni kama hilo ni tatizo la kudumu bali la msimu. Huo mtu si wa kudumu bali wa msimu hivyo maswali ya msingi ni kwa nini wakati si wa mvua serikali isitengeneze mfumo wa kuudhibiti huo mto?

Nimeona maeneo mbali mbali ya nchi mito ya msimu inavyodhibitiwa.Maana kwa mujibu wa picha zilizowekwa, huo mto ni wa msimu kupeleka maji mto Msimbazi. Maana yake wakati si wa masika kuna fursa kubwa sana ya kutengeneza njia hiyo ya maji kuwa salama.
 
Kama viwanja hivyo vilipimwa na kuidhinishwa na serikali kwa makazi ya watu, kwa hilo serikali inawajibika kwa kugawia wananchi viwanja vya kujenga maeneo hatarishi.

Lakini kama ujenzi ni wa holela kwa kuvamia maeneo kwa kupimiana viwanja kwa hatua za miguu ninyi kwa ninyi, serikali haitabeba mzigo huo, kwani mlijitakia wenyewe na hivyo mnabeba mizigo mliyojibebesha wenyewe.
 
Poleni sana.mlitakuwa kuhama tuhapo,serikali msiitegemee sana
 
Back
Top Bottom