Kama viwanja hivyo vilipimwa na kuidhinishwa na serikali kwa makazi ya watu, kwa hilo serikali inawajibika kwa kugawia wananchi viwanja vya kujenga maeneo hatarishi.
Lakini kama ujenzi ni wa holela kwa kuvamia maeneo kwa kupimiana viwanja kwa hatua za miguu ninyi kwa ninyi, serikali haitabeba mzigo huo, kwani mlijitakia wenyewe na hivyo mnabeba mizigo mliyojibebesha wenyewe.