Kuna wakati wanachama wa ccm walijaribu kutaka kutenganisha URAIS na UENYEKITI wa chama chao na sababu kubwa iliyowafanya wawe na shauku hiyo ni jinsi Mwenyekiti wao ambaye pia alikuwa Rais wa nchi alivyokuwa anakiweka chama hicho rehani kwa wafanyabiashara na wao hawakuwa na jinsi ya kumthibiti, kwani pia alikuwa mkuu wa vyombo muhimu vya dola!! Walidhania kwa kufanya hivyo wangeweza kuondoa conflict of interest iliyokuwepo; hata hivyo Kikwete akiwa madarakani aliweza kuzima jaribio hilo la kutenganisha kofia ya Rais na mwenyekiti kwani alihisi kuwa hilo lilikuwa jaribio la kutaka kudhoofisha uongozi wake.
Hive sasa Kikwete sio Rais tena lakini bado ni mwenyekiti wa ccm. Rais Magufuli ndiye Rais wa nchi ambae kwa siku za mwanzo wa ungozi wake ameonesha nia ya dhati kabisa ya kutaka kuleta maendeleo ya nchi kwa kasi ya peke yake kwa kuhumiza watu wafanye kazi; kupiga vita ufisadi kwa vitendo na kuweza kukusanya kodi ya kutosha. Utendaji wa serikali ya Magufuli ni tofauti kabisa na utendaji wa awamu ya Kikwete hivyo kuweka wazi kabisa kuwa chama na serikali yake huko nyuma vilikuwa havifanyi kazi ipasavyo. Ni uwekaji hadharani huu wa udhaifu wa awamu zilizopita ndiko kunakowatisha Kikwete na wafuasi wake ndani ya chama kuwa iwapo Magufuli ataachiwa kuwa Mweneyekiti wa ccm na pia rais wa nchi kama ilivyozoeleka huko nyuma , anaweza kuwaumbua na kuwathibiti mafisadi wengi waliojificha kwa mgongo wa chama na ndio maana hivi sasa juhudi kubwa zinafanywa kumzuia asiwe mweneyekiti wa ccm . Vinara wakubwa wanaoongoza juhudi hizo ni Mwenyekiti wa ccm wa sasa anayetaka yeye mwenyewe aendelee ili aweze kutumia ngao hiyo ya uenyekiti kujikinga na maovu yake ama sivyo amsimike kibaraka wake achukue nafasi hiyo; na ndio maana wameanza kupima upepo kwa kuyataja majina ya kina Anna Makinda kuwa mmoja wa prospective wenyeviti wa ccm!!
Makinda amekuwa mwanachama wa siku nyingi na kusema kweli amekulia ndani ya ccm; huwezi kumtenganisha na uozo wote ulikuwa unatendeka ndani ya chama hicho. Kumuweka Makinda kama mwenyekiti wa chama hicho utakuwa mwendelezo wa mambo yale yale yaliyokuwa yanafanyika miaka nenda miaka rudi ambayo sasa hivi ndio majipu yanayotubuliwa na Rais Magufuli. Jinsi alivyolelewa na kukuzwa Anna Makinda ndani ya chama ni lazima atajaribu kuyaficha majipu hayo hivyo ili Magufuli afanikiwe kuyatumbua nilazima apewe uenyekiti wa ccm; iwapo itatokea watamyima na kumpa mtu ambaye atajaribu kuyaficha hayo majipu kwa kutumia mgongo wa chama hapo ni lazima kutatokea mgongano ambao kwa vyovyote vile Magufuli ambaye ndio ana dola atashinda, na ili kuepusha mgongano huo ni vyema Rais Magufuli akawa pia mwenyekiti wa ccm!