Makinda: Matokeo ya SENSA yatatangazwa mwisho wa mwezi Oktoba 2022

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022, Spika mstaafu Anne Makinda amesema matokeo ya sensa hiyo iliyofanyika Agosti 23 yatatangazwa mwisho wa mwezi huu na matokeo yatabandikwa kwenye mbao za matangazo.

Makinda ameyasema hayo leo Oktoba 12 na kusema hatua zote za uchakataji wa takwimu zimeshakamilika na matokeo yapo tayari, yakisubiri kutolewa tarehe yoyote mwishoni mwa Oktoba.

โ€œTangu kukamilika kwa kazi ya kuhesabu watu, wataalam wamekuwa wakiendelea na uchakataji wa taarifa zilizokusanywa, nitumie fursa hii kuwaeleza kuwa kazi hii imekamilika. โ€œMatokeo haya yatazinduliwa na Rais mwishoni mwa mwezi huu katika tarehe itakayotangazwa na maandalizi ya tukio hiyo yanaendelea,โ€ amesema Makinda.

Pamoja na kutangazwa amesema taarifa za matokeo hayo zitawekwa katika mbao za matangazo katika kata, shehia, vijiji, mitaa na vitongoji.
 
Sawa Usipohesabiwa Ujue Fungu Lako Halipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ