Makonda aanza kukamata wakusanya madeni (auctioneers) wanaotumwa na mabenki

Waliouziwa nyumba kupitia mkopo kausha damu na Kampuni ya Heritage financing limited y iliko Arusha tukutane kwa makonda Kesho saa 4 asubuhi. Tuna jambo letu
Fanyeni chap Makonda baba wa upendo namwombea hii operation ije na mafanikio. Tumechoka na uhuni wa hizi taasisi
 
Huyu ndio Kiongozi sasa. Mkopo wa milioni tatu na mkopaji analipa unaenda kuuza nyumba ya milioni hamsini? Tia ndani!!!
 
Jaribu kutumua akili kidogo. Hizi ni acquisition ambazo zinatakiwa kuwa treated with utmost care. Huwezi kuamuru watu wawekwe ndani kabla ya hata ya kusikiliza pande zote. Wajinga wajinga kama wewe ndiyo mnafanya nchi izidi kudidia kwenye matatizo.
 
Elimu mbovu imekuwa ni disaster kwa nchi yetu. Watu wengi hamwezi kutafakari mambo kwa upana na urefu. Pole sana kwa ufinyu wako wa kutafakari kwa sababu wanaoona Makonda ni shujaa mko wengi na siyo kosa lenu, bali mfumo wa elimu.
huo ujumbe ungeugeuza kisha ukaanza kujitafakari , kwamba Makonda awashike wakusanya madeni yao bila sababu za msingi , umeandika ujumbe mzuri ila unakuhusu wewe na mnaompinga Makonda , hata Msukuma haez mshika mkusanya madeni bila sababu ya ziada , WAJINGA MSIOPENDA KUMENG'ENYA MAMBO MPO WENGI SANA , MKISOMA HABARI INASEMA MAKONDA AKAMATA WAKUSANYA MADENI BASI MNAIMEZA KAMA ILIVYO NA HAMTAK KUMENG'ENYA ZAID KUUJUWA UKWEL , HASA WENGI WENU MNAENDESHWA NA CHUKI DHIDI YA MAKONDA

SIO WOTE TUNAMUUNGA MKONO MAKONDA KWENYE , NI MASHABIKI WA UONGOZ WA MAKONDA LKN JAMII INAYOJITAMBUA HUWA HAIFANYI MAAMUZI KWA CHUKI BALI KWA UHALISIA WA JAMBO
 
Jaribu kutumua akili kidogo. Hizi ni acquisition ambazo zinatakiwa kuwa treated with utmost care. Huwezi kuamuru watu wawekwe ndani kabla ya hata ya kusikiliza pande zote. Wajinga wajinga kama wewe ndiyo mnafanya nchi izidi kudidia kwenye matatizo.
Sawa dada mkubwa mwenye akili.
 
hiyo ndiyo mikopo ya kausha damu ipigwe marufuku
 
Iuzwe ikatwe 3M chenchi arudishiwe. Dawa ya deni ni kulipa tu
 
Iuzwe ikatwe 3M chenchi arudishiwe. Dawa ya deni ni kulipa tu
Mpaka inafikia kuuzwa hao hawataki 3m. Itakuwa riba ilikuwa kubwa deni halilipiki ila kwa ilipofikia hapo watachukua hiyo hiyo tatu yaishe. Tena pengine kwa awamu.
 
Umepost upupu gani yani mtu anadaiwa miliion 3 unamuuzia Nyumba? Hizi Demokrasia zinatumika vibaya watu kama hawa ni wakunyonga tu.
Umekopa lipa! Au tafuta hizo mi3 sehemu nyingine sio kufilisi bank. Ukipewa pesa rudisha ili apewe mwingine, kila mtu akipewa pesa Akakaa nazo bank zitafilisika
 
#Mama yupo Kazini.
 
Hakuna lazima alipe yote huo ndio ya utaratibu
Mpaka inafikia kuuzwa hao hawataki 3m. Itakuwa riba ilikuwa kubwa deni halilipiki ila kwa ilipofikia hapo watachukua hiyo hiyo tatu yaishe. Tena pengine kwa awamu.
 
Umekopa lipa! Au tafuta hizo mi3 sehemu nyingine sio kufilisi bank. Ukipewa pesa rudisha ili apewe mwingine, kila mtu akipewa pesa Akakaa nazo bank zitafilisika
Kuna madeni yakuuza nyumba ila sio Million tatu ! sehemu kama Arusha CC kiwanja cha millioni tatu utakipata mtoni sembuse Nyumba ?
 
Umekopa lipa! Au tafuta hizo mi3 sehemu nyingine sio kufilisi bank. Ukipewa pesa rudisha ili apewe mwingine, kila mtu akipewa pesa Akakaa nazo bank zitafilisika
Bank haifanyagi huu ujinga. Taratibu za kuweka dhamana ya nyumba bank ili ukopeshwe ni ngumu kidogo na wapo makini na uwezo wa mkopaji hata kama ana dhamana, unless huo uongozi uwe wa kijinga. Bank hizi zinazojielewa ikishafikia kuwa inauza nyumba si rahisi kupona, itauzika, hata uende kwa waziri mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…