Hivi hujui kwa katiba yetu hii ya hovyo, hairuhusu mtu yeyote kufungua kesi ya jinai dhidi ya yeyote, isipokuwa DPP? Kwa katiba yetu hii ilivyo, hata kama jitu likaja hapo kwako likamwua mwanao huku ukiwepo, na hilo jambazi ukalitambua kwa jina na sura, bado DPP asipotaka kulifungulia kesi, wewe huna cha kufanya, zaidi ya kupiga kelele tu!! Ndiyo maana hili shetani, chini ya mwavuli wa "Wasiojulikana", lilisimamia mauaji mengi likiwa na uhakika wa kutoshtakiwa kwa sababu ushetani aliokuwa anaoufanya ulikuwa na baraka za mkuu wa Serikali.