Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Nafahamu kwa Mada za Nyama choma ya Makonda kule Arusha ziko nyingi sana humu JF, % kubwa za mada hizo zikiwa ni za kusifia, hili la kusifia chakula cha Bure si geni kwa Wabongo kutokana na dhiki kali inayowakabili, Watani zangu Wangoni wana msemo mmoja kuhusu njaa, nanukuu, "NJALA LIKOKO LIKOMA NA MUHABHI" Mwisho wa kunukuu, Kwa tafsiri ya kiswahili wanamaanisha kwamba Njaa ni kama Fisi inaua hata Mchawi, Kama nakosea Ndumbaro au Jenista Mhagama wanaweza kunisahihisha.
Kwa bei ya Vijijini kabisa ng'ombe mmoja mkubwa wa kuchinja hawezi kuwa chini ya sh laki 7 za kitanzania, sasa kwa hesabu za shule ya msingi au Kayumba.com ng'ombe 400 wanagharimu mil 280, Hela hizi si ndogo na kwa kadri ya vipato vya halali vya Wakuu wa Mikoa wa Tanzania, haiwezekani Mkuu wa Mkoa kulisha watu ambao kwao wameacha ugali na dagaa kwa gharama hii, hana hela hizo.
Ikumbukwe kwamba hiyo mil 280 ni gharama ya ng'ombe tu, haihusu Wachinjaji, Wachomaji, Majiko, viungo na gharama zingine, Makonda ametoa wapi hela za kugharamia mchakato huu wa kugawa bure mitaani?
Mnaweza kushangaa kwamba labda inakuwaje tunahoji masuala ya chakula tu, na mkaona kama ni kitu kidogo, ni hivi, tukiacha kuhoji zilikotoka hela hizi tutakuwa tunakosea sana, Mkuu wa Mkoa hana hela hizo na wala hakuna mtu wa kumchangia vitita hivyo kwa hiyari, Zingatia neno hiyari.
Je Makonda alipata wapi mamilioni ya hela ya kuyatumbua kirahisi namna hii tena bila sababu yoyote ya msingi, Kama ni ziara Rais anatembea Nchi nzima, Ni wapi kwingine walifanya hivyo, huko hakuna Wakuu wa Mikoa?
Naomba Kuwasilisha.