Pre GE2025 Makonda amjibu Waziri Bashe, asema atamhoji sababu yeye ndiye anakitafutia kura chama

Pre GE2025 Makonda amjibu Waziri Bashe, asema atamhoji sababu yeye ndiye anakitafutia kura chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ukweli na jibu ni moja tu kuwa chama ni kikubwa kuliko serikali na ndicho kilichounda serikali.kwa hiyo Mheshimiwa Makonda ambaye ndiye msemaji wa chama anaweza kumuhoji na kutaka majibu kutoka kwa waziri yeyote yule akiwepo Bashe mwenyewe.

Kwa hiyo kama kwa mfano Mheshimiwa Bashe hataki kuhojiwa na kuulizwa na Mheshimiwa Makonda inatakiwa ajiuzulu haraka sana uwaziri wake ili Mheshimiwa Rais ateue waziri mwingine atakayetoa ushirikiano mzuri kwa chama, ambacho ndio kitakacho kwenda kuomba kura kwa wananchi.

Huu mchezo hauhitaji hasira wala kupandisha mabega wala kuvuta mdomo .chama ndio Top.
 
Yani kama naona Shule ya Msingi hapa watoto wanapiga kelele.

"ZIPIGWEEE, ZIPIGWEE".

Halafu mtoto mshari mmoja anajaza mchanga kiganjani, anawafuata wote wawili anawaambia "PUTAAA, PUTAAA".
Umenikumbusha mbali kiranga nimewahi kumchapa mtu hivi hivi wakati huo kisa hii michezo ya kuwekeana michanga
 
Umenikumbusha mbali kiranga nimewahi kumchapa mtu hivi hivi wakati huo kisa hii michezo ya kuwekeana michanga
Hiyo kama umesoma shule zetu enzi zetu kazima uijue.

Halafu ukishawekewa mchanga upute, it is a matter of honor. Yani usipoputa ukitoka hapo wewe si kidume 🤣🤣

Na ukiputa tu, shughuli inaanza.
 
Hiyo kama umesoma shule zetu enzi zetu kazima uijue.

Halafu ukishawekewa mchanga upute, it is a matter of honor. Yani usipoputa ukitoka hapo wewe si kidume 🤣🤣

Na ukiputa tu, shughuli inaanza.
Hapo ni suala la kuwaiana tu mkipiga mchanga hamna kupoteza muda ni kumtandika mwenzako chap chap😆 ukizembea ana kunyuka wewe.

Msipo pigana mnaonekana wote wazembe. Muda mwingine ugomvi hata hamna ila tu ili apatikane mbabe wa darasa kinachapwa kwa mtindo huo😀😀
 
Akili kubwa na chawa wa muhimu Kwa Kiongozi Huwa ni chawa.

Makonda anatafuta kura za Samia,Bashe anatafuta kura za nani? Anaweza kutumbuliwa na Ubunge akakatwa.

Japo wote ni Vijana wa Mama anawamudu.
Bashe kwa sasa ni waziri, ni mtumishi wa Umma, hayupo kutafuta kura. Hii nchi imeharibiwa kwa akili hizi hizi za kusaka kura kila wakati.
 
Hapo ni suala la kuwaiana tu mkipiga mchanga hamna kupoteza muda ni kumtandika mwenzako chap chap😆 ukizembea ana kunyuka wewe.

Msipo pigana mnaonekana wote wazembe. Muda mwingine ugomvi hata hamna ila tu ili apatikane mbabe wa darasa kinachapwa kwa mtindo huo😀😀
Ila ukifuatilia watu tuna unyama fulani hivi.

Tabia zetu ni zlle zile za ku mark territory, ku establish dominance, kutaka kuonekana zaidi.

Yani it doesn't matter mtoto wa shule, waziri, silverback gorilla, deep down tuna hiyo violent and competitive streak.

Mimi najaribu sana kuikwepa hii siku hizi.

Hapa JF mpaka unashangaa, kitu kidogo tu watu wanalipuana.
 

Bashe ni akili kubwa, ni mtu makini anayejua kusimamia anachoamini, kubwa zaidi sio mnafiki.

Makonda ni akili ndogo, mtu anayeweza kutumika vizuri na baada ya matumizi akatupwa mbali. Yeye hajali, yeyote mwenye madaraka anaweza kumtumia kwa kazi yoyote.

Hakuwezi kuwa na vita kati ya akili kubwa na akili ndogo, hapo ni mmoja anaanika ujinga wake na mwingine anaanika ubora wake.
Usimdanganye Mheshimiwa Bashe na kumjaza upepo wa uongo. Chama ni kikubwa kuliko serikali.waziri hayupo juu ya chama.kwa hiyo lazima ufahamu ya kuwa Mheshimiwa Bashe Hawezi kuleta kiburi wala dharau wala jeuri kwa chama na viongozi wa chama akiwepo Mheshimiwa Makonda.

Mheshimiwa Bashe Anaweza kupigiwa simu na mheshimiwa Makonda ili atoe majibu na itampasa atoe majibu stahiki. Bashe alijisahau tu pengine alitanguliza hasira na jazba badala ya hekima,busara na unyenyekevu. Alisahau kuwa anaweza kuitwa na viongozi wa chama. Mtu anayefahamu hadhi ya CCM, historia ya CCM na nafasi ya chama katika serikali hawezi kusema kuwa ana mabosi wanne tu.

Maana hapo inaonekana amekidharau chama ikiwepo na viongozi wake kuanzia makamu mwenyekiti Taifa,katibu mkuu,na naibu katibu wakuu n.k.

Swali ni je mpaka amekuwa waziri alikuwa nani awali? Si alikuwa mbunge? Je unaweza kuwa mbunge bila chama cha siasa? Kwahiyo leo chama hakina hadhi na viongozi wake baada ya yeye kuwa waziri? Je uchaguzi ujao atarudi kugombea na kuingia bungeni kupitia njia ipi? Je hafahamu kuwa hata Mheshimiwa Mwenyekiti wetu amefika hapo alipo kwa kuwa chama kilimpendekeza na kumpa baraka katika hatua mbalimbali mpaka kufikia hapo?

Mawaziri vijana waache kujisahau na kutoa maneno ya dharau na kutaka kujiona wamekuwa wakubwa sana.huo uongozi na uwaziri amepata ni kwa kuwa chama kilipambana majukwaani kupata kura nyingi na kuunda serikali na hivyo naye akapata nafasi ya kuteuliwa kuwa waziri.kwa hiyo Mheshimiwa Bashe asilete kiburi kwa chama.
 
Mnapenda uchongonganishi hayo maneno kasema wapi? Weka video tuone akimtaja bashe.
 
Ndiyo shida ya kuweka Vijana kwenye nafasi kubwa za Uongozi kama hizo!
 
Akili kubwa na chawa wa muhimu Kwa Kiongozi Huwa ni chawa.

Makonda anatafuta kura za Samia,Bashe anatafuta kura za nani? Anaweza kutumbuliwa na Ubunge akakatwa.

Japo wote ni Vijana wa Mama anawamudu.
Safi sana ndugu yangu umetoa jibu zuri sanaa. Mheshimiwa Makonda anapambania chama na kumtafutia kura Mheshimiwa Rais .halafu hapo hapo Bashe anataka kupunguza kura za Mheshimiwa Rais kwa kuleta kiburi na ujuaji. Bashe afahamu kuwa yeye siyo waziri wa kwanza wa kilimo.anaweza ondolewa hapo alipo na akakaa mtu mwingine na kazi zikaenda vizuri kabisa .

Kwa hiyo asilete ujuaji na visasi vyake. Kwani mawaziri waliotoa ushirikiano kwa chama wamepungukiwa nini na amewazidi nini? Mbona hadi waziri mkuu wetu kwa unyenyekevu mkubwa kabisa alisema serikali imepokea maelekezo ya chama juu ya migogoro ya ardhi? Kwahiyo Bashe ni special sana na anajiona ana akili sanaa kuliko hao mawaziri wengine wote ee akiwepo hadi waziri Mkuu wetu?
 
The Second Coming
BY WILLIAM BUTLER YEATS

Turning and turning in the widening gyre
The falcon cannot hear the falconer;
Things fall apart; the centre cannot hold;
Mere anarchy is loosed upon the world,
The blood-dimmed tide is loosed, and everywhere
The ceremony of innocence is drowned;
The best lack all conviction, while the worst
Are full of passionate intensity.

Surely some revelation is at hand;
Surely the Second Coming is at hand.
The Second Coming! Hardly are those words out
When a vast image out of Spiritus Mundi
Troubles my sight: somewhere in sands of the desert
A shape with lion body and the head of a man,
A gaze blank and pitiless as the sun,
Is moving its slow thighs, while all about it
Reel shadows of the indignant desert birds.
The darkness drops again; but now I know
That twenty centuries of stony sleep
Were vexed to nightmare by a rocking cradle,
And what rough beast, its hour come round at last,
Slouches towards Bethlehem to be born?
 
Back
Top Bottom