Pre GE2025 Makonda amjibu Waziri Bashe, asema atamhoji sababu yeye ndiye anakitafutia kura chama

Pre GE2025 Makonda amjibu Waziri Bashe, asema atamhoji sababu yeye ndiye anakitafutia kura chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Akili yako siyo nzuri kiafya
Screenshot_20231111_190308_Google.jpg
 
Nani amekwambia mimi ni mpinzani? Napinga nini kwanza? Ujinga umewafanya muone kila anayekosoa na kushauri ni mpinzani.
Huwezi ukawa kwenye timu ukasapoti mambo ya timu nyingine kwa kigezo cha kukosoa. Kama umeamua kuwa mpinzani kuwa mpinzani kama ni CCM ni CCM... Usilete unafiki
 
Hizi ni Sarakasi na kupotezeana muda na kumdanganya mwananchi kwamba mambo yanafuatiliwa..., fumba fumbua miaka mitano / kumi imepita na hakuna kinachofanyika.....

Badala ya kusema nitamuhoji kwanini asitumie huo muda kuhoji ?!!!, By the way sio yeye tu hata mimi nina mengi ya Kumuhoji hata Rais sababu kama hii ni Merikebu sasa hivi inakwenda Mrama.....
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=Ht5d6FpCBF8

Ukitaka kujua ukaribu wao ‘bi-tozo’ siku hizi atoi mkono wake kiholela, ila kwa Makonda hana shida kumpa mkono.

Body language tu inakwambia ni watu wa karibu sana sidhani kama kuna kiongozi wa serikali au chama anaweza ongea na raisi akiwa relaxed kama Makonda anavyoonekana kwenye hiyo clip.
 
Mbona naona jambo tofauti? Wote wanaigiza na hawamaanishi!
Wenye sukari kwenye magodauni wamemwaga mpunga wa haja kwa mwenye kipasa sauti ili apaze sauti yake kuzuia na ama kuchelewesha matumizi ya bei elekezi ya sukari nao wamalize mzigo kwa kuuza bei iliyopo sokoni sasa.
Mwenye bei elekezi kang'amua mbinu hiyo na kujidai kuilinda kauli yake ya bei elekezi huku akijua Hana sukari ya kuuza bei elekezi!
Hii sanaa Yao ni ngumu mno wanaoshangilia kwa kuchagua upande kujua dhima ficho ya Hawa watatu yaani wafanyabiashara, mpaza sauti na mwenye bei isiyoelekezeka. Walaji tumedungwa, badala ya kugugumia maumivu tunapiga mayowe ya kushangilia mithili ya mazuzu. Ccm ni mabingwa wa dramma!
 

View: https://m.youtube.com/watch?v=Ht5d6FpCBF8

Ukitaka kujua ukaribu wao ‘bi-tozo’ siku hizi atoi mkono wake kiholela, ila kwa Makonda hana shida kumpa mkono.

Body language tu inakwambia ni watu wa karibu sana sidhani kama kuna kiongozi wa serikali au chama anaweza ongea na raisi akiwa relaxed na kama Makonda anavyoonekana kwenye hiyo clip.

Yaani anaishika pua yake na mkono huo anampa rais naye anaupokea bila kuchukua tahadhari ya kiafya! Nimetetemeka kwa uoga wa COVID-19!
 
Yaani anaishika pua yake na mkono huo anampa rais naye anaupokea bila kuchukua tahadhari ya kiafya! Nimetetemeka kwa uoga wa COVID-19!
Utoi mkono kwa raisi mpaka akupe wake. Tazama hapo wote wamefunga mikono yao.

Raisi mwenyewe siku hizi atoi mkono wake ovyo kampa Makonda tu. Inakwambia huyo ni mtu wake wa inner circle na anamuamini kama anavyomuamini mtoto wake wa kumzaa.

Kwa sasa vita na Makonda is not a good idea, anachozumgumza ni kile ambacho boss hataki kukisema mwenyewe kwa jinsi walivyo karibu inavyoonekana.
 
Siasa ndio sarafu ya taifa kwa wakati huu.

Tena siasa za majitaka.

Nani kidume zaidi ya mwenzake katika siasa za majitaka kati ya hao wawili?

Simtakii yoyote kati yao ushindi.
 
Yaani anaishika pua yake na mkono huo anampa rais naye anaupokea bila kuchukua tahadhari ya kiafya! Nimetetemeka kwa uoga wa COVID-19!
Aisee nimeshangaa sana, afu ona Makonda hana habari na Nchimbi...

Nchimbi anaonekana kama Mgeni wa mambo ukiangalia kisaikilojia unaona kuna mission ya hali ya juu sana kwa kijana huyu.

Asante sana Clip imenifungulia jambo
 
Yani kama naona Shule ya Msingi hapa watoto wanapiga kelele.

"ZIPIGWEEE, ZIPIGWEE".

Halafu mtoto mshari mmoja anajaza mchanga kiganjani, anawafuata wote wawili anawaambia "PUTAAA, PUTAAA".
[emoji23][emoji23]
 
Imekuwa wiki ya kutupiana vijembe kati ya mahasimu wa muda mrefu Husein Mohamed Bashe na Paulo Christian Makonda, mahasimu hao wa muda mrefu toka 2014 wakiwa katika makundi ya kuusaka urais wa 2015, Makonda ambae ni kijana wa Sitta adui mkubwa wa Mzee Lowassa walianza kutupiana maneno makali muda mrefu.

Makonda akiwa ziarani siku ya jana amemjibu waziri wa kilimo Bashe kuwa atamhoji tu kwasababu yeye ndio anakitafutia kura chama hicho.

Bashe alinukuliwa mwisho wa wikii hii akiwajia juu wafanyabiashara wa sukari kwa kufanya lobbying kwa Paul Makonda ili aondoe bei elekezi.

Rai Yangu: Ni vyema vyombo vya maamuzi visiingilie ugomvi huu kwasababu ni kutunishiana misuli kwa vijana wala hakuna jambo serios sana, asitokee wa kuonewa maana wote wanaviziana muda mrefu tu, asionewe mtu.
Makonda akiihoji miradi inamaana anamuhoji Mama Samia, hilo hatoweza kufanya, usifiri yeye hana akili.

Utakuta unaeadndika ni fataani tu mooja ambae sio CCM na chama chako hakina sera unaanza fitina za kijinga.

Wakihojiana wasihojiane, wewe kinakuwashia nini?
 
Malumbano na mivurugano yenu; ndiyo furaha yetu sisi wapenda mabadiliko.
Malumbano yao hayajawahi kuwa msaada wowote kwa wapenda mabadiliko, ikifika wakati wa uchaguzi wana ushirikiano na lugha moja kuliko sisi wapenda mabadliko.

Wanajua kucheza na akili za watu wengi, tumekuwa wasambazaji wa taaifa zao zaidi na focus imekuwa kwa shu zao kuliko mijadala ya kuleta mabadiliko. Sad.
 
Kama unge

KAMA ungejua serkali inatekeleza ilani ya chama ambacho ni ccm ungekaa kimya.
Bashe yuko hapo kwa mgongo wa chama asilete usanii ataliwa kichwa na wanamjua ni timu Lowasa na Msomali
Usilazimishe mambo yasiyo na maana. Huo unaoutetea ni upuuzi, yaani upuuzi wa katiba.
 
Back
Top Bottom