ukikaidi utapigwa2
JF-Expert Member
- Feb 24, 2015
- 15,265
- 29,991
Kwa akili zake huyo jamaa sijui kama ata hudumu miaka 2 hio nafasi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ninachokiamini ni kwamba,kauli aliyoitoa imejaa chuki kubwa na visasi.Anaongea kuanzia mwisho kurudi mwanzo kwa anayeamini ni adui yake.Muda hutoa sauti kuu.😊😊
Labda kuna ambao wanataka nafasi yake. Au uwepo wake duniani kwa wengine wanaona ni kero hivyo watataka kumdhuru
Uhalisia hujidhihirisha hata mtu akivungavunga kuenenda na mapigo ya tumbuizo la muziki.😀😀
Unahasira naye Mkuu.
Wanapofyeka majina ya wagombea Mwenezi hashiriki?Kwenye nafasi yake hiyo anawezaje kulipa kisasi hata kama angetaka kulipia kışasi?
Ninachokiamini ni kwamba,kauli aliyoitoa imejaa chuki kubwa na visasi.Anaongea kuanzia mwisho kurudi mwanzo kwa anayeamini ni adui yake.Muda hutoa sauti kuu.
Kwa akili zake huyo jamaa sijui kama ata hudumu miaka 2 hio nafasi
Mwenye hila hakosi jambo.Akishindwa kudhuru mwili,atasonya ujikwae.Wanapofyeka majina ya wagombea Mwenezi hashiriki?
Mpe muda.Ataongea kwa lugha ya picha zenye rangi nzurinzuri.Ni kama hadithi ya mfalme mwenye masikio marefu kama masinia ya ubwabwa.Sasa hapo kwenye visasi ndio mimi nimeachwa. Yaani yeye kakosewa jambo gani kama kiongozi alafu wananchi wasijue? Jambo hilo ambalo ndilo anakiri hadharani kuwa hatalipa kisasi. Hapo ndipo mimi nimeachwa.
Kwa mfano Lisu, watanzania wote na Watu duniani tunajua alipigwa Risasi. Yeye akisema hatalipa kisasi anauhalali kwa sababu Watu wote tunajua kilichotokea.
Lakini haiwezekani mtu labda kama mimi niseme zitalipa kisasi wakati ninyi hamjui nini nimefanyiwa.
Kwanza niliamini ule ujumbe ulikuwa kwa GSM.Bila shaka Mko Pouwa!
Makonda amesema mbele za Watu kuwa hatalipa Kisasi, kumaanisha kuwa kundi kubwa la Watu analoliambia kuwa hatalipa Kisasi linajua mabaya aliyofanyiwa Makonda.
Hapo kwa upande wangu nimeachwa kidogo kwa sababu sijui nini na kina nani walimfanyia ubaya Makonda mpaka kufikia hatua ya kusema hatalipa kisasi(akimaanisha amesamehe).
Mandela yeye kwa upande wake alisema amesamehe na hatalipa kisasi na wote tunajua nini kilitokea na wabaya wake ni kina nani.
Yesu alipokuwa anasulubishwa naye aliongea maneno hayahaya ya Makonda, hadharani kuwa Mungu awasamehe(asimlipie kisasi) kwa sababu hawajui watendalo. Na wabaya waliomsulubisha walikuwa wanafahamika. Halikadhalika na Stephano aliyekuwa anapigwa Mawe mpaka kufa.
Lakini Kwa Makonda nimeachwa Njia panda, au kuna taarifa imenipita. Sasa nataka yeyote anayejua atuambie ni nini kibaya ambacho Makonda alifanywa ambacho alitakiwa alipe kisasi lakini ameamua kusamehe? Na waliomfanyia huo ubaya ni kina nani?
Ukizingatia kuwa Yeye ndiye ambaye analaumiwa na kushutumiwa kwa ubaya.
Nipo hapa,
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Makonda na hofu ya Mungu [emoji23][emoji23]Visasi ni sehemu ya siasa sasa Huyu Makonda kwa vile ana hofu ya Mungu wa mbinguni amesema hatafanya siasa za visasi!