Makonda anataka kuifikisha wapi tasnia ya habari?

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
01JNTNWQ1SNNF356EFEJX5SVV5.webp

Nimemsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda akizungumza na watumishi wa Wizara yake baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dodoma Januari 13, 2026.

Katika hotuba yake, Makonda aliyekuwa Naibu Waziri akisaidiana na Khamisi Mwinjuma (Mwana FA) chini ya Profesa Palamagamba Kabudi, alitambulisha kuwa ni mtu aliye wazi na asiyependa unafiki, Aliwataka watumishi wa wizara hiyo kujizatiti (kuenea kwenye viti vyao).

Pamoja na ahadi nyingine alizotoa Makonda kwa wizara hiyo, nimejiuliza tu, je anataka kuifikisha wapi tasnia ya habari ambayo ni sehemu ya tasnia anazosimamia.

Fourth Estate

Pamoja na kwamba mawaziri huwajibika kwa aliyewateua, lakini Waziri Makonda ajue kuwa anakuja kuitumikia wizara yenye Mhimili wa nne katika Dola (Fourth Estate).

Dhana ya Mhimili wa Nne katika uandishi wa habari inarejelea vyombo vya habari kama nguvu muhimu na huru katika jamii, vinavyofanya kazi ya kuisimamia na kuikosoa serikali pamoja na taasisi nyingine zenye mamlaka.

Tunajua kuwa katika Dola kuna mihimili mitatu ambayo ni Serikali (Utawala), Bunge na Mahakama, sasa Habari ni mhimili wa nne.

Dhana hii inasisitiza jukumu muhimu la uandishi wa habari katika kuhakikisha uwazi, uwajibikaji, na jamii yenye taarifa sahihi, kwa kuwawajibisha wenye madaraka na kuwezesha mjadala wa umma. Kwa msingi huo, vyombo vya habari vinachukuliwa kuwa nguzo muhimu ya demokrasia.

Ni bahati mbaya kwamba dhana hii imekuwa ikipuuzwa na ikikandamizwa kiasi cha vyombo vya habari kushindwa majukumu yake yanayotakiwa. Njia inayotumiwa na watawala ni sharia kandamizi na kwa hapa Tanzania tuna Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, ambayo bado inalalamikiwa tangu ilipopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Baadhi ya malalamiko yamefanyiwa kazi na bado Serikali ina deni la kusikiliza malalamiko hayo. Kwa mfano wakati Nape Nnauye akiwa waziri wa wizara hiyo, kulikuwa na kamati inayoratibu malalamiko hayo iliyoibua malalamiko 22, lakini yalishughulikiwa malalamiko tisa tu.

Kutoshughulikiwa kwa malalamiko ya sheria hii ndiyo yamefanya vyombo vya habari kushindwa kufanya kazi iliyotarajiwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Kwanza intaneti ilizimwa na hata vyombo vya habari vilivyoendelea kufanya kazi kama redio na televisheni, havikueleza ukweli kuhusu yaliyotokea siku hiyo na kuendelea, yakiwamo maandamano, vurugu, uharibifu wa mali, ukatili na mauaji yaliyofanyika siku hizo za giza.

Wananchi walinyimwa haki ya kupata taarifa kwa mujibu wa Katiba kwa kisingizio cha kulinda amani, badala yake baadhi ya wananchi kwa kutumia simu zao ndio walirekodi matukio mbalimbali yaliyoendelea wakati intaneti imezimwa.

Kwa hiyo Makonda kama waziri mpya, ajue kwamba ana deni la kuhakikisha Sheria ya Huduma za Habari ina malalamiko yanayotakiwa kufanyiwa kazi, kabla ya kuendelea mbele.

Mbali na sheria hiyo, kuna sheria nyingine zinazokwaza uhuru wa habari ambazo ni Sheria ya Makosa ya Mitandao (Cyber Crime Act), Sheria ya Takwimu na Kanuni za Maudhui mitandaoni (Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations).

Mashirika ya habari ya kimataifa

Nimemsikia Makonda akisema, ataunda kikosi kitakachohakikisha habari za Tanzania zinasikika kwenye vyombo vya habari vya kimataifa. Alitoa mfano wa habari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Wang Yi aliyeitembelea Tanzania hivi karibuni na kuzungumza na Rais Samia Suluhu Hassan.

Makonda amesema angetamani kuona habari hiyo ikitokea kwenye mashirika ya habari ya kimataifa kama Aljazeera na CNN. Ni jambo jema, lakini ajue kanuni ya uandishi wa habari inabaki pale pale ya kujua vigezo vya kupima habari.

Tumeona Serikali ikiingia kwenye mgogoro na vyombo vya habari vya kimataifa vilivyotangaza matukio ya vurugu za uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alilalamikia Aljazeera, CNN, BBC na DW kwa kutangaza habari hizo, huku akivipongeza vyombo vya habari vya ndani kwa kukaa kimya.

Kwa hiyo kama Makonda anataka habari zitangazwe na mashirika ya habari ya kimataifa, ajue hayafuati sharia za Tanzania, bali yanafuata miiko ya taaluma ya habari inayofanana duniani kote. Hayo mashirika ya habari hayafuati maelekezo ya Serikali zao wala yoyote duniani, bali yanafuata miiko ya taaluma.

Uchumi wa wanahabari

Nimemsikia Waziri Makonda akisema atamwomba Rais Samia kati ya Sh1 bilioni hadi Sh2 bilioni ili kuwasaidia wanahabari wa mitandao (online) ili wafanye kazi zao. Kwanza nimkumbushe Waziri Makonda kwamba, vyombo vya habari havisaidiwi kiuchumi, bali vinapaswa kujiendesha na kujitegemea kiuchumi.

Vyombo vya habari vya Tanzania vimekuwa masikini na hata waandishi wamekuwa masikini kwa makusudi na Serikali ndiyo imechangia wawe masikini. Kwanza sharia kandamizi zimesababisha wanahabari washindwe kufanya kazi kwa uhuru na kupata habari nzuri za kuuza ili wapate kipato.

Pili, vyombo vya habari vinadai fedha za matangazo na Serikali ni miongoni mwa wadaiwa wakubwa.

Januari 2023, aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Nape Nnauye aliunda Kamati ya Kutathmini Uchumi wa Vyombo vya Habari Tanzania, kutokana na agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, inayoongozwa na Tido Mhando. Kamati hiyo ilifanya kazi yake na kutoa ripoti kwa Serikali, lakini tatizo ni utekelezaji wake.

Leo Makonda anapokuja kusema atakwenda kuomba Sh2 bilioni kwa ajili ya waandishi wa habari, ndio anatekeleza mapendekezo ya hiyo kamati? Au ni kitu kipya? Hizo fedha zinatoka kwenye bajeti gani?

Nadhani Makonda angerejea kwenye utekelezaji wa mapendekezo wa hiyo kamati kwanza kwa sababu ilishaeleza chanzo cha tatizo na namna ya kutekeleza.

Isitoshe, Makonda ajue kwamba, tatizo sio fedha tu, nimeeleza huko juu changamoto za kisheria zinavyokwaza utendaji wa vyombo vya habari, angezitatua kwanza kabla ya kukimbilia kugawa fedha.

Watengeneza maudhui mitandaoni

Katika wizara hiyo pia kuna malalamiko ya watengeneza maudhui mitandaoni (content creators). Kumekuwa na tabia ya Serikali kudhibiti mitandao ya jamii ambayo imeajiri vijana wengi, kwa madai yasioeleweka. Kwa mfano, mpaka sasa serikali imefungia mtandao wa X (zamani Twitter), lakini kila siku viongozi wa Serikali wapo humo wanatuma maudhui yao.

Mtandao mwingine uliolalamikiwa kufungwa ni Tik Tok, ambao kwa kiasi kikubwa umejaza vijana waliojiajiri kwa kutegeneza maudhui na kufanya biashara zao huko. Sasa mitandao hii inapofungwa, biashara zinafanywaje? Ajira kwa vijana zinapatikanaje?

Inawezekana kweli kuna ukosoaji mkubwa wa Serikali kwenye mitandao hiyo na mambo mengine maovu, lakini hiyo haiondoai umuhimu wa mitandao hiyo, hivyo Serikali iache mitandao hiyo ifanye kazi na ijirekebishe inapokosolewa.

Pia watengeneza maudhui wakiwamo waigizaji, wachekeshaji, waelimishaji na wanahabari wanalalamikia kuwekewa vikwazo vya maeneo ya kupiga picha wanapotengeneza maudhui yao.

Hayo ndio mambo ambayo Makonda anapaswa kuyafanyia kazi ili kuwanufaisha Watanzania katika wizara hiyo.
 
View attachment 3529751

Hivi wanaARUSHA aliwaahidi nini vile mkimchagua kuwa MBUNGE?
 
Tanzania mnapiga macktime tu ili siku ziende. Uongozi wa kinafki.
 
makonda yule aliyevemia clouds akiwa na mitutu ya BUNDUKI anakuwaje waziri wa habari na wewe mwandishi utegemee habari njeme toka kwake?
huyu alipaswa kuwa jela siyo kuwa waziri
 
Bashite waga ana mbuli/swaga sana.. afu badae boom 💥 .. anaharibu kazi. 😁
 
Naunga mkono hoja
P
 
Duh kumbe Twitter X,TikTok,jamiiforums, internet nchi nzima etc vyote viliwahi kufungiwa na hii serikali, ni wabunge tuu ndio watakaoweza kubadilisha lakini sio hawa wa CCM,useless makonda atafanya atakachoambiwa na boss wake msitegemee jipya
 
Naunga mkono hoja
P
ukiniambia makonda kaenda pale kama MDHIBITI wa HABARI nitakuelewa.
lakini kutegemea jipya toka kwake nitakushangaa sana
Mtu huyu aliyeweza kutoka kwake na walinzi, tena wenye SILAHA ZA MOTO, wakavamia KITUO CHA CLOUDS ambacho ni mdau kwenye wizara yake leo kawa waziri wakimkera si ATAWAUWA KABISA HUYU?
Kwamba hakuna watanzania wengine wenye sifa mpaka MAKONDA ?
Shame
 
Back
Top Bottom