Makonda anaweza fanya kuamka asubuhi Bashe sio waziri wala mbunge

Chama kina nguvu kuliko serikali makonda ndie boss wa mawaziri na wakuu wa mikoa,wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi na wote wanaoteuliwa na raisi,bashe asilete ujuaji labda kama kachoka kula Kodi zetu akicheza atamfata Ally Hapi shambani
Unasema Chama halafu unamuongelea Makonda pekee. Makonda si Chama. Yaani wapambe mnakosa hekima ambayo yeye Makonda anayo. Yeye mwenyewe anasema Chama kimeelekeza hiyo ina maana hata uamuzi wa kumuondoa Bashe ikibidi utakuwa ni wa vikao na sio wa mtu. Makonda amewekwa hapo kupitia maamuzi ya vikao. Heshimuni Taasisi yenye vikao rasmi na katiba. Ingekuwa chama ni mtu kuna wengi wangekuwa hawako CCM kwasababu tu walitofautiana na kina fulani.
 

Msimvimbishe kichwa Makonda. Hicho cheo ni kidogo sana. Sana sana kilianza kujulikana wakati wa Nape. Hicho cheo kimepata nguvu wakati wa Polepole kwa sababu ya the Iron Man behind it aka JPM.

Watu bado anatake advantage ya legacy ya Magufuli ya kusujudiwa including Maza mwenyewe.
 
Hii imenikumbusha na kunitafakarisha matukio ya nyuma sana huko uyahudi, wafarisayi wakiulizwa ile dinari ina chapa ya nani? Wakajibu ya Kaisari! basi ufafanuzi ukatolewa kuwa ya kaisari apewe kaisari na Muumba apewe muumba.

Hii pia Ndg. Bashe yaweza tumika kwa busara afuate yaliyohitajika na chama kwani ndicho chenye sera, kwani hata aonapo mapungufu kwa Ndg. Makonda ayachunie kwani ndeye aliyeteuliwa na viongozi wake kusimamia ila i kwa niaba
 
Bashe ana nguvu gani ya maamuzi ndani ya chama cha CCM juu ya Makonda ?
Mkuu mwache tu huyo Dogo kumuuliza mambo makubwa zaidi ya uwezo wake. Nakumbuka mwaka 2015 wakati wa mchakato wa kumtafuta Mgombea Urais kupitia CCM, Kuna watu walidai Lowassa ana nguvu sana ndani y CCM na hakuna wa kumkata!🤣🤣🤣🤣

Mwisho wa siku alikatwa na yeye kuhamia Chadema na baadae kurudi CCM kama ng'ombe aliyekatwa mkia!
 
Dogo unaijua vizuri CCM au ni wivu wako kwa Makonda?
 
TUNAMWOMBA AAMKE TUONE KAMA ANA UWEZO HUU NI UJINGA KUMPA UWEZO ASIONAO

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Chama kina nguvu kuliko serikali makonda ndie boss wa mawaziri na wakuu wa mikoa,wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi na wote wanaoteuliwa na raisi,bashe asilete ujuaji labda kama kachoka kula Kodi zetu akicheza atamfata Ally Hapi shambani
Huwa namshangaa sana Bashe, sijui kwanini huwa ana ujuaji mwingi!
 
Siku izi amebadili kauli anasema maelekezo ya chama, ila ukimuuliza hicho chama kimekaa saa? Hawezi kukupa jibu
 
By the way
Bashe nae ni msanii tuu kama Makonda
 
Watu bado mna mawazo ya enzi hizo za rimoti.......... Rimoti betri zimeisha kaka safu inaanza kupangwa upya bila rimoti
 
Luhaga Mpina kaitwa kuhojiwa na viongozi wa CCM kata au wilaya huko jimboni kwake.😁

Huyo Nape alitumika sana tu akiwa mwenezi kumkaanga Mamvi waziwazi miaka ile kuelekea uchaguzi na kilichotokea tunakijua,itakuwa mbunge Bashe?
 

Makonda amewasha sababisha waziri gani akaondoka kwenye nafasi yake mpaka sasa?
Hawezi bado sana
 
Chama kina nguvu kuliko serikali makonda ndie boss wa mawaziri na wakuu wa mikoa,wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi na wote wanaoteuliwa na raisi,bashe asilete ujuaji labda kama kachoka kula Kodi zetu akicheza atamfata Ally Hapi shambani

Makonda si bosi ya mawaziri, wote uliowataja wana report kwa rais, makonda si rais. Na wana uwezo wa kumgomea ku report na asifanye chochote. Hana nguvu kisheria
 
Mnataka kusema Bashe si Mtanzania?
 

View: https://www.instagram.com/reel/C2u79hTq6bB/?igsh=bXpwbTlsNnF5bGNm
 
Dogo unaijua vizuri CCM au ni wivu wako kwa Makonda?
Kwanza mimi siyo dogo. Wakati tunaianzisha JF ulikuwa bado Kinder.

Makonda siyo kiongozi ni mbangaizaji tu. Simuonei wivu bali naionea huruma Tanzania kuwa na viongozi kama hawa na kuwa na supporters kama wewe.
 
Bashe zaidi ya usomali na kinga ya Rostam Aziz ana kitu gani cha ziada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…