Wanabodi,
Katika mambo ambayo nimefurahishwa nayo ni kitendo cha kiuungwana kwa RC Makonda kwenda Clouds Media na kutoa pole. Pamoja na msuguano wake na Ruge, tofauti hiyo leo haijajionesha wazi. Nampongeza sana Ruge, Kijana huyu anaonekana kuwa na busara sana katika jambo hili ambalo ni gumu kwake na timu yake.
Mara zote, hata kwetu kijijini,matukio ya huzuni kama misiba ndio huwaunganisha watu zaidi kuliko kuwagawa. RC Makonda wakati anaondoka amempa ahadi Boss Kusaga kuwa amewaongezea lisaa limoja la Fiesta. KITENDO HICHO NI CHA KIUUNGWANA hasa katika kuwapa ari vijana katika kupambana na umaskini na kukuza vipaji. Hawahawa ndio watatusaidia ikifika 2020 wakati wa kampeni zetu nchi nzima bila kujali itikadi za vyama. Tuwapendeke, tuwasaidie.
Achilia mbali positive impact za FIESTA, ni kweli kuna kelele na mambo mengine ya kihalifu. Ninaamini kuwa likipangwa vizuri jambo hili, naamini RC Makonda ataruhusu jambo hili la Fiesta lifanyike hadi asubuhi. Ombi Maalum kwa RC Makonda, waruhusu Clouds wapige Fiesta kama zamani. Wasaidie ili angalau vijana watakaopanda jukwaani wapate kipato chao wakatunze familia zao. Wewe ni kama MZAZI hapa Dar es Salaam. Licha ya kuwa na umri mdogo ila una nguvu katika mfumo wa utawala. Ukizingatia kuwa bado una safari ndefu katika maisha na vijana wenzako hao, hebu wasaidie kutimiza ndoto zao kama ulivyosaidiwa wewe ona hapa chini ulivyoelezea...
Fanya kama ulivyofanya kipindi cha nyuma. Ondoa tofauti zilizopo kati yako na wao. Dereva naamini anasumbuka abiria wanapomsumbua anapoendesha gari lake hasa katika kipindi hiki ambacho vuguvugu la kupambana na 'mafisadi' linaendelea.Nimekusikiliza hapa ulivyotimiza ndoto zako. Hebu wasaidie hao jamaa. Mungu naamini atashusha baraka zake kwako. Kawaombee kibali hata kwa Mh. Rais, naamini anavyowapenda, atawaruhusu kwa siku hiyo moja kufanya hiyo event.
Mungu ibariki Tanzania,
Nelson,
Dar es Salaam
22/11/2017