Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana alifanya ibada maalum kanisani kwa ajili ya makontena yake yenye samani za shule yanayoshikiliwa na TRA

Katika ibada hiyo Makonda alionya watakao nunua makontena yake watapata laana kali

Pia aliwarushia dongo TRA akisema ni watu wabaya wasio na huruma na kudai kuwa wanamchukia Makonda

"Kama wanachukia Makonda waondoe nembo ya majina yangu kwenye makontena hayo" alisema Makonda

Ni mara nyingine viongozi wa serikali wanasuguana na taasisi za serikali katika kutekeleza majukumu yake huku kiongozi huyo wa mkoa akihisi anaonewa na ni wivu unaofanywa na TRA kisa anafanya vizuri katika mkoa wake

Juzi Paul Makonda alikaririwa na vyombo vya habari kuhusu kupigwa mnada makontena yake,akisema yeye hatishiki na ni mlima hawezi kuyumbishwa na wale wasiomtakia mema katika harakati zake za maendeleo ya Dar es salaam

Kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kuwa Makonda analaumu serikali kumhujumu na hakubaliani na TRA na mambo inayomfanyia

pole sana kiongoz mungu atakuttea na makontena yatatoka kwa jina la yesu
 
huyu jamaa anafanya mambo ya ajabu halafu anategemea huruma.
refer matukio yake ya nyuma
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana alifanya ibada maalum kanisani kwa ajili ya makontena yake yenye samani za shule yanayoshikiliwa na TRA

Katika ibada hiyo Makonda alionya watakao nunua makontena yake watapata laana kali

Pia aliwarushia dongo TRA akisema ni watu wabaya wasio na huruma na kudai kuwa wanamchukia Makonda

"Kama wanachukia Makonda waondoe nembo ya majina yangu kwenye makontena hayo" alisema Makonda

Ni mara nyingine viongozi wa serikali wanasuguana na taasisi za serikali katika kutekeleza majukumu yake huku kiongozi huyo wa mkoa akihisi anaonewa na ni wivu unaofanywa na TRA kisa anafanya vizuri katika mkoa wake

Juzi Paul Makonda alikaririwa na vyombo vya habari kuhusu kupigwa mnada makontena yake,akisema yeye hatishiki na ni mlima hawezi kuyumbishwa na wale wasiomtakia mema katika harakati zake za maendeleo ya Dar es salaam

Kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kuwa Makonda analaumu serikali kumhujumu na hakubaliani na TRA na mambo inayomfanyia
INASIKITISHA sana serikali yaani TRA kumhujumu Makonda ili hali ni jasho la wana DIASPORA waliojitolea kwa ajili ya maendeleo ya wa Dar es salaam , watu wamejinyima ili kuletea watanzania maendeleo na sasa yanakwamishwa kwa sababu ya wivu sie wana diaspora mnatuvunja moyo kabisa .Tuanaomba kwa dhati Rais aingilie kati jambo hili kwa mstakabali wa maendeleo ya Mkoa wa Dar es salaam. Chonde Mheshimiwa Raisi tuko chini ya miguu yako tusaidiwe tumalize jambo hili mkoa wa Dar ufaidi matunda ya wana Diaspora.
 
Kwan makonda ni nan hasa kias kwamba awanyime uhuru taasisi kubwa ya kiserikali kufanya kazi zake kwa uhuru?

Kuna mambo mengine viongoz Wetu wanafanya kias kwamba unajiuliza uyu mpaka leo anafanya nin kwann asipangiwe kazi nyingine ya kufanya au apigwe tuu chin..!!!!

Uyo jamaa kwa jinsi magu anavyo mlea ipo siku atakuja toa kauli za dhiaka kwa rais na uwongoz wake....

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoto anapotishia watu wakubwa ni dhahiri kuwa huyo mtoto yupo aliye nyuma yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mcha Mungu hata mmoja aliye mwepesi kuomba laana imfikie adui yake. Ni shetani tu na wafuasi wake ndo wenye tabia na roho ya namna hii sababu ya kujwa na kiburi kilichopitiiza. Lakini ukiona mtu anaanza kusema sawa tu Mungu anakuona ujue anaashiria kukata tamaa na ni dalili za kushindwa na kulemewa katika vita. Kuna siku niliwahi kuandika humuhumu ya kuwa watu wengi tu wanakamatwa na kuteswa polisi na kupelekwa mahakani kwa madai ya kutoa lugha za uchochezi lakini huyu jamaa siku zote amekuwa akiwatukana watu hadharani kuwaita wajinga wapumbavu na kuwadharau hata watu wazima na hachukuliwi hatua. Nadhani sheria za Tanzania sio moja kwa kila mtu, yaani nataka kusema watanzania wote tuko sawa mbele ya sheria lakini wengine wako sawa zaidi. Sina hela tu, ningekuwa nazo ningeenda kununua vitu vyote hivyo niione hiyo laana ya Mungu wake mpenda visasi na uonevu. LEO NIMEPATA SOMO ZURI SANA. KUMBE KILA BINADAMU HUWA ANATENGENEZA MUNGU WAKE MWENYEWE KULINGANA NA MAHITAJI YAKE!!!!! SITASHANGAA KUSIKIA NA MAJAMBAZI NAO WANAMUOMBA MUNGU WAO KABLA YA KWENDA KUKABA
Naomba nikupe Live Like!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umleavyo....... wakati Rais anaambiwa kuhusu huyu mtoto wake akaona anapangiwa na kufundishwa kazi, ona sasa Mungu alivyo mkubwa mbona hapa anataka kutuonyesha unafiki wetu sisi kama binadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapinzani uchwara walikuwa wanasema ati makontena yamejaa samani za majumbani pamoja na Toyota SUV moja,lakini kwa sasa yameshafunguliwa wamekuwa wakimya sana...Wapinzani Uchwara acheni fitna.
Umeyaona? Au ndio nawe ni mmoja wa mandundame yaani wasaidizi wa mganga so unajaribu kuagua? Swali ni kwanini yaje kwa jina lake na sio ofisi anayohudumu? Au ofisi haina anwani? Na kwanini yasije kwa jina la wizara anayohudumu pia? Kuna sababu nyingi za msingi ambazo sheria za kodi zinashindwa kumpa exemption na badala yake inabidi ayalipie kwa vyovyote bila kuingiza visingizio vya huduma ambazo hakuombwa na jamii bali mahaba yake!
Na ikitokea kukawa na double standard akasamehewa basi hata ile mizigo ya kitaasisi hasa za kidini na kijamii nazo zipewe msamaha! Alipe kodi!
 
Back
Top Bottom