Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Ha ha ha ha,naona Mh.RC Makonda kashikwa pabaya pia gwajima alisha mvua vyeo vyote na alimpa muda atubu,sasa naona yanaelekea kutimia
 
Wewe ni mwansheria uchwara kama uchwara yoyote yule. Mhalifu aliyetishia vyombo vya serikali vinavyotekeleza majukumu yake anaombwa? Siyo kuwa anachukuliwa sheria?
Nashangaa sana, hizi ni taratibu gani za kiutawala!? Makonda ni mtumishi wa Serikali kwa ngazi ya u RC. TRA ni chombo cha serikali cha ukusanyaji mapato yake. Huu mgongano wa waziwazi kati ya RC na TRA ni maadili kweli ya utendaji kazi serikalini? Inafikia hadi taasisi moja(hata u RC ni taasisi pia) inatamani na hakika inatishia kufanya hujuma kwa taasisi nyinginge ya serikali na mamlaka husika zinaona ni jambo la kawaida na wananchi akiwemo mwanasheria msomi Petro E. Mselewa anaona ni jambo dogo tu! Eti Makonda "aache kuwatisha kimaombi wanunuzi wa makontena', halafu basi liishie hapo!

Mkuu wa mkoa kujitokeza hadharani na kutoa wito hayo makontena yake yasinunuliwe na mtu yeyote tena kupitia mnada halali wa taasisi halali ya serikali sio jambo la kiuhalifu hilo? Sio uhujumu uchumi huo? Mnatuonyesha nini sisi kama wananchi!? Siamini kwakweli kama viongozi wa juu hasa mamlaka yake ya uteuzi wanaliona hili na hawachukulii kama ni serious crisis( kuna element ya criminality ndani yake) , na kama mamlaka za juu yake hazilioni jambo hili basi amakweli safari hii Watanzania kama Taifa tumepatikana!

Nakuuliza Mselewa, Makonda anaweza kwenda mahakamani kwa capacity yake ya u RC kuishtaki TRA? Yaani Serikali iishtaki serikali? Pengine angekua mtu binafsi angeweza kwenda kushtaki mahakamani kama ana hoja na hakika zipo kesi nyingi baina ya watu, makampuni na taasisi mbalimbali dhidi ya TRA na huo ndio utaratibu wa utawala wa sheria. Hivi atokee mtu binafsi au taasisi hasa ya kidini itoe wito na kufanya kampeni za kupinga shughuli halali za serikali angevumiliwa!? Mamlaka ziache hizi double standards mnajijengea wenyewe chuki kwa wananchi
 
conformation. kilichomo kwenye makontena ya makonda pale bandarini ni fenicha za hotel yake hapo mwanza.. ndo mana kil siku tunasema huyo anayeitwa mwadilifu sio mwadilifu sio hivyo.tuone kwenye hili atafanyaje?
unajua maana ya bajeti kiongozi?
 
Mkuu, iko wazi kuwa Makonda hawezi kuishtaki TRA wala Serikali. Anachokifanya ni kutaka Rais aseme jambo kuhusu jambo hilo. Ni kama anasaka huruma ya Rais na wananchi, hasa waumini wenzake.
 
nazani izo containers zitakuwa na magendo kwanini akataze TRA kupiga mnada?
 
naanza kumuona bashite akitaKAFARI[emoji37] anaanzaje maisha ya uswazi.
jinsi anavyosakamwa kilakona huyu ataishia kusikoeleweka[emoji125] [emoji125] [emoji125]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waislam tunaomba msome tena ile albadiri[emoji4][emoji4] I’m happy with the results from the first albadiri[emoji4][emoji4]

Watu wanajichanganya changanya tu ovyo saa hizi
 
Kwa Kawaida mimi huwa mvivu kuandika lakini kwa hili uvivu umenitoka. Ni jambo la kushangaza kwa kiongozi mwandamizi wa ngazi ya ukuu wa mkoa , kulalamikia serikali ambayo yeye ni mmojawapo wa wasaidizi wa raisi. Kama ni kweli yeye kama mkuu wa mkoa hajatendewa haki au kwa maana nyingine kadhulimiwa, inakuwaje kwa mwananchi wa kawaida? Hii inaleta picha gani kwa utawala huu wa awamu ya tano ambapo wananchi wengi tumetokea kuiamini? Kiongozi unapaswa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi yetu na sio kulalamika ovyo, na kujiona kwambia wewe huko juu ya katiba. Kwa hili tafadhali mweshimiwa raisi chukua hatua , hatuwezi kuwa na viongozi wa aina hii.
 
Jamaa hana ujasiri wowote mkuu.ni kwamba yeye ni mtanzania pekee mwenye kinga ya kutokuguswa hata angefanya jambo gani baya.kuna invisible power inayomlinda.otherwise alitakiwa awe amefukuzwa mara tu alpoitoa hiyo kauli ya vitisho.
 
Mkuu mbona mpango kasema vizuri tu kwamba kisheria, ofisi za tawala za mikoa hazipewagi misamaha? Inamaana hata kama angeweka RC Dar, bado ingetakiwa kodi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Angeandika wizara ya Elimu au hata Tamisemi, tatizo ni misifa ndiyo imemponza angeomba hata ushauri kabla nyaraka za mizigo hazijaandaliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…