muda wa ukombozi
Senior Member
- Jun 28, 2013
- 129
- 118
Ni kitu cha kushangaza kuona uwepo wa taarifa ya familia moja yaani watoto wa baba mmoja kugombana hadharani kwa vitu vidogo ambavyo vinaweza kumalizwa aidha na wakubwa zao kiumri au wazazi wao, hapa namaanisha baba au mama ndani ya familia.
Ugomvi unao dharirisha familia, ugomvi unao ruhusu majirani kuwasema vibaya,
unaonesha hakuna mawasiliano mazuri ndani ya familia moja.
Kwanini haya yanatokea, ni uoga, kumuogopa baba yao au ni misimamo tu.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Makonda aliomba msaada kutoka Kwa watanzania wanaoishi marekani thamani pamoja na vifaa vya mashuleni, vifaa hivyo vimekuja lakini vimekwama bandarini Kwa sababu ya kodi, waziri wa fedha pamoja na mamlaka ya mapato wanao shughurika na kodi wametoa Kauli yao kwamba vifaa hivyo vimekuja lazima vilipiwe kodi na Kama sivyo vitapigwa Mnada Kama sheria inavyotaka.
TATIZO NINI?
vifaa hivyo ingawa ni vifaa kwa ajili ya mashuleni, lakini havikuja kwa Jina la wizara husika, ila vifaa hivyo vimekuja kwa jina la Paul Makonda, hii inamaana kwamba ni vifaa vyake yeye mwenyewe anataka atoe msaada yeye mwenyewe au labda kwa niaba ya hao rafiki zake wa ughaibuni, sasa kwa utaratibu wa sheria za kodi kuna vitu ambavyo vinamsamaha lakini Mkuu wa Mkoa hana msamaha wa kodi kwa vitu vyake anavyoagiza au kupewa toka nje ya nchi labda kwa maelekezo toka kwa mwenye madaraka makubwa kuliko yoyote ndani ya nchi.
KIPI KIFANYIKE!
Mkuu wa Mkoa aidha alipe kodi, au vile vifaa vikiwa palepale bandarini aandike barua kwa waziri wa fedha kupitia mamlaka ya mapato, akivitoa vitu hivyo kwa wizara husika, wizara ya elimu, akielezea ujio wa hivyo vitu hapa nchini kwa lengo la kutokomeza mazingira magumu mashuleni, sasa wizara husika ndiyo itashughurika na kodi kama kuomba isamehewe au kulipa, kwasababu bajeti ya kununua thamani mbalimbali mashuleni naamini ilikuwepo kama kuna huu unafuu wanaweza kulipa kodi.
HAIWEZEKANI.......!!!!!!!
haiwezekani husamehewe kodi kwa vitu ulivonunua au kupewa iwe unataka kutoa msaada au kugawa bure kama sheria haijatoa maelekezo tofauti haiwezekani ata umwambie prezo hiyo sahau, sio kwa jina lako, waziri na mamlaka ya mapato wako sahihi.
SWALI LA KUJIULIZA....?
hivi kweli mmeshindwa kuwasiliana kiofisi na kuyamaliza kiofisi hadi mnaongea kwenye madhabaho ya kanisa, kwenye mitandao ya kijamii?
Mmeshindwa kulifanya hili jambo kuwa ni la ndani kwa kupeana maelekezo kupitia vi- memo?
Sent using Jamii Forums mobile app