Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Kwahiyo wewe una akili kuliko mawaziri sio?
 
Tusipindishe sheria kwa mgongo wa huruma kila mtu akija kwa njia hiyo nani atalipa kodi?

Kwanini hujawahi kutetea kodi ambazo zinawaumiza wananchi wa kipato cha chini na hata kupandisha gharama za maisha yao leo unamtetea mtu mmoja ambaye kwa mujibu wa taratibu amekiuka na sheria inachukua upande wake kwanini kwa huyu sheria unataka iwe na huruma kwa wengine isiwe nayo?

Acha sheria ifuate mkondo wake ili na wao wafeel namna inavyoumiza huenda watapata uelewa wa kutunga sheria vizuri
 
Sheria ifuatwe no matter what.
 
Kwa nini mwanzo alikataa makontena si yake halafu baadae ndio aje kukubali. Makonda anafanya kazi lakini hapa kachemka, sasa kila mtu akileta mizigo kwa jina lake akijidai ni msaada na asemehewe kama Makonda sheria itakuwa imetupwa mbali sana. Sheria ichukue tu mkondo wake kama kawaida. Hatufurahii viuzwe lakini Makonda mwenyewe alishaonyesha mashaka kipindi alipoyakana.
 
Mkuu Techinically umeandika jambo zito na lenye kuhitaji akili zinaoongozwa na utaifa kwanza.

Ni kweli kabisa RC alikosea kwa kutotengeneza mazingira ya kuhakikisha huo mzigo unakombolewa bandarini, kabla hata meli haijaondoka kutoka huko ilipotoka.

Tunafanya masikhara kwenye mambo ya maana na tunapenda kujifanya tupo makini kwenye mambo ya kipuuzi. Tumeukumbatia ujinga mpaka tunashindwa kutofautisha kati ya akili zenye faida na ujinga wenyewe.

Hizo furniture zingeleta kitu fulani kipya kwenye shule za Dar lakini kama kawaida siasa za kipumbavu ndio zinapewa nafasi.
 
Mkuu technically kwanza nakusalimu. Pili, nakushukuru kwa mada yako. Tatu, nami naomba nichangie kuwa Waziri wa Fedha yuko sahihi katika aliyoyasema kwakuwa ameyasema ya kweli. Ametaka sheria ifuatwe na kama kodi ilipwe au mnada ufanyike. Waziri Mpango amesema yaliyo ya kweli. Kwanini makontena yaliyoletwa kwa ajili ya mkoa/ofisi ya Mkuu wa Mkoa yabebe jina binafsi la Mkuu wa Mkoa? Kodi ilipwe au mnada uendelee. Yeye aendelee na 'maombi' yake ya kulaani.
 
Dunia ya fake news!
Ogernized slave masters criminal gangs in a government coverage! PERIOD!
 
Siku nyingi sikuoni hapa jukwaaani mkuu, karibu tena
 
Kama ni kweli vifaa hivyo ni kwa ajili ya shule, serikali ifanye yafuatayo:
1. ifuatilie kujua vilikotoka na staili iliyotumika kuvisafirisha;
2. Makondo ale kiapo kwamba vifaa hivyo ni kwa ajili ya mashule ya Dar es Salaam ili kuepuka kugeuziwa kibao;
3. ivipe msamaha wa kodi;
4. ihakikishe kwamba vinagawiwa vyote mashuleni kwa kumshirikisha yeye (Makonda).
Vinginevyo, mivutano hii itagawa chama na serikali. Kumbukeni tunajenga nyumba moja na hatuna sababu za kugombania fito!
Jitafakarini!
 
Ignorance ya Makonda kisiwe kisingizio cha kutokufuata sheria. Makonda anajulikana kuwa sio muadilifu kwani alipiga sana enzi za Home Shopping Centre hivyo ni vigumu kumuamini kuwa kweli alikuwa na nia njema na hayo makontena. Toka akiwa DC anajua wazi kuwa kama hayo makontena yangeletwa kupitia registered NGO na sio jina lake , yangeweza kuingizwa bila Ushuru!! Lakini Makonda for reasons best known to the powers that be thinks that he is above the law!! Rais kuingilia sakata hili na kuruhusu sheria kuvunjwa atakuwa ana create a disastrous precedent kwa watendaji wa serikali.
 
Mkuu, sithani kwa kweli TRA hawajui wanachokifanya, aidha, sina hakika kama TRA hawajajiridhisha kuhusu huo mzigo. Hata hivyo, ni kwa nini hakuingizwa kwa jina la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam au Idara ya Elimu, Mkoa wa Dar es Salaam. Ninachofahamu ni kuwa kuna tofauti kati ya Paul Makonda na Mkuu wa Dar es Salaam. Paul Makonda ni mtu ilhali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni Taasisi. Mzigo kwa ajili ya Paul Makonda ni lazima uwe cleared na Paul Makonda lakini Mzigo wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa cleared na Afisa Ugavi wa Mkoa.
 
Jamani eh. Kodi nayo ikilipwa si itaingia uko uko katika kusaidia elimu, kununua madawa hospitalini, kujenga miundombinu n.k sasa kwanini isilipwe ili ata watu wasio wakazi wa Dar es Salaam wafaidike

Sent from my SM-G610F using Tapatalk
 
namimi naongeza na alaaniwe kabisa atakae vinunua.
Kwa mujibu wa sheria ya karma, hakuna laana yoyote inayoweza kumpata mtu aliyenunua mali kihalali hata kama mali hiyo ni ya wizi au dhuluma, ila laana humpata yule aliyedhulumu, hivyo kwa case ya containers za Makando, laana itamhusu anayetoza kodi vitu vya bure vya masikini waalimu wetu!.

P.
 
Mbona ni wepesi kusahau?Mali iliyondani ya makasha imetolewa kwa hisani ya watanzania waishio ughaibuni kama mchango wao wa kuboresha elimu mkoa wa Dar-es-Salaam.
Mpaka hapo ni sawa,lakini kwa kuwa aliewezesha mchakato mzima ni Makonda shida ndio hiyo,witch hunt.
Ni juu ya serikali kushirikiana badala ya kulumbana mnatia kichefuchefu.
 

Prove beyond reasonable doubt kwamba ali aim kuvigawa hivyo vifaa ktk shule dsm, usifikiri serikali haina akili kama ya DAB,watu wanaona sana ujinga wa DAB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…