Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda amesha tuonesha mashaka kwa jina lake tuu lina utata mpka sasa halijulikani lipi ni la kweli. Tunawezaje kuamini Makonda ktk mambo makubwa namna hii yanayo husu Taifa ikiwa ya kwake yamemshinda ?

Hatuwez mwacha aendelee kughushi nyaraka wakati ana kesi ina msubiri ya jinai ya kufoji jina amezoea huu mchezo wake sasa mwishoo ebo !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mambo mengine yanatia kinyaa!

Makonda ali-mobilize watu(diaspora) kuchangia samani za shule. Wito ukaitikiwa kwa kuchangia na kuzisafirisha hadi Dar. Aliye-mobilise ni Makonda, ametumiwa Makonda akazikabidhi katika shule za serikali.

Suala hapa kama serikali ina wasiwasi na nia hii ya Makonda basi ifuatilie konteina moja moja kuhakikisha mizigo yote inagawiwa mashuleni na si vinginevyo!

Mara nyingi mizigo mingi inayotumwa kutoka nje kwenda kwenye taasisi za serikali jina la mtu wa kufuatilia (Attn. so and so) huandikwa! Hii inakuwa rahisi kwa mtumaji kupata uthibitisho wa mizigo kufika!

Sasa ni nini watu wenye PhD kinawachanganya hapa?
 
Waziri ashikilie hapo hapo, huu ni ujanja ujanja wa Bashite, kwa kuisingizia waliamu na wanafunzi, tutaamini vipi?? Ndani ya zile fenicha Kuna vitanda, viti vya kuzunguka, viti vingine Kama vya kwenye hotel, haiwezekani kabisa, Kuna wafanya biashara wakubwa walikuwa wanamtumia huyu Bashite kupitisha Mali zao ili kukwepa kodi. TRA sio wajinga, mchezo mzima wanaujua. Waziri sio mjinga anajua Kila kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu ndicho nashangaa watu wanavyonishambulia hapo juu lakin ukweli unajulikana kabisa hivyo vitu n vya shule
 

Mzigo ulikuwa ni kwa ajili ya Hoteli ya DAB Mwanza
Stuka
 
Pia makonda auambie uma ni msaada toka taasisi au shilika gani umetoka muzigo huu
 
kauli sahihi.ingekuwa.
SISI KAMA TRA TUNATOA MSAMAHA WA KODI KWA MAKONTENA HAYA.
KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RC WA DAR.KATIKA KUKUZA NA KUENDELEZA ELIMU.
KWA WATOTO WALIOPO MKOA WA DAR.

Sent using Jamii Forums mobile app
 



Serikali moja,viongozi wamoja,vifaa kwa ajili ya serikali hiyo hiyo, shida iko wapi sasa.
 
Ndugu sheria zinasemaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asee technically nimeona bandiko lako. Ila nakuomba usiwe unaendeshwa na matakwa ya mtu.
Ndio maana tunataratibu na kanuni. Kila mtu anaweza akafanya anavyotaka kufanya Makonda.

Wezi ni wengi na wanambinu nyingi sana.
 
Hakuna hata ya kubadili shelia kisa tu Makonda kasema hivyo.
Sheria zifuatwe na kama zinabadirishwa sio kwa muziko huu.
 
Aliagiza kama makonda au mkuu wa mkoa?
Kwa nini mwanzo alikataa?
Unafikiri kwa nini anatishia watu na laana?
Kwani anajua atakaye vinunua kwa mnada ataenda kugawa kwenye shule ipi?

Acha njaa za muwatetea wezi dogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
serikali inajua kila kitu, haijakurupuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda mwenyewe kaikataa hiyo mizigo anasema si yake.

Serikali ya Tanzania na michezo yake ya kuigiza isiyoisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…