Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

hawa wanaotetea haya ya makonda ni walewale ambao siku zote wapo mtanadoni kumsifia kwa kila kitu. wanaishi kwa ujira wa kumsifia makonda kila kukicha hata kwa vitu vya kijinga kabisa!
 
Issue kubwa kuna sheria ya kodi "income tax Act" ndiyo inayotoa taratibu za ulipaji kodi kwahiyo hapo ni kuangalia upande Gani? unafuata sheria na upande gani unalazimisha kwa kutumia mamlaka zao...........
Ila mwisho wa siku tujikumbushe kuwa katiba yetu inatuambia nchi inafuata utawala wa sheria na sio matamko.......na Rais wetu utumia nguvu nyingi sana kutueleza watz kuhusu hilo.
Ngoja tuone mwisho wa picha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kwa mlio walimu mtanielewa ninaposema waziri kakurupuka wala hazijui changamoto za elimu
ukisikiliza kwa umakini kwenye hotuba yake ya juzi utagundua kabisa aelewi anachokiongea...

Anaongelea maswala ya elimu bure kitu ambacho ni nje kabisa ya mada ya makontena

swala hapa ni vifaa kwa ajiri ya kusaidia elimu ya dsm ambayo ina changamoto nyingi ikiwa na mrundikano wa wanafunzi na mambo kibao

Makonda inawezekana kuna sehemu alikosea katika mchakato huo lakini serikali walitakiwa kuwa wajanja wangeruhusu kwanza vitu viingie ndio waanze kuvimonitor wapate ushahidi wa kutosha ndio waje kumtuhumu.

matokeo yake wananchi nao wameyabeba na kusahau watoto wao ndio wanakaa chini milele
mimi niko na ushahidi kabisa nilienda shule moja na taasisi fulani kutoa msaada wa computer lakini unakuta walimu stafu viti tu vya kukalia haviwatoshi hii ni aibu kama mwalimu hana kiti stafu mwanafunzi je darasani itakuwaje?

tukiweka siasa pembeni Makonda yupo sahihi kabisa na ana nia njema ingawa anaweza kuwa kafanya makosa kutumia jina lake kwa ushauri mbovu wa watendaji waliopo chini yake lakini naamini tatizo letu la elimu ni kubwa mno kuliko jina la makonda kuwa kwenye makontenana hili swala tunalibabe kishabiki sana kama kawaida yetu...

kwamba mimi ni chadema Gambo akifiwa na mzazi wake nashangilia, mimi ni ccm Sugu akipata msiba nashangilia upuuzi mtupu.

Hivi waziri anavipiga mnada vitu vya shule za dsm watu tunashangilia leo halafu kesho jangwani secondary inakuwa ya mwisho tunaanza kumponda makonda ...

Hivi vitu vikinunuliwa na wafanya biashara sisi wananchi wa kawaida tutafaidika vipi direct kama ambavyo tungeviona kwenye shule zetu? namimi naongeza na alaaniwe kabisa atakae vinunua.

"Form four wanakaribia pia kuanza mtihani msisahau kuleta mrejesho hapa wa shule za umma"

Ni kweli Makonda alikosea kwenye kuandika Bill of lading -ila, kwa kuwa inaeleweka vifaa vilikuwa kwa ajili ya shule za Dar es Salaam, busara ilikuwa ni kupokea na kukaa na Makonda kumwelimisha. Halafu serikali ingesimamia kuhakikisha kuwa beneficiaries wa vifaa hivyo ni exclusively shule za Dar es salaam
 
Kwa hili Dr.Mpango na Wasaidizi wake wapo Sahihi,alafu mbona zile Samani Ukizichungulia kwenye lile kontena ni kama za Saint ..., Shule ya msingi Gongolamboto 'B' au Shule ya Msingi N'zasa pale Mbagara hata siku tatu hazikai, kiti cha laki 6 mjini, labda Bunge Primary School au Muhimbili P/School
 
Kama ilikuwa vifaa vya shule mbona Wizara ya Elimu haikuhusishwa
Acheni kutetea uovu
bashite anacheza michezo michafu mingi tu.Wakati umefika wa kuwekewa speed governor
Enough is enough!
 
Mkuu technically kwanza nakusalimu. Pili, nakushukuru kwa mada yako. Tatu, nami naomba nichangie kuwa Waziri wa Fedha yuko sahihi katika aliyoyasema kwakuwa ameyasema ya kweli. Ametaka sheria ifuatwe na kama kodi ilipwe au mnada ufanyike. Waziri Mpango amesema yaliyo ya kweli. Kwanini makontena yaliyoletwa kwa ajili ya mkoa/ofisi ya Mkuu wa Mkoa yabebe jina binafsi la Mkuu wa Mkoa? Kodi ilipwe au mnada uendelee. Yeye aendelee na 'maombi' yake ya kulaani.
Swali ni je kati ya Makonda na hao waliotoa msaada wa hivyo vifaa nani amekosea kwa kuandika jina la mtu binafsi?
 
Mkuu, sithani kwa kweli TRA hawajui wanachokifanya, aidha, sina hakika kama TRA hawajajiridhisha kuhusu huo mzigo. Hata hivyo, ni kwa nini hakuingizwa kwa jina la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam au Idara ya Elimu, Mkoa wa Dar es Salaam. Ninachofahamu ni kuwa kuna tofauti kati ya Paul Makonda na Mkuu wa Dar es Salaam. Paul Makonda ni mtu ilhali Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni Taasisi. Mzigo kwa ajili ya Paul Makonda ni lazima uwe cleared na Paul Makonda lakini Mzigo wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa cleared na Afisa Ugavi wa Mkoa.

GHARAMA YA KUAGIZA MZIGO UGHAIBUNI SI INGETOSHA KUTENGENEZA SAMANI HIZO HAPA BONGO? TENA KWA MKOA WA DAR TENDA WANGEPEWA MAGEREZA WANGETENGENEZA.Mie nahisi kuna jambo ndani yake
 
Tutakapoanza kupindisha au kuzi-ignore sheria kwa sababu yeyote ile, then tutakuwa tuna-set precedent ambayo itakuja kusumbua sana huko mbele.. Mzigo huo ulipe kodi stahili, na kama imeshindikana basi uuzwe kwa mnada, ili wengine waone how serious serikali ilivyo katika suala la kukusanya mapato..
 
Mkuu Techinically umeandika jambo zito na lenye kuhitaji akili zinaoongozwa na utaifa kwanza.

Ni kweli kabisa RC alikosea kwa kutotengeneza mazingira ya kuhakikisha huo mzigo unakombolewa bandarini, kabla hata meli haijaondoka kutoka huko ilipotoka.

Tunafanya masikhara kwenye mambo ya maana na tunapenda kujifanya tupo makini kwenye mambo ya kipuuzi. Tumeukumbatia ujinga mpaka tunashindwa kutofautisha kati ya akili zenye faida na ujinga wenyewe.

Hizo furniture zingeleta kitu fulani kipya kwenye shule za Dar lakini kama kawaida siasa za kipumbavu ndio zinapewa nafasi.
Kwa hiyo waziri kusimamia kiapo chake leo hii imekuwa upuuzi? Yalaaaaaa!
 
Hotel yake ya mwanza ndio mwathirika wa kwanza kwa kukosa hizi furniture. vitanda ni vya walimu? sofa?
 
GHARAMA YA KUAGIZA MZIGO UGHAIBUNI SI INGETOSHA KUTENGENEZA SAMANI HIZO HAPA BONGO? TENA KWA MKOA WA DAR TENDA WANGEPEWA MAGEREZA WANGETENGENEZA.Mie nahisi kuna jambo ndani yake
Shtuka, huenda kuna vifaa alipewa msaada kutoka huko USA kwa ajili ya shule za Dar, lakini yeye akajiongeza kwa kachangnya na vya kwake anataka aingize kwa mgongo wa msaada. Serikali haiwezi kukutaa kuingiza bure kama kweli ni msaada, mbona Wizara zinaingiza magari ya misaada bure iweje wakatae vifaa vya shule tena kipindi hiki cha elimu bure ambacho wadau wanahitajika katika kusaidia juhudi za kutoa eleimu bure.
 
Kwanza kwa mlio walimu mtanielewa ninaposema waziri kakurupuka wala hazijui changamoto za elimu
ukisikiliza kwa umakini kwenye hotuba yake ya juzi utagundua kabisa aelewi anachokiongea...

Anaongelea maswala ya elimu bure kitu ambacho ni nje kabisa ya mada ya makontena

swala hapa ni vifaa kwa ajiri ya kusaidia elimu ya dsm ambayo ina changamoto nyingi ikiwa na mrundikano wa wanafunzi na mambo kibao

Makonda inawezekana kuna sehemu alikosea katika mchakato huo lakini serikali walitakiwa kuwa wajanja wangeruhusu kwanza vitu viingie ndio waanze kuvimonitor wapate ushahidi wa kutosha ndio waje kumtuhumu.

matokeo yake wananchi nao wameyabeba na kusahau watoto wao ndio wanakaa chini milele
mimi niko na ushahidi kabisa nilienda shule moja na taasisi fulani kutoa msaada wa computer lakini unakuta walimu stafu viti tu vya kukalia haviwatoshi hii ni aibu kama mwalimu hana kiti stafu mwanafunzi je darasani itakuwaje?

tukiweka siasa pembeni Makonda yupo sahihi kabisa na ana nia njema ingawa anaweza kuwa kafanya makosa kutumia jina lake kwa ushauri mbovu wa watendaji waliopo chini yake lakini naamini tatizo letu la elimu ni kubwa mno kuliko jina la makonda kuwa kwenye makontenana hili swala tunalibabe kishabiki sana kama kawaida yetu...

kwamba mimi ni chadema Gambo akifiwa na mzazi wake nashangilia, mimi ni ccm Sugu akipata msiba nashangilia upuuzi mtupu.

Hivi waziri anavipiga mnada vitu vya shule za dsm watu tunashangilia leo halafu kesho jangwani secondary inakuwa ya mwisho tunaanza kumponda makonda ...

Hivi vitu vikinunuliwa na wafanya biashara sisi wananchi wa kawaida tutafaidika vipi direct kama ambavyo tungeviona kwenye shule zetu? namimi naongeza na alaaniwe kabisa atakae vinunua.

"Form four wanakaribia pia kuanza mtihani msisahau kuleta mrejesho hapa wa shule za umma"
wenye vyeti feki utawajua tu.
wanafananaaaa weee!
 
Back
Top Bottom