Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Mbona hatuulizi ni kwa nini basi Makonda aliweza kutoa contena 16 kwa jina lake kutoka 36 za awali. Na je hizo 16 amezigawa wapi? Anayejua hili atuambie!
 
Mkiendekezi hii tabia, ipo siku mtu ataingiza mizigo yake kwa style hii ambayo kwanza hakuna mwenye uhakika kama vifaa hivyo vyote kweli vinawafia walengwa au ni janja tu.

Na kwa jinsi jambo hili linavyokwenda mpaka sasa, ni dhahiri unahitajika uchunguzi wajulikane ni kina nani walituma vifaa hivyo na shule gani hasa zilizolengwa kupewa hiyo misaada.

Hili jambo lina ukakasi unaohitaji uchunguzi maana huenda si kila kifaa kitaenda kutolewa kama msaada.

Na nikwambie tu, vifaa hivyo vingekuwa vimeingizwa na mtu kutoka upinzani, vingeshapigwa mnada siku nyingi tena huyo Makonda angeweza hata kuingilia viuzwe haraka japo kisheria hahusiki.

Tena namshauri waziri Mpango awe makini na kama kuna mtu atamshinikiza atoe msamaha,basi ahakikishe mtu huyo anatoa agizo kwa njia ya maandishi vinginevyo ajiuzulu kwani ipo siku anaweza kuja kujikuta anawajibika kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuikosesha serikali mapato.

Wanasiasa sio watu, hawachelewi kukugeuka.

Tukumbuke sheria tunatunga wenyewe na kuzipitisha kwa mbwembwe.

Swali: Iweje leo tuzione chungu?

Tunavuna tulichopanda.
Vyombo vya kusimamia vifaa vifike vinapotakiwa viko vingi wala haliitaji uchunguz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani hapa ndo Wana ccm wameshindwa wawe wapi either kwa RC or Waziri.
Mana unaweza ukawa kwa Wazira yakamkuta ya Nape wakashindwa kula matapishi yao, wakawa kwa RC ukasikia amepangiwa majukumu mengine? Niwashauri tu Wana ccm mlivyokua ni wafuata upepo kuweni tu katikati uku mkisubri Baba yenu ataamua nini, ili atakako favor ndo muende uko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaaaaaaaaa ni bendera fuata upepo wengi shubaaamit zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wengine ni watu wa ajabu sana. Na huyu mtoa mada naye ni great thinker!
 
Huyu karudi toka ughaibuni lini hasa,...nchi hii sura tulizonazo sio halisi.

Hilo la shida za ofisi ni moja, na la kufuata taratibu ni jingine.

Uwe mwangalifu.

Safi kwa ujumbe lakini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paschal huwa nakuheshimu sana ila kwa hili tumia akili kwanza.Nilitarajia ufanye utafiti nakujiridhisha kujua nyuma ya pazia lakini hata Eagles wameshindwa kukwambia ukweli. Nakwambia mizigo hiyo wameweka vitu vya shule vichache lakini vitu vingi ni kwa matumizi ya hotel yake inayojengwa mwanza. Suala la walimu wa Dar Es Salaam linatumiwa lakini linakitu nyuma ya Pazia. Hivi hukumbuki simba wakati wanaenda kucheza chambion league africa walikwa wakienda na mipira mingi ila ikifika kule wanakokwenda basi mipila inachukuliwa wanapewa mingine. Huo wakati ilikuwa ndo ujanja wakuuza Gnada kwa wafadhili simba wa wakati huo.Sasa suala la vifaa vya Makonda kunakitu kikubwa nyuma ya Pazia. Kama shida ipo basi waliovitoa watoe na lisiti walipovinunua. Fuatalia kama utaona ukweli kama kuna watanzania wamechangia mzigo huo. Mbona container 16 zimesimanishwa kuja TZ na hao waliok markeani baada ya ngoma kugoma. Mbona Makonda aliikataamizigo mwanzoni alipohojiwa. Kunauchafu mwingi nyuma ya hii sakata. Waziri kahukua uamzi sahihi.
Mkuu Kimla, kwanza asante kuniheshimu, heshima is earmned, na ikipotea, its gone!. Siku zote mimi ni mkweli na very transparent, nikiamini transparency ndio the only way ya ku resolve hii issue. Containers zile 20 zimefunguliwa, ni samani new and used.

Hoja yangu ni ndogo sana, maadam, samani hazina msamaha wa kodi, kiwango cha kodi ni bilioni 1.2, itaigharimu serikali yetu, kutumia bilioni 20 kununulia the same amount of samani zenye the same quality and finishing kutoka Keko.

Hiyo kodi serikali inadai, kodi ya 1.2 bilions kwenye samani za shule, halafu inakuja kulipa bilioni 20, kununua the same samani toka Keko!. Hii ni akili au matope?!.

Hii sii mara ya kwanza kwa serikali yetu kufanya maamuzi ya ajabu. Ni sakata la Richmond.
  1. Tume ya Mwakyembe imesema Richmond ni kampuni hewa, wanatuibia kupia capacity charges za milioni 152 kwa siku, hivyo wakashauri tuvunje mkataba, na hatutashitakiwa, popote kwa sababu kampuni hewa, haiwezi kushitaki popote, hivyo tukavunja mkataba.
  2. Tukawasha mitambo ya IPTL kwa inayofua umeme mdogo kwa gharama kubwa mara 2 ya Richmond, huku ikitumia mitambo chakavu mara 10 ya Richmond, na kuchafua mazingira mara 100 ya Richmond. Na malipo haya ndio yamezalisha escrow.
  3. Tukashitakiwa kwa kuvunja mkataba, tukalipishwa tozo ya Dowans, waliotushauri tuvunje, wakajiapiza hatulipi "over my dead body"
  4. Msingi wa kulipishwa ni japo Richmond ni kampuni hewa, mitambo ya Richmond sio mitambo hewa, na umeme unaofuliwa na mitambo hiyo, ni umeme kweli sio umeme hewa, hivyo malipo ya Richmond, ni malipo ya capacity chargers za mitambo kweli na malipo ya umeme unaofuliwa.
  5. Kiukweli hiyo tozo tulilipa kimya kimya ambapo gharama yake ni mara 10 ya malipo ya halali kama tusingevunja mkataba!.
  6. Mitambo ile ikanunuliwa na Simbion, mitambo ile ile, capacity charges zile zile na tukalipa na kuendelea kulipia hadi Magufuli ameingia.
  7. Waliotushauri kuvunja mkataba na kujiapiza, ndio wale wale waliokuwa wakicheza ngoma na mama Clinton siku Simbion inazaliwa.
  8. Tumevunja mkataba wa Richmond wa capacity charges ya milioni 152 kwa siku, tukalipishwa faini ya mara kumi zaidi, kisha tukasaini mkataba wa Simbion wa capacity charges ya milioni 152 kwa siku!.
  9. Hii ni akili au matope?!.
  10. Sasa tunauza samani za shule kwa mnada kutafuta bilioni 1.2 ya kodi za serikali. Halafu serikali hiyo hiyo inatoa bilioni 20, ya kodi kununulia samani za waalimu kutoka Keko. Hii ni akili au matope?.
P.
 
Mbona hatuulizi ni kwa nini basi Makonda aliweza kutoa contena 16 kwa jina lake kutoka 36 za awali. Na je hizo 16 amezigawa wapi? Anayejua hili atuambie!
Hatuna haja ya kuuliza, si tunataka kodi, we unayetaka kuuliza ruksa tutapotezeana muda, kuna nchi jirani hawana bandari tunahitaji hiyo nafasi ya macontena
 
mkuu hapo ni sheria imefuatwa, unataka ipindishwe? Mmezoea vya kunyonga vya kuchinja hamuviwezi! Usiwe mgumu kuelewa ni nani atadhibitisha kua vinaenda mashuleni? Hii inaonyesha ni mali ya mtu binafsi hivyo lazima itozwe kodi stahiki!

Katiba inavunjwa kupindisha sheria ndio tabu? Mbona imekuwa jambo la kawaida kutosimamia sheria au kumwangalia usoni mhusika? Anachosema mleta mada ni kuwa haikutarajiwa Makonda kufanyiwa hivyo. Meaning something is unfolding!
 
Hapo tatizo ni kwa nini aingize mzigo wa msaada kwa jina lake basi hayo mengine wao hawayahitaji
Hajaingiza kwa jina lake, Kaingiza kwa jina la paul makonda! Labda ni jina la shule jamani! Hivi kwani hamna shule inayoitwa paul makonda? Nimeambiwa DAB NDIYO SHULE ALIYOISOMEA KULE KOLOMIJE. Nawakilisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hatuulizi ni kwa nini basi Makonda aliweza kutoa contena 16 kwa jina lake kutoka 36 za awali. Na je hizo 16 amezigawa wapi? Anayejua hili atuambie!
Hatuna haja ya kuuliza, si tunataka kodi, we unayetaka kuuliza ruksa tutapotezeana muda, kuna nchi jirani hawana bandari tunahitaji hiyo nafasi ya macontena
Kama ni kweli vifaa hivyo ni kwa ajili ya shule, serikali ifanye yafuatayo:
1. ifuatilie kujua vilikotoka na staili iliyotumika kuvisafirisha;
2. Makondo ale kiapo kwamba vifaa hivyo ni kwa ajili ya mashule ya Dar es Salaam ili kuepuka kugeuziwa kibao;
3. ivipe msamaha wa kodi;
4. ihakikishe kwamba vinagawiwa vyote mashuleni kwa kumshirikisha yeye (Makonda).
Vinginevyo, mivutano hii itagawa chama na serikali. Kumbukeni tunajenga nyumba moja na hatuna sababu za kugombania fito!
Jitafakarini!
Acha hotuba Lipa kodi kwa maendeleo ya Taifa ndio slogan yetu. Slogan ya msamaha ipo kwenye dini hilo ulielwe sawa mkuu?
 
SAKATA LA MAKONTEÑA YA MAKONDA KUPIGWA MNADA LITIZAMWE UPYA

Na: Mtetezi wa Wanyonge.

Nimemsikia Waziri Mipango akisema kuwa Lazima Makontena hayo Yalipiwe Kodi ama yapigwe Mnada ili serikali ipate Kodi yake...

My Take

Tukumbuke kuwa Makontena hayo ya Vifaa ni Watanzania wenzetu wamejitolea na ndiyo maana hakuna kiwanda kilichopewa tenda hiyo na huo ni msaada kama alivyopata misaada ya Miguu Bandia, Ujenzi wa Hospital, Viwanja vya Mpira, magari ya Police , Pikipiki, Computer [emoji335] na vingine vingi alivyowai kufanya.

Makonda aliomba Samani si kwa faida yake bali kwa faida ya Watanzania na Kuipunguzia Serikali mzigo wa Manunuzi ya Vifaa hivyo.

Leo Kigezo Kimekuwa SHERIA! Sawa lakini Sheria zinatungwa, kusomwa na kutafsiriwa na wanadamu na bado huacha mwanya wa busara kutumika na kila kesi huamliwa kulingana na mazingira na ushahidi wake. (Ndio maana kuna Dissenting decision/Opinion and or Consential/Concurring Opinion)

Na Ikumbukwe Kuwa Sheria ya kodi inaruhusu busara kutumika pale inapoonesha kuwa vitu au mali zitatumika kwa manufaa ya jamii ya wanyonge na sio mtu binafsi.

Ikiwa Makanisa, NGOs nk. Kila kukicha yanapewa misamaha ya kodi kwa idhini ya MaRC na MaDC kulikoni hasa haya Makontena ya Viti vya Walimu? Computer za Shule? Meza na nk...?

Nikweli Yalitumwa kwa Jina la Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Lakini kampeni yake Iko wazi tangu awali na si ya kificho, Walioyatoa walitamka wazi ni ya nini na hayana faida kwa Makonda bali kwa Taifa na Watu wake hasa Wanyonge walio wengi.

Sasa Msuguwano Huu unatoka wapi?
Hiyo Kodi Ni Bei gani?
Kodi inadaiwa hapo inathamani Kubwa kuliko Samani ya hivyo Vifaa?
Hiyo Kodi Inaweza kununua vifaa vyote hivyo?
Haya Vikipigwa Mnada Serikali itapata Bei Gani? Hiyo Bei Inaweza kununua Samani zote hizo?

Tusing'ang'ane na Sheria inayotupotezea kingi zaidi kwa Kukomalia Kodi nakupoteza Mali Kubwa zaidi ya Kodi, Hekima na Busara zinaweza Tatua hili kwa Kukaa nakujadili Faida na Hasara za Kodi, Faida na Hasara zakuendelea kuwa na Vifaa hivyo, Faida na Hasara za Vifaa hivyo Kuingia kwenye Majengo yanayongoja Vifaa na Wanyonge kuvitumia.

RC Makonda Ameomba Misaada Majengo yamejengwa yanahitaji Samani, Serikali Imesaidiwa na Wazalendo wa Taifa hili waishio ughaibuni kwanini Tuwafanye wajione hawana Thamani kwa Kujitoa kwao kusaidia Nchi yao?

Mh Waziri Mipango na Wasaidizi wako na Watu wa TRA mlitizame Upya Jambo hili.

Mlio Karibu na Mh Rais Fikisheni Kilio cha Wanyonge wakatumie Vifaa hivi.
Iko Misamaha Mingi sana ya Kodi Kupitia Vifaa hivyo kuwa Vinaenda kuhudumia Jamii basi Dhamila Kuu ikatimie kwa Vifaa hivyo Kusamehewa Kodi na Vikatumike Mashuleni.

Mnyonge Mnyongeni haki yake Mpeni!
Hapa Hatumkomoi Makonda ila Tunataka Kuwakomoa Walimu na Watoto wa Shule wenye uhitaji wa Vifaa hivyo.

Sakata la Makontena Liangaliwe upya kwa Maslahi Mapana ya Taifa Hili na Wanyonge wenye Uhitaji wa Vifaa hivyo.

Waziri Mipango Fanya Mipango Vifaa viwafikie Wanyonge bila Kodi, Manake hata Mkisema Kodi ilipwe analipa nani?
Makonda aloomba kwa Niaba ya serikali?

Au Tuwaombe Pesa Walotupa Msaada tena wao Ndo walipe Kodi tena?

Kwani Tunataka Kumfurahisha nani katika hili? Au Kumkomoa Nani katika Hili?

Wanaoteseka ni Walimu na Watoto wa shule, Misuli tunayotunishiana Viongozi Haitusaidii sisi watanzania kwa ujumla.

Kodi na Mnada kwa Vifaa hivyo Vyote vinatuumiza kwani Vinapelekea Kupoteza Vifaa vyenye uhitaji kwa wanyonge.

Kodi tunazikusanya ili Tununue Vifaa vya Shule, Leo Hii Vifaa Vimekuja Buree na Vingi vyenye ubora zaidi sisi hatuvitaki kisa Kodi.

Inasikitisha sana hii Hali....


Tunaomba Viongozi walitizame upya jambo huli.

Makontena haya Faida kwa Mkonda zaidi ya Faida kwa Wanyonge na Serikaki yao ambao wanahitajika Kuhenyeka kwa Mika kadhaa huku wakilipa kodi ndo waweze kununua Vifaa vyote hivyo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kwa mlio walimu mtanielewa ninaposema waziri kakurupuka wala hazijui changamoto za elimu
ukisikiliza kwa umakini kwenye hotuba yake ya juzi utagundua kabisa aelewi anachokiongea...

Anaongelea maswala ya elimu bure kitu ambacho ni nje kabisa ya mada ya makontena

swala hapa ni vifaa kwa ajiri ya kusaidia elimu ya dsm ambayo ina changamoto nyingi ikiwa na mrundikano wa wanafunzi na mambo kibao

Makonda inawezekana kuna sehemu alikosea katika mchakato huo lakini serikali walitakiwa kuwa wajanja wangeruhusu kwanza vitu viingie ndio waanze kuvimonitor wapate ushahidi wa kutosha ndio waje kumtuhumu.

matokeo yake wananchi nao wameyabeba na kusahau watoto wao ndio wanakaa chini milele
mimi niko na ushahidi kabisa nilienda shule moja na taasisi fulani kutoa msaada wa computer lakini unakuta walimu stafu viti tu vya kukalia haviwatoshi hii ni aibu kama mwalimu hana kiti stafu mwanafunzi je darasani itakuwaje?

tukiweka siasa pembeni Makonda yupo sahihi kabisa na ana nia njema ingawa anaweza kuwa kafanya makosa kutumia jina lake kwa ushauri mbovu wa watendaji waliopo chini yake lakini naamini tatizo letu la elimu ni kubwa mno kuliko jina la makonda kuwa kwenye makontenana hili swala tunalibabe kishabiki sana kama kawaida yetu...

kwamba mimi ni chadema Gambo akifiwa na mzazi wake nashangilia, mimi ni ccm Sugu akipata msiba nashangilia upuuzi mtupu.

Hivi waziri anavipiga mnada vitu vya shule za dsm watu tunashangilia leo halafu kesho jangwani secondary inakuwa ya mwisho tunaanza kumponda makonda ...

Hivi vitu vikinunuliwa na wafanya biashara sisi wananchi wa kawaida tutafaidika vipi direct kama ambavyo tungeviona kwenye shule zetu? namimi naongeza na alaaniwe kabisa atakae vinunua.

"Form four wanakaribia pia kuanza mtihani msisahau kuleta mrejesho hapa wa shule za umma"
According to TRA officer hata ingeagiza office ya mkoa bado ingelipa kodi bcoz they are exclusive in tax exemption.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naungana na mtoa post kupinga vikali upigwaji mnada vifaa hivo tena vya msaada, japo nakiri kwel Makonda kukosea hasa pale alipo amua kutumia jina lake badala ya taasis ya Elimu.

Bado nawasihi viongozi watumie busara na hekima hasa katika utatuzi wa matatizo mbali mbali ili kutoleta sintofaham kwa umma zisizo na tija kwa jamii.

Da Pride

Sent using Jamii Forums mobile app
Kupiga mnada na kuingiza fedha hazina ndio busara na hekima namba 1kusamehe kodi inabidi tutafute chuo walichompa mpango uDR wafanye mpango wafute na mteule atengue nafasi yake, ili mpango akose kazi ya mpango. Atakubali Mpango akose mipango?
 
Mbona watetezi ni wengi sana kwenye hili swala?
Watumishi tunakatwa Kodi kila uchao.
Kinachoshindikana nini yeye kulipa kodi?
Acheni 'sound' acha MTU alipe kodi.
Vimishahara vya kuunga tu huku serikalini kodi yake mpaka unasema ebwana ndio.
Huyu anatafuta janja janja ya kutolipa.
Mpango komaa atoe mzigo wetu
Tujifunze ustaarabu, tulipa kodi. MTU wa kodi kodi!!!
 
Mbona watetezi ni wengi sana kwenye hili swala?
Watumishi tunakatwa Kodi kila uchao.
Kinachoshindikana nini yeye kulipa kodi?
Acheni 'sound' acha MTU alipe kodi.
Vimishahara vya kuunga tu huku serikalini kodi yake mpaka unasema ebwana ndio.
Huyu anatafuta janja janja ya kutolipa.
Mpango komaa atoe mzigo wetu
Tujifunze ustaarabu, tulipa kodi. MTU wa kodi kodi!!!
Mbona watetezi ni wengi sana kwenye hili swala?
Watumishi tunakatwa Kodi kila uchao.
Kinachoshindikana nini yeye kulipa kodi?
Acheni 'sound' acha MTU alipe kodi.
Vimishahara vya kuunga tu huku serikalini kodi yake mpaka unasema ebwana ndio.
Huyu anatafuta janja janja ya kutolipa.
Mpango komaa atoe mzigo wetu
Tujifunze ustaarabu, tulipa kodi. MTU wa kodi kodi!!!
bahasha za khaki kazini
 
Back
Top Bottom