Simbachawene kafanya nini tena? Mbona imekuwa mapema sana kutenguliwa kwake!
Tutamkoma Makonda master misifa au tuseme kuhamasisha AFCON kwa Tanzania imemfanya apate nafasi?
==================
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kutenguliwa ni kama ifuatavyo:-.
(i) Mhe. Patrobas Paschal Katambi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Katambi alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, anachukua nafasi ya Mhe. Boniface George Simbachawene (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
(ii) Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum). Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Prof. Kabudi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;
(iii) Mhe. Paul Christian Makonda (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Makonda alikuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo;
(iv) Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Londo alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;
View attachment 3527178View attachment 3527177