PostGE2025 Makonda ateuliwa kuwa Waziri wa Habari, Simbachawane atenguliwa Uwaziri wa Mambo ya ndani ya Nchi

PostGE2025 Makonda ateuliwa kuwa Waziri wa Habari, Simbachawane atenguliwa Uwaziri wa Mambo ya ndani ya Nchi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Simbachawene kafanya nini tena? Mbona imekuwa mapema sana kutenguliwa kwake!

Tutamkoma Makonda master misifa au tuseme kuhamasisha AFCON kwa Tanzania imemfanya apate nafasi?
==================
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kutenguliwa ni kama ifuatavyo:-.

(i) Mhe. Patrobas Paschal Katambi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Katambi alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, anachukua nafasi ya Mhe. Boniface George Simbachawene (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;

(ii) Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum). Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Prof. Kabudi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;

(iii) Mhe. Paul Christian Makonda (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Makonda alikuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo;

(iv) Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Londo alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;

UTEUZI NA UTENGUZI - 08 JANUARI, 2026.jpg
UTEUZI NA UTENGUZI - 08 JANUARI, 2026(1).jpg
 
Kweli ? Simbachawene alimsifia sana Samuya

TOKA MAKTABA:

April 2, 2023
VIDEO: SIMBACHAWENE na JENISTA MHAGAMA WALIVYOKULA KIAPO CHA UWAZIRI MBELE ya RAIS SAMIA IKULU..

View: https://m.youtube.com/watch?v=1a1L940NW5U
.Rais Samia Suluhu Hassan, leo April 2, 2023 amewaapisha mawaziri wawili aliowateua katika mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri aliyoyafanya hapo jana.Walioapishwa katika hafla ndogo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, ni Jenista Mhagama ambaye anakuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), akichukua nafasi ya George Simbachawene.Pia Rais Samia amemuapisha George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, akibadilishana nafasi na Mhagama.
 
Back
Top Bottom