Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Mgombea ubunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda ametoa elimu ya namna ya kupiga kura kwa baadhi ya wananchi wa visiwani Zanzibar.
Makonda ambaye amewasili visiwani humo mapema leo Ijumaa, Oktoba 24, 2025 kwa ajili ya kumuombea kura mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameelekeza hatua kwa hatua namna ya kumpigia kura mgombea urais wa CCM na mgombea mwenzao wake, Dk Emmanuel Nchimbi.
"Kwenye uchaguzi huu wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna alama tatu, mojawapo utakuta alama ya Chama cha Mapinduzi sababu kila mgombea lazima ajulikane ametokea chama gani, unakuja hapa huyu ni mgombea mwenza, unakuja hapa huyu ni mgombea urais kwa hiyo unapotiki unakuwa umetiki kwa Samia," amesema Makonda.