The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewaomba viongozi wa dini mkoani humo kutumia nafasi zao kuhamasisha waumini wajitokeze katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na amani itawale.
Makonda amesema hayo leo Jumanne Novemba 19, 2024 alipozungumza na viongozi wa dini wa madhehebu kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Soma pia: RC Makonda apiga chai na maandazi wakati akitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kujiandikisha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa
Makonda amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuhamasisha uchaguzi huo ufanyike kwa amani hasa katika kipindi cha kampeni zinazotarajiwa kuanza kesho.
"Rais anatambua mchango na nafasi yenu, niwaombe viongozi wa dini tuhakikishe katika mchakato huu wa kupata viongozi ikiwamo kampeni zinafanyika kwa amani na utulivu, viongozi wa dini sauti zenu ni muhimu sana katika mchakato huu," amesema Makonda.
Chanzo: Mwananchi