Uchaguzi 2020 Makonda azuiwa kukaa Jukwaa Kuu kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM

Uchaguzi 2020 Makonda azuiwa kukaa Jukwaa Kuu kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM

"Adui muombee njaa" wamesema wabongo fleva, adui wa kumuombea njaa Bakhresa hawezi kuwa Mo au Manji. Mama Mwajuma ndalandefu atamuombea njaa Mrs Mangi mwenye duka mtaani, angalau hawa wako karibu na njaa, inaweza kutokea kweli.

Prince kalikoroga, mfalme akijivika uso wa mbuzi, Prince atazeeka vibaya kwakuwa mitano ya pili ikiisha, ndio itakuwa baaaaasi, si amechagua kutumikia mtu badala ya kiti, chama au raia!
 
Nimeogopa sana
Mtu anasema
"Nimenunua ndege" - Raia Kimyaaaaaa
"Nimejenga meli" - Raia Kimyaaaaaa
"Nimetoa ajira elfu ngapi" - Raia Kimyaaaaaa
"Najenga bwawa la umeme" - Raia Kimyaaaaaa
"Najenga makao makuu" - Raia Kimyaaaaaa

Si mnapenda eeeee - Raia wachache - Ndioo

Watu hawana kitu mifukoni, hali mbayaaaaa sana

Mitaani baa zinajaa jumamosi ya kwanza ya mwisho wa mwezi, baada ya hapo huoni mtu tena
 
Na baaaado yajayo yatamhuzunisha sana.

Afu kuna mtu kwenye jukwaa hili aliwahi kutabiri eti huyu bwana ndo atarithi mikoba ya mkuru 2025 , Dah maisha kweli yanakimbia kwa kasi sana lkn pia maadam hatujui kesho yetu lolote linaweza tokea watu wanatumia kila aina ya nguvu kupata madaraka
 
Vijana tukipata vyeo kidogo tuna jimwambify sana"Askofu Shoo" leo hii binadamu aliyekuwa anapata raha kuliko binadamu yoyote ni wakuzuiwa kweli na Green Guard? Hii itoshe kutupa funzo kuwa vyeo hivi ni dhamana tu; siku ukipoteza cheo chako hata nzi watakudharau.

Nasikia wasanii huko Dodoma wanamnyanyapa kama ukomaa yani, saivi ni aibu kuonekana kwamba una urafiki na Bashite ilihali walikuwa wanajaa pale ofisini kwake kuomba kupiga naye picha tu.

Hata physical appearance yake haikuwa poa. Viatu vina vumbi hajachana nywele; inaonekana ana sonono kuliko kawaida, mfadhaiko wa moyo mpaka akili.

N:B Yajayo yanafurahisha. Ile IST atatamani hata kuwa nayo!
Apandacho mtu ndicho atakachovuna!
 
Raia mwenzetu huyu..
IMG_20200829_235653.jpeg
IMG_20200829_235658.jpeg
 
Tujikumbushe kauli zake pendwa
  1. Mimi ni jemedari kwelikweli
  2. Huyu jamaa anasema wakipimwa wakikutwa wanayo marinda yeye yupo tayari kwenda jela
  3. Wabunge wote warudi bungeni haraka sana, sitaki kuwaona mkoani kwangu
  4. Sitaki kuona mtu anaingia mjini akiwa hajaoga
  5. Kuanzia leo hii nyinyi nyote sio waratibu elimu kata, ondokeni
  6. Ninayo orodha ya wauza madawa ya kulevya, na leo nitaitaja
  7. Kuna watu wanajiona ni wakubwa kuliko mimi, nawaambia hata hao wakubwa zao wao, mimi wananiheshimu
  8. Nitahakikisha zoezi hili la upimaji tezi dume linafanyika nyumba kwa nyumba, hakuna kukimbia
  9. Barakoa anavaa mgonjwa ili asiambukize wengine, nyie mnaovaa barakoa na hamjapima nawashangaa
  10. Kila mtu ahakikishe anavaa barakoa kila anapoenda kwenye mkusanyiko wa watu, ni lazima sio ombi
  11. Watu mmefunga maduka kisa corona, huo ni uzembe
  12. Kila mwanamke aliyetelekezwa na mtoto aje, hao wanaume tutawaita, leo binti yake lowasa amekuja analia, mzee yule anamkataa
  13. Leo natangaza vinywaji vyote kuuzwa kwa nusu bei, wamiliki wote wa bar, hotel na kumbi za burudani wameshafahamishwa
  14. Nimefurahi sana kumuona mama aliyepita hapa mbele, ni mama wa mfano, sio hawa wakina Piere waleviwalevi hawa
  15. Sikuwahi kutegemea hata siku moja, kumuona mchaga anampa pesa mlemavu
  16. Mwenye picha hii, aende kituo chochote cha polisi Dar es salaam aseme amefuata ujumbe wangu
  17. Hivi mnajua kwann jana katangaza anaahirisha mikutano, mtoto wake kakutwa na coronaaaaaaa
  18. Na nimetoa fursa, watu wanaowafahamu wanaofanya biashara za ushoga, watutumie meseji, na nimetoa namba zangu za simu
  19. Nipeni ridhaa na nitawatumikia kwa uaminifu mkubwa.............................................WAJUMBE HAWAKUELEWA SOMO
  20. MAMBO NI MENGI MUDA NI MCHACHE, ONGEZA NA ZAKO UNAZOZIKUMBUKA
All in all, we had a good/bad/best/worst time with you mwamba, pumzika kwa amani.
 
Wananchi wakimuona Makonda hasira zao zinawaka juu ya raisi.

Asilimia 65 ya wanaomchukia rais inatokana na wale wateule wake wasio hekima wabpumbavu na wajivuni kama Makonda, Sabaya na wote wa namna hiyo.
So walinzi wa rais washaligundua hilo ndio maana wanalifanyia kazi kwa vitendo
Yule wa Iringa simsikii sikuizi sijui kapatwa na nini, kapunguza sana kiherehere, amebaki wa Mbeya Chalamira huyo naye ana kilimilimi.
 
Wanangoja uchaguzi uishe wampe cheo kingine. Wamemtumia vibaya na kwakuwa hiki ni kipindi cha kampeni,watajidai kumtenga ili asiwaathiri na makandokando yake, ila uchaguzi ukiisha, watampa tena nafasi.

Subirini mtakuja kuniambia.

Utabiri: 2020 Makonda anaweza kupigwa chini ili kutafuta kura halafu uchaguzi ukiisha anapewa kitengo kingine
Mbona hili liko wazi tu! Jiwe na huyu bwana mdogo kuna jambo lenye siri kubwa sana la kinadhiri linalowafunga. Jiwe hawezi kumtupa akajisababishia matatizo.
Sema huyu bwana mdogo DAB busara zake ndogo sana. Kipindi hiki cha mpito anatakiwa kujishusha kwa unyenyekevu kama vile hayupo.
 
Kama alitaka kukaa jukwaa kuu basi ana matatizo. Alishawahi kuwa kiongozi na utaratibu anaujua, sasa kwa nini ajidhalilishe mbele ya umma?
Ni ulevi wa madaraka na kuutaka utukufu tu!!

Alisahau "...mualikwapo kwenye karamu msikimbilie viti vya mbele msije kuaibishwa wajapo wenyewe!!"
Atalilia kanisani leo!!!
Ameanza kupata malipo kwa aliowadhalilisha pia hadharani. Aendelee kutubu na awaombe msamaha aliowaumiza hadharani vinginevyo ataadhiriwa zaidi.
Coco sijui alilionaje tukio lile!!
 
Sijui ni nani alimshawishi akagombee ubunge aache ukuu wa mkoa.

Alikuwa na nafasi nzuri ya kujipanga. Angeweza kugombea ubunge 2025.
Hilo ni kosa kubwa alilofanya Mr Makonda, Kigamboni haikuwa karata nzuri kwake. Wakongwe ndani ya chama tulimwambia ila alifikiri pesa itawanunua wajumbe.
 
Hilo ni kosa kubwa alilofanya Mr Makonda, Kigamboni haikuwa karata nzuri kwake. Wakongwe ndani ya chama tulimwambia ila alifikiri pesa itawanunua wajumbe.
Kibamba ilimfaa zaidi,hata wagombea wake hawakuwa wanafahamika kuliko yule wa Kigmboni.
 
Back
Top Bottom