Uchaguzi 2020 Makonda azuiwa kukaa Jukwaa Kuu kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM

"Adui muombee njaa" wamesema wabongo fleva, adui wa kumuombea njaa Bakhresa hawezi kuwa Mo au Manji. Mama Mwajuma ndalandefu atamuombea njaa Mrs Mangi mwenye duka mtaani, angalau hawa wako karibu na njaa, inaweza kutokea kweli.

Prince kalikoroga, mfalme akijivika uso wa mbuzi, Prince atazeeka vibaya kwakuwa mitano ya pili ikiisha, ndio itakuwa baaaaasi, si amechagua kutumikia mtu badala ya kiti, chama au raia!
 
Nimeogopa sana
Mtu anasema
"Nimenunua ndege" - Raia Kimyaaaaaa
"Nimejenga meli" - Raia Kimyaaaaaa
"Nimetoa ajira elfu ngapi" - Raia Kimyaaaaaa
"Najenga bwawa la umeme" - Raia Kimyaaaaaa
"Najenga makao makuu" - Raia Kimyaaaaaa

Si mnapenda eeeee - Raia wachache - Ndioo

Watu hawana kitu mifukoni, hali mbayaaaaa sana

Mitaani baa zinajaa jumamosi ya kwanza ya mwisho wa mwezi, baada ya hapo huoni mtu tena
 
Na baaaado yajayo yatamhuzunisha sana.

Afu kuna mtu kwenye jukwaa hili aliwahi kutabiri eti huyu bwana ndo atarithi mikoba ya mkuru 2025 , Dah maisha kweli yanakimbia kwa kasi sana lkn pia maadam hatujui kesho yetu lolote linaweza tokea watu wanatumia kila aina ya nguvu kupata madaraka
 
Apandacho mtu ndicho atakachovuna!
 
Tujikumbushe kauli zake pendwa
  1. Mimi ni jemedari kwelikweli
  2. Huyu jamaa anasema wakipimwa wakikutwa wanayo marinda yeye yupo tayari kwenda jela
  3. Wabunge wote warudi bungeni haraka sana, sitaki kuwaona mkoani kwangu
  4. Sitaki kuona mtu anaingia mjini akiwa hajaoga
  5. Kuanzia leo hii nyinyi nyote sio waratibu elimu kata, ondokeni
  6. Ninayo orodha ya wauza madawa ya kulevya, na leo nitaitaja
  7. Kuna watu wanajiona ni wakubwa kuliko mimi, nawaambia hata hao wakubwa zao wao, mimi wananiheshimu
  8. Nitahakikisha zoezi hili la upimaji tezi dume linafanyika nyumba kwa nyumba, hakuna kukimbia
  9. Barakoa anavaa mgonjwa ili asiambukize wengine, nyie mnaovaa barakoa na hamjapima nawashangaa
  10. Kila mtu ahakikishe anavaa barakoa kila anapoenda kwenye mkusanyiko wa watu, ni lazima sio ombi
  11. Watu mmefunga maduka kisa corona, huo ni uzembe
  12. Kila mwanamke aliyetelekezwa na mtoto aje, hao wanaume tutawaita, leo binti yake lowasa amekuja analia, mzee yule anamkataa
  13. Leo natangaza vinywaji vyote kuuzwa kwa nusu bei, wamiliki wote wa bar, hotel na kumbi za burudani wameshafahamishwa
  14. Nimefurahi sana kumuona mama aliyepita hapa mbele, ni mama wa mfano, sio hawa wakina Piere waleviwalevi hawa
  15. Sikuwahi kutegemea hata siku moja, kumuona mchaga anampa pesa mlemavu
  16. Mwenye picha hii, aende kituo chochote cha polisi Dar es salaam aseme amefuata ujumbe wangu
  17. Hivi mnajua kwann jana katangaza anaahirisha mikutano, mtoto wake kakutwa na coronaaaaaaa
  18. Na nimetoa fursa, watu wanaowafahamu wanaofanya biashara za ushoga, watutumie meseji, na nimetoa namba zangu za simu
  19. Nipeni ridhaa na nitawatumikia kwa uaminifu mkubwa.............................................WAJUMBE HAWAKUELEWA SOMO
  20. MAMBO NI MENGI MUDA NI MCHACHE, ONGEZA NA ZAKO UNAZOZIKUMBUKA
All in all, we had a good/bad/best/worst time with you mwamba, pumzika kwa amani.
 
Uchaguzi ukiisha anaweza kupewa cheo tena
 
Yule wa Iringa simsikii sikuizi sijui kapatwa na nini, kapunguza sana kiherehere, amebaki wa Mbeya Chalamira huyo naye ana kilimilimi.
 
Mbona hili liko wazi tu! Jiwe na huyu bwana mdogo kuna jambo lenye siri kubwa sana la kinadhiri linalowafunga. Jiwe hawezi kumtupa akajisababishia matatizo.
Sema huyu bwana mdogo DAB busara zake ndogo sana. Kipindi hiki cha mpito anatakiwa kujishusha kwa unyenyekevu kama vile hayupo.
 
Kama alitaka kukaa jukwaa kuu basi ana matatizo. Alishawahi kuwa kiongozi na utaratibu anaujua, sasa kwa nini ajidhalilishe mbele ya umma?
Ni ulevi wa madaraka na kuutaka utukufu tu!!

Alisahau "...mualikwapo kwenye karamu msikimbilie viti vya mbele msije kuaibishwa wajapo wenyewe!!"
Atalilia kanisani leo!!!
Ameanza kupata malipo kwa aliowadhalilisha pia hadharani. Aendelee kutubu na awaombe msamaha aliowaumiza hadharani vinginevyo ataadhiriwa zaidi.
Coco sijui alilionaje tukio lile!!
 
Sijui ni nani alimshawishi akagombee ubunge aache ukuu wa mkoa.

Alikuwa na nafasi nzuri ya kujipanga. Angeweza kugombea ubunge 2025.
Hilo ni kosa kubwa alilofanya Mr Makonda, Kigamboni haikuwa karata nzuri kwake. Wakongwe ndani ya chama tulimwambia ila alifikiri pesa itawanunua wajumbe.
 
Hilo ni kosa kubwa alilofanya Mr Makonda, Kigamboni haikuwa karata nzuri kwake. Wakongwe ndani ya chama tulimwambia ila alifikiri pesa itawanunua wajumbe.
Kibamba ilimfaa zaidi,hata wagombea wake hawakuwa wanafahamika kuliko yule wa Kigmboni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…