Makonda: CHADEMA wamekimbia kufanya mikutano na kuanza kulilia vyombo vya habari kufanyiwa mahojiano

Makonda: CHADEMA wamekimbia kufanya mikutano na kuanza kulilia vyombo vya habari kufanyiwa mahojiano

Huyu Mwenezi ni Mjinga WanaCHADEMA mpuuzeni.

Sote tunajua yeye na Chalamila ndio wako nyuma ya Sakata hili la WASAFI.
Acheni kulialia nyie.fungueni kituo Chenu cha Tv na redio na siyo kwenda kuharibu shughuli za watu maofisini huko. Ruzuku zikitoka mnaziona tamu sana na mnazitafuna zote kama mchwa.
 
Acheni kulia lia ndugu zangu.fungueni Tv na redio yenu.kwani si mmepokea mamilioni kwa mamilioni ya Ruzuku? Hapa majuzi tu si mmebugia Billion 2.7? Mlishindwa nini kufungua Tv kwa miaka yote? Miaka yote si mmekuwa mnalialia tu? Kwanini hamjawahi kuchukua hatua za kufungua Tv zenu? Mtalialia mpaka lini? Mtang'ang'ania mpaka lini kwenye ofisi za watu ili mfanyiwe mahojiano?
Wewe fatilia maslahi yako kwa kazi yako. Chadema maslahi yao kwa mambo yao..
Wote mna maslahi...
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mheshimiwa Paul Makonda Mwamba na Jabali la siasa na kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara hapo jana aliitetemesha Mbeya kwelikweli,alilisimamisha jiji na kuteka mioyo ya wananchi , shughuli zote zilisimama na kubaki na shughuli moja tu ya kutega masikio kwa Mwamba Mwenyewe Makonda.

Akiwa katika viwanja vya Rwanda nzovwe maarufu kama viwanja vya CCM aliwalipua Wana Mbeya kwa vicheko visivyokatika pale alipowaambia kuwa CHADEMA wameacha na kukimbia kabisa kufanya mikutano ya hadhara na sasa wameanza kulilia vyombo vya habari ili wafanyiwe mahojiano.akasema walitaka mikutano ya hadhara Mheshimiwa Rais akawaruhusu lakini Mwamba mwenyewe Makonda alipoingia mitaani CHADEMA wote wakatimua mbio kali sana kwenda kujificha, ambapo hadi sasa hawaonekani mitaani na sasa wanaanza kuvamia ofisi za watu wakililia kutaka kufanya mahojiano.

Ndugu zangu hata mimi niliona CHADEMA na Lissu wake ni kama watu ambao hawapo sawa kichwani na ni watu wasio jitambua kabisa.hivi unaanzia wapi kulazimisha kuhojiwa kwenye chombo binafsi? Kama mhusika kakupigia simu ukiwa kwako kwamba usije kwenye mahojiano mpaka wakati mwingine,sasa kwanini ulazimishe kwenda kuvamia ofisi za watu na kusimamisha shughuli za watu eti unataka uelezwe sababu za kufutwa kwa mahojiano yako? Kwani uliopitwa mara ya kwanza uliambiwa kwa nini unataka kufanyiwa mahojiano? Kwani ni lazima wewe kuhojiwa?

Je kile chombo cha habari ni mali ya CHADEMA? Kama siyo mali ya CHADEMA unataka kulazimisha ili iweje? Kwanini msifungue Tv yenu ndio muwe mnakwenda wakati wote kuhojiwa au muwe mnajirusha hata mnapokura chakula na familia zenu? Miaka yote mmepokea mamilioni kwa mamilioni ya pesa za Ruzuku kwanini mmeshindwa kuanzisha Tv au redio yenu? Hapa majuzi tu si mmetoka kutafuna zaidi ya Billion tatu kasoro kidogo tu pesa za Ruzuku? Je fedha hizo zilikuwa hazitoshi kuanzisha Tv mnazolilia Lilia kama watoto walio kliniki kutaka kuhojiwa?

Hivi Lissu na CHADEMA yake watakuwa lini na kukomaa kiakili? Halafu wafuasi wao walivyo mazuzu eti wanahangaika mitandaoni kulalamika kwanini Lissu hajahojiwa? Sasa kuhojiwa ni lazima? Je hakupewa taarifa kuwa kipindi kimefutwa? Hii yote ni kuonyesha CHADEMA hasa viongozi wake hawana kazi za aina yoyote ile wanazofanya za kuwapatia kipato zaidi ya kutegemea kupiga porojo ,Makele na uzushi midomoni pao,kwa sababu mtu mwenye kazi zake tulitegemea alipopewa taarifa tena kabla ya siku husika kufika basi angeendelea na kazi zake na shughuli zake kama kawaida na kufurahi kuwa kazi zake hazitasimama kwa siku hiyo.

Sasa kwa kuwa CHADEMA ni madalali wa kisiasa na wamefanya siasa kama sehemu ya kuneemesha matumbo yao na kuponya njaa zao ndio maana mtu anachukua gari na kufunga safari kwenda kuvamia ofisi za watu na kuanza kulilia eti anataka aambiwe sababu za kufutwa mahojiano .hivi huu siyo ujinga kweli? Siyo uwendawazimu huu? Siyo ugonjwa huu kweli? Siyo kujikatia tamaa huku kweli? Siyo kukosa kazi huku? Siyo kwamba hawa jamaa wamechanganyikiwa?

Mimi naona kuna namna mambo hayapo sawa katika vichwa vya CHADEMA,Lissu ameathirika kisaikolojia na anahitaji ushauri kumsaidia kupona .maana hili siyo jambo la kawaida hata kidogo.yaani chombo cha habari siyo chako,siyo mali yao,huna hisa wala wewe siyo mwana hisa,huchangia chochote katika chombo hicho,huwasaidia kulipa hata bili ya maji tu halafu unatoka huko mbio mbio eti nataka nielezwe kwanini hamtaki kunipa nafasi ya kufanya mahojiano na ninyi? Sasa ni lazima kufanya hivyo? Vipi kama wangeamua wakae kimya tu kama mabubu na kuweka headphone ili wasikilizage hata nyimbo za injili? Je angebaki anaongea pekee yake kama kichaa au mwendawazimu? Vipi kama maiki yake wangeiondoa sauti? Angesikika kwa nani zaidi ya kuonekana kama picha tu?

Kwanini CHADEMA wanakuwa na utoto kiasi hiki? Kwanini hawakui kiakili ? Kwanini hawakomai kifikira? Kwanini wanafanya mambo kama watoto wadogo? Kwanini wasifungue Tv zao? Ruzuku na michango kibao inakwenda wapi? Kama wanapenda sana sura zao kuonekana kwenye Tv kwanini wasifungue zaooooo? Ndio maana watanzania wanaendelea kuwapuuza sanaa CHADEMA. ila ukweli ni kuwa nje ya siasa viongozi wa CHADEMA hawana kazi zozote zile za kiuchumi wanazozifanya huku mitaani,hakuna kitu wanachozalisha kuchangia katika uchumi wetu wala kutoa hata ajira kwa vijana kumi tu.ndio maana kwa kukosa kwao kazi wanaanza kufunga safari kwenda kung'ang'ania kwenye ofisi za watu.

CHADEMA acheni kupenda vya dezo na mteremko ,kama mnapenda sana kuonekana katika Tv basi fungueni zenu na siyo kutafuna pesa zote halafu muanze kuleta usumbufu kwa watu waliofanya uwekezaji kwenye Tv na radio zao.acheni kuharibu biashara za watu,acheni kuvuruga shughuli za watu,acheni vurugu na utoto wenu.fanyeni vitu kama watu wazima na siyo kama watoto wadogo waliozibuka akili.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

View attachment 2897538View attachment 2897539View attachment 2897540View attachment 2897541View attachment 2897543View attachment 2897544
Wanaandamana kwenda kukilia UN,wanacholilia Hadi Leo hii UN haikijui 😁😁😁😁
 
Acheni kuvamia ofisi za watu kulazimisha ujinga wenu.
Ofisi zipi???
Una upungufu flani wewe!!!
Sio kila anaekupinga ni chadema...

HII NCHI IMEKOSA VIJANA WAZALENDO. INA VIJANA CHAWA KAMA WEWE...
WASIOJUA MASLAHI YA NCHI, WENYE KUPIGA UCHAWA KWA AJILI YAO.
UZALENDO NI KUILINDA NA KUIPIGANIA NCHI YAKO DHIDI YA MAADUI. BILA KUJALI ITIKADI YA CHAMA!!
CHAMA CHA SIASA NI SEHEMU/CHOMBO CHA KUWAKILISHA MAONI YA WATU.
TUMEPOTEA SANA...HASA MLIO CHAWA.
 
Kwa hiyo pale WASAFI FM alipokwenda Lissu kulazimisha mahojiano siyo ofisi? Au
 
Acheni kulialia nyie.fungueni kituo Chenu cha Tv na redio na siyo kwenda kuharibu shughuli za watu maofisini huko. Ruzuku zikitoka mnaziona tamu sana na mnazitafuna zote kama mchwa.
Tunayo CHADEMA MEDIA lakini kweni hii WASAFI MEDIA ni ya Makonda na Chalamila?
 
Acheni kulia lia ndugu zangu.fungueni Tv na redio yenu.kwani si mmepokea mamilioni kwa mamilioni ya Ruzuku? Hapa majuzi tu si mmebugia Billion 2.7? Mlishindwa nini kufungua Tv kwa miaka yote? Miaka yote si mmekuwa mnalialia tu? Kwanini hamjawahi kuchukua hatua za kufungua Tv zenu? Mtalialia mpaka lini? Mtang'ang'ania mpaka lini kwenye ofisi za watu ili mfanyiwe mahojiano?

Hivi kijana unaelewa kilichotokea?
Au unadhan kila sehemu na kila hoja ni ya kukimbillia Tu

Unadhan kwanini nape akatumwa haraka kuongea na waandishi wa habari?

Watu kama ww ndio wanafanya viongozi wasiwajibike then badae mnakuja kulalamika

Hata hao watu wanaokwenda Kwa makonda kutoa malalamiko Yao chanzo ni watu kama ww kutetea ujinga
 
Lengo ni kufikisha ujumbe kwa jamii iwe kwa mikutano ya hadhara,media ikiwemo radio,tv nk
Halikadhalika maandamano yote ni njia ya kufikia jamii/wananchi.
Kila mtu ashinde mechi zake.
Hawezi kufanya kazi yake bila kutaja vyama vingine.??
Na wewe mchumia tumbo mleta mada angalia usije beba ujauzito kwa kumwaga sifa kibao kwa waume za watu.
Maisha haya jiangalie aisee usijiachie sana..))
 
Kwani Lissu hakuambiwa kipindi kimeahirishwa na itapangwa wakati mwingine? Sasa alikuwa anang'ang'ania nini tena kwenda huko studio kuvuruga shughuli za watu? Kwani ni lazima yeye kuhojiwa? Kuna kifungu gani cha katiba kama asipohojiwa au hata kama asiingeitwa? Kile ni chombo binafsi na wala siyo mali ya CHADEMA wala wachadema haina hisa lake wala kodi za wananchi hazitumiki kuendesha kituo kile ,bali chenyewe ndio kina lipa kodi serikalini.
 
Lengo ni kufikisha ujumbe kwa jamii iwe kwa mikutano ya hadhara,media ikiwemo radio,tv nk
Halikadhalika maandamano yote ni njia ya kufikia jamii/wananchi.
Kila mtu ashinde mechi zake.
Hawezi kufanya kazi yake bila kutaja vyama vingine.??
Na wewe mchumia tumbo mleta mada angalia usije beba ujauzito kwa kumwaga sifa kibao kwa waume za watu.
Maisha haya jiangalie aisee usijiachie sana..))
Fungueni Tv yenu na siyo kulilia walizoanzisha wenzenu na kuanza kulilia ndani
 
Tunayo CHADEMA MEDIA lakini kweni hii WASAFI MEDIA ni ya Makonda na Chalamila?
Kwani mheshimiwa Makonda ndio muendesha kipindi? Ndiye aliyewazuieni? Hiyo CHADEMA media nani anaifahamu? Ipo na kupatikana kwenye king'amuzi kipi? Kwanini msiitumie hiyo media yenu?
 
Fungueni Tv yenu na siyo kulilia walizoanzisha wenzenu na kuanza kulilia ndani
Alialikwa kijana mbona unakuwa slow learner au ndio mahaba kwa chama chako huoni husikii.??
Amekufa Thadei Ole Mushi mliobaki kwenye chama Chenu kuandika nguvu za hoja hakuna mmebaki kusifiana hata kwa ujinga.
 
Back
Top Bottom