Pre GE2025 Makonda: Dereva wangu alikuwa anafunga namba za RC DSM na kutapeli watu

Pre GE2025 Makonda: Dereva wangu alikuwa anafunga namba za RC DSM na kutapeli watu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni vyema akapeleka taarifa hizi kwa wahusika ili huyo dereva ashtakiwe kwa makosa hayo ya wizi. Ni aibu kulea wezi halafu unalialia mbele ya watu.
Siyo hivyo Mkuu. Hakuna dDreva wa Serikali anaweza kufanya hivyo. Bali Makonda ndiye aliyekuwa anachukua fedha kwa kusema katumwa na Magufuli. Rejea issu ya nyumba waliokuwa wanagombea na GSM mfadhili wa Yanga
 
Huu ni utetezi wa kitoto amnao unahitaji akili ndogo mithili ya kuku kuuelewa. Maturity ni kunyamaza kwani watu wanaelewa.
Ajitetee kiutu uzima, kwani anazo akili? Cheti cha Form IV anachotumia nicha Paul Christian Makonda. Na yeye ni Daudi Albert Bashite
 
Hii story inafanana na story ya polisi [TANPOL] kukana kuhusika na matukio ya utekaji watu, kutesa na kuwaua na kisha kuwatupa misituni.......

Cha ajabu ni kuwa, kundi hili la ujambazi na ugaidi linatumia jina la TANPOL kufanya matukio haya ya uhalifu na mauji na polisi hawashituki wala kuchukua hatua yoyote ili kuwatia ktk mikono ya sheria watu hawa hatari kabisa ndani ya nchi yet, tafsiri yake rahisi kabisa ni kuwa POLISI WANADANGANYA. NI WAO NDIO WANAHUSIKA........!!

Kwa sababu jukumu kubwa la polisi kwa mujibu wa sheria na katiba ni KULINDA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO. Kwa polisi mpaka sasa kushindwa kulitia nguvuni kundi hili la kigaidi na ujambazi, ni wazi kuwa wanaukana wajibu wao huu muhimu wa kisheria na kikatiba......!

Je, wanastahili kuwepo na kuendelea kulipwa kwa kodi zetu na kutumia hovyo misaada ya wafadhili ya mabeberu wa Ulaya, America na Asia....?

Upande wa pili kuna huyu (PAUL MAKONDA a.k.a ALBERT BASHITE MALYANGILI). Yeye ktk kujivua kwake lawama anachukua mzigo wa lawama dhidi ya uhalifu, makosa na dhambi zake anamtwisha huyo anayemwita kuwa ni "dereva wake"......

Kama aliweza kugundua kuwa dereva wake hufanya ujambazi na uhalifu huo kwa kuji - "impersonate" kama RC wa DSM, tujiulize alichukua hatua gani huku yeye akiwa ndiye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa DSM.? Kama hakuchukua hatua, tafsiri yake kama ilivyo kwa polisi, YEYE NDIYE ALIKUWA ANAMTUMA, YEYE NI MUHUSIKA KTK KILA UHALIFU HUO PAMOJA NA DEREVA WAKE NA KIKOSI CHAKE CHOTE. Asijaribu kupima intelligence yetu....!

Kwa upande wa pili, inashangaza kuwa hata wale waliokuwa wanamsikiliza akitema utumbo huu walikuwa wanachekelea na kumpigia makofi na bila shaka pale palikuwepo watu wasomi, wenye vyeo, na wenye akili timamu kabisaaa lakini wakakubali kumezeshwa utumbo na uchafu huu.....!!

Kwake yeye Makonda huku ni kuweweseka kulikofikia hatua ya juu kabisa kuelekea ktk uangamivu na mwisho wake. Shetani anamsereresha kidogo kidogo kuelekea mautini na kaburini kwake.......

Na anasikitisha na kushangaza sana kwa kukosa unyenyekevu mbele ya Mungu na badala yake ameruhusu kiburi kitawale nafsi na roho yake.......

Anachopaswa kufanya kuchukua hatua ya ujasiri, kwenda msalabani pa mwokozi Yesu Kristo na kwa Mungu Baba Mwenyezi atue mizigo yake ya dhambi na makosa yote aliyoibeba hapo. Huku ndiko kupona kwake......

Lakini huu ujanja janja wa kishetani hautamfikisha popote huyu jamaa badala atakufa kifo cha kijinga sana wakati ana fursa nzuri sasa ya kujiokoa mwenyewe....

Hatumhukumu Paul Makonda. Lakini tabia na mwenendo wake unathibitisha kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake tangu nyakati zile ni za kweli.......

Aombe rehema na neema ya Mungu ktk Kristo Yesu naye atapata amani na furaha tena.....
Halafu unasikia kuna wapumbavu wanasema eti katika watu wanaweza kuwa Rais wa Tanzania baada ya Samia ni huyu Bwege??
 
Siyo hivyo Mkuu. Hakuna dDreva wa Serikali anaweza kufanya hivyo. Bali Makonda ndiye aliyekuwa anachukua fedha kwa kusema katumwa na Magufuli. Rejea issu ya nyumba waliokuwa wanagombea na GSM mfadhili wa Yanga
Kwamba, hakuna dereva wa Serikali anaweza kufanya hivyo mimi naafikiana na wewe. Hoja yangu ni kuwa kwa vile jamaa anamtuhumu dereva wake kwa kufanya wizi, ni vyema akatoa ripoti polisi ili dereva hiyo ashughulikiwe na siyo kalalamika tu hadharani pasipo kuchukua hatua stahiki.
 
Hapana kabisa, hujui uhalisia. Hebu wewe uje ujaribu kutaka kuonana na kiongozi kama waziri uone. Wateule wengi wanakuwa wamefanyiwa vetting za kutosha hawezi kuwa mchukua rushwa
Daah Unaishia sayari ya wapi wewe?
 

Jana kwenye nyama choma aliyoandaa kwa Wakuu wa Mashirika Mjini Arusha, anasema alipokuwa RC Dar, wakati yeye yupo amepumzika ndani, Dereva wake alikuwa anakuja kuchukua gari kisha kuweka namba za RC Dar na bendera kisha kwenda kwa matajiri kuomba/ kuchukua fedha kwa jina lake.

My Take:
Huyu anatafuta kujisafisha tu, ila iko siku atatuambia alimficha wapi Roma na alimzika wapi Ben Saanane
Ujinga huu na mjinga atakaye amini
Alimtuma yeye
 
Alifanya nini baada ya hapo ? Sababu kama alijua uhalifu na akakaa kimya basi na yeye awajibike by association; Au ndio anajisafisha kwamba kilichotokea ingawa alikuwa yeye watu wadhani hakuwa yeye...
 
Back
Top Bottom