Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Makonda ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 31,2019 wakati akizungumza na wasanii katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Amesema katika mtandao wa Instagram ameona picha ikimuonyesha Harmonize anayetamba na wimbo Paranawe akivuta kitu hicho hivyo ameomba ichunguzwe kama ni bangi au lah.
Harmonize ambaye yupo nchini Ghana, katika mtandao wa Instagram picha yake ikimuonyesha akivuta kitu kinachotoa moshi.
“Nimemuagiza Gavana wa huko achunguze ile ni bangi au nini na ikigundulika ni bangi atakapotua tu hapa ni pingu na kupelekwa lock up, Vizuri namlea mwenyewe na mtoto anapokosea lazima umshikishe adabu bila kujali unampendaje,” amesema Makonda.
Chanzo: Mwananchi