MAKONDA: Ikithibitika Harmonize anavuta bangi akamatwe awekwe ndani

MAKONDA: Ikithibitika Harmonize anavuta bangi akamatwe awekwe ndani

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
1548944878393.png

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ameagiza mwanamuziki Harmonize achunguzwe baada ya kuonekana akivuta kitu kinachotoa moshi na iwapo itathibitika kuwa bangi atamweka ndani.

Makonda ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 31,2019 wakati akizungumza na wasanii katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.

Amesema katika mtandao wa Instagram ameona picha ikimuonyesha Harmonize anayetamba na wimbo Paranawe akivuta kitu hicho hivyo ameomba ichunguzwe kama ni bangi au lah.

Harmonize ambaye yupo nchini Ghana, katika mtandao wa Instagram picha yake ikimuonyesha akivuta kitu kinachotoa moshi.

“Nimemuagiza Gavana wa huko achunguze ile ni bangi au nini na ikigundulika ni bangi atakapotua tu hapa ni pingu na kupelekwa lock up, Vizuri namlea mwenyewe na mtoto anapokosea lazima umshikishe adabu bila kujali unampendaje,” amesema Makonda.

Chanzo: Mwananchi
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda ameagiza vyombo vya usalama kumchunguza, harmonize_tz kama anatumia bangi au lahh! ili achukuliwe hatua za za kisheria.

Ikumbukwe kuwa Mkuu huyo wa Mkoa ni Mlezi wa WASAFI inayoongoozwa na Diamond Platinumz ambayo Harmonize ni moja ya member wa kundi hilo.
 
Huwezi kumshataki Mtu kwa jinai aliyofanya Kwenye Nchi zingine

Taifa pekee linalofanya hivyo Ni Marekani pekee Na wao hufanya hivyo kwa Ubabe wao sio Sheria

Kama Bhange kavutia Ghana huwezi kumshataki kwa Hakimu Mkazi kisutu
 
Division 0 oyee

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ha ha ha.. Ndio maana watu wanalalamika hawa wakuu wa mikoa na wilaya kutopewa semina elekezi.. Msimlaumu Bashite kwa hili, inawezekana anaamini madaraka yake yanavuka mpaka nje ya mipaka ya Tanzania..

😀😀😀
 
Huwezi kumshataki Mtu kwa jinai aliyofanya Kwenye Nchi zingine

Taifa pekee linalofanya hivyo Ni Marekani pekee Na wao hufanya hivyo kwa Ubabe wao sio Sheria

Kama Bhange kavutia Ghana huwezi kumshataki kwa Hakimu Mkazi kisutu
Hii kitu kuna mdau humu aliwahi kuniambia kuwa kuna wadau Kilimanjaro wanavukaga upande wa Kenya wanapiga mirungi na pombe alafu wanavuka boda kuja TZ tena
 
Huwezi kumshataki Mtu kwa jinai aliyofanya Kwenye Nchi zingine

Taifa pekee linalofanya hivyo Ni Marekani pekee Na wao hufanya hivyo kwa Ubabe wao sio Sheria

Kama Bhange kavutia Ghana huwezi kumshataki kwa Hakimu Mkazi kisutu
Bashite sheria azijulie wali?
 
Back
Top Bottom