Ana utani wa kizamani .....unaacha kazi unaomba kazi?
Watiania ya ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini wameendelea kujinadi mbele ya wajumbe wa CCM, akiwemo aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.
Akizungumza leo, Julai 31, 2025, mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata uliofanyika katika Kata ya Sokoni 1, Makonda amesema anaamini wajumbe wanamfahamu vyema, na kwamba ameacha kazi ili wampatie kazi, kwani anaiomba kazi anayoiweza na kuifahamu vizuri.
Hata hivyo, amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuwa Mbunge wao atahakikisha anaboresha miundombinu ya barabara ambayo amedai kuwa ni kero kubwa kwa wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini.