Pre GE2025 Makonda: Kuanzia kesho (Machi 3) kila Mwanaume hapa Arusha am-post mpenzi wake

Pre GE2025 Makonda: Kuanzia kesho (Machi 3) kila Mwanaume hapa Arusha am-post mpenzi wake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Huko Arusha, Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda amesema kuanzia Jumatatu Machi 3, mpaka Machi 7 kila Mwanaume wa Arusha am-post mpenzi au mke wake kwenye mitandao ya kijamiii kuonesha upendo. Na ukiona haujapostiwa basi uende ukafanyiwe maombi tarehe 8 siku ya Wanawake.

Wazee wa Challenge vipi imepokelewa?

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akiongea mbele ya Wanawake wa Arusha leo March 02,2025, Makonda amesema;

"Kuanzia kesho kila Mwanaume, kama kweli wewe ni Mwanaume na huyo Mke uliyenaye au Mpenzi uliyenae unampenda, kuanzia kesho tunaanza challenge hapa Arusha Wanaume kupost Wake zao, kuanzia March 03 hadi March 07,2025 kila Mwanaume anatakiwa kumpost Mke wake, ukiona haujapostiwa njoo tufanye maombi hapa March 08,2025 na Dkt. Samia"

"Kwakuwa March 08 ni siku ya Wanawake hiyo tutaacha kuitumia kwa ajili ya Wake zetu, kwa mfano Mimi nimemuambia Baba yangu mzazi ampost Mke wake na Mimi nitampost Mke wangu, kuanzia kesho tuone Wanawake wanaopendwa na Wanaume zao na ukiona haujapostiwa March 08 uje usikilize hotuba ya Dkt. Samia ndio itakayokuponya"

"Sasa kuna Watu wanasema ooh Mimi sina Instagram page, mpost hata kwenye status basi, yaani wewe kwenye WhatsApp status haumpost, Insta, Facebook haumpost, kwenye DP profile haumuweki, aah atakaa moyoni kweli huyo!?, tunataka kuona Watu wanaojivunia Wake zao, tuitumie Wiki hii kuwapa moyo Wake zetu, kuwapa faraja na kuonesha kwamba tunajivunia uwepo wao kwenye maisha yetu"
 
Watanzania wazalendo kwa nchi yao wanajiuliza kwa jinsi jua lilivyokali mwaka huu hivi ingekuwaje mgao wa umeme kama Hayati Magufuli asingejenga bwawa la umeme la mwl Nyerere?.
Ni majenereta mangapi yangeingizwa? Zingezaliwa Richmond ngapi?
Mwaka huu mvua ni chache nchi nzima na jua linatandika kwelikweli kiasi kwamba wakulima wamekosa mazao yao kwa kukauka shambani, lakini bado mafisadi yanaona aibu kutangaza mgao wa umeme kwa sababu wanaogopa watawaambia nini Watanzania kwa sababu wanajua bwawa lao la umeme walilojengewa na Rais wa wanyonge limekamilika na linauwezo wa kutoa megawati 2115.
Mafisadi kwa vikao vyao yanajiuliza sasa tutakula wapi? Na yanapofikia hiyo hatua humlaani Hayati Magufuli kwa kuanzisha ujenzi wa bwawa hilo na yakimaliza yanamlaani pia Rais Samia kwa kukubali kumalizia miradi yote iliyoachwa na Magufuli ikiwemo hilo bwawa la umeme.
Matarajio ya mafisadi ilikuwa ni kwamba pale tu Magufuli alipofariki na ujenzi wa bwawa ungeishia hapo.
 
Wakuu

Huko Arusha, Makonda amesema kuanzia kesho kila Mwanaume hapa Arusha am-post mpenzi wake

View attachment 3255928
Hiyo ndiyo miradi ya maendeleo wanayohubiri wateuliwa wa rais.
Hawa ndio viongozi wanaoonekana Wabunifu Tanzania

Poor African Country!

Watawala wa nchi za kiAfrika wamekuwa ni majanga tupu kwa Wananchi waliopo katika nchi zao.
Sasa na huyu naye eti ni mtu mwenye sifa za Kuwaongoza binadamu kweli? Seriously?
 
Paul Christian Makonda ni kiongozi mwenye maono na ubunifu mzuri,atafika mbali.
 
Back
Top Bottom