Pre GE2025 Makonda: Kuanzia kesho (Machi 3) kila Mwanaume hapa Arusha am-post mpenzi wake

Pre GE2025 Makonda: Kuanzia kesho (Machi 3) kila Mwanaume hapa Arusha am-post mpenzi wake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watanzania wazalendo kwa nchi yao wanajiuliza kwa jinsi jua lilivyokali mwaka huu hivi ingekuwaje mgao wa umeme kama Hayati Magufuli asingejenga bwawa la umeme la mwl Nyerere?.
Ni majenereta mangapi yangeingizwa? Zingezaliwa Richmond ngapi?
Mwaka huu mvua ni chache nchi nzima na jua linatandika kwelikweli kiasi kwamba wakulima wamekosa mazao yao kwa kukauka shambani, lakini bado mafisadi yanaona aibu kutangaza mgao wa umeme kwa sababu wanaogopa watawaambia nini Watanzania kwa sababu wanajua bwawa lao la umeme walilojengewa na Rais wa wanyonge limekamilika na linauwezo wa kutoa megawati 2115.
Mafisadi kwa vikao vyao yanajiuliza sasa tutakula wapi? Na yanapofikia hiyo hatua humlaani Hayati Magufuli kwa kuanzisha ujenzi wa bwawa hilo na yakimaliza yanamlaani pia Rais Samia kwa kukubali kumalizia miradi yote iliyoachwa na Magufuli ikiwemo hilo bwawa la umeme.
Matarajio ya mafisadi ilikuwa ni kwamba pale tu Magufuli alipofariki na ujenzi wa bwawa ungeishia hapo.
Hivi ni kweli hao mafisadi wanawazidi nguvu?
Mbona upinzani mnakabiliana nao chap?!
 
Wakuu

Huko Arusha, Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda amesema kuanzia Jumatatu Machi 3, mpaka Machi 7 kila Mwanaume wa Arusha am-post mpenzi au mke wake kwenye mitandao ya kijamiii kuonesha upendo. Na ukiona haujapostiwa basi uende ukafanyiwe maombi tarehe 8 siku ya Wanawake.

Wazee wa Challenge vipi imepokelewa?

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akiongea mbele ya Wanawake wa Arusha leo March 02,2025, Makonda amesema;

"Kuanzia kesho kila Mwanaume, kama kweli wewe ni Mwanaume na huyo Mke uliyenaye au Mpenzi uliyenae unampenda, kuanzia kesho tunaanza challenge hapa Arusha Wanaume kupost Wake zao, kuanzia March 03 hadi March 07,2025 kila Mwanaume anatakiwa kumpost Mke wake, ukiona haujapostiwa njoo tufanye maombi hapa March 08,2025 na Dkt. Samia"

"Kwakuwa March 08 ni siku ya Wanawake hiyo tutaacha kuitumia kwa ajili ya Wake zetu, kwa mfano Mimi nimemuambia Baba yangu mzazi ampost Mke wake na Mimi nitampost Mke wangu, kuanzia kesho tuone Wanawake wanaopendwa na Wanaume zao na ukiona haujapostiwa March 08 uje usikilize hotuba ya Dkt. Samia ndio itakayokuponya"

"Sasa kuna Watu wanasema ooh Mimi sina Instagram page, mpost hata kwenye status basi, yaani wewe kwenye WhatsApp status haumpost, Insta, Facebook haumpost, kwenye DP profile haumuweki, aah atakaa moyoni kweli huyo!?, tunataka kuona Watu wanaojivunia Wake zao, tuitumie Wiki hii kuwapa moyo Wake zetu, kuwapa faraja na kuonesha kwamba tunajivunia uwepo wao kwenye maisha yetu"

DAB ni zero brain. Ni mtu wa kutegemea ngweshi kushine.

ngweshi= ndumba
 
Duuh kumbe mtu akifeli shule kokote atakaoenda, chochote atakachoazimia, lolote atakalotenda, yeyote na wote atakao kutana nao atadhihirisha fikra finyu alizo nazo!

Aljukuja kwa mbwembwe akaanzisha utaratibu wa kupokelewa kwa misafara ya mirefu ya magari (Tanzania Specialist.Com walihusika)!

Akaanzisha utaratibu wa kambi za matibabu ya kibingwa kutoka kwa wataalamu. Zoezi lilifanyika bila maandalizi ya kutosha, likafeli. Hakuna muendelezo. Hakuna Daktari anataka kushiriki tena.

Akaanzisha utaratibu wa kukudana na wdudu na kuwajaza ujasiri. Kilichotokea ni wizi, uporaji, bangi na madawa.

Akatangazia umma kwamba wageni wakitaka kufunga ndoa wake Arusha watalipiwa gharama kwenye hotels kubwa kubwa! Hilo zoezi haijulikani lipo ama laah!

kaingilia kati maandalizi ya mshindano ya pikipiki pale Laki laki. Kilichotokea wadudu kuzamia shughuli, bangi, madawa, wizi, uporaji, ufuska na vifo vijaacha alama mbaya sana.

Akaanzisha legal aid nayo haijulikani kama itarudiwa.

Akaanzisha maandamano ya magari aina ya Land Rover. Washiriki waliingia gharama kubwa sana bila kujua ROI yake. Na tukio hilo haijulikani kama litarudiwa tena!

Kaanzisha vile vile utaratibu wa kutweza, kudharaulisha, kubagua na kulete mivutano baina ya watendaji, jamii na kuvuana nguo na viongozi wenzake.

Sasa anaandaa day trip ya wanawake 800 kwenda day trip Ngorongoro siku ya wanawake duniani

Katikati ya maandalizi siku ya wanawake Duniani Makonda anawaelekeza wanaume namna ya kuishi na wake zao kwenye mitandao ya kijamii!

Kifupi Makonda ni boya mpenda sifa!
 
1000022611.jpg
 
Watanzania wazalendo kwa nchi yao wanajiuliza kwa jinsi jua lilivyokali mwaka huu hivi ingekuwaje mgao wa umeme kama Hayati Magufuli asingejenga bwawa la umeme la mwl Nyerere?.
Ni majenereta mangapi yangeingizwa? Zingezaliwa Richmond ngapi?
Mwaka huu mvua ni chache nchi nzima na jua linatandika kwelikweli kiasi kwamba wakulima wamekosa mazao yao kwa kukauka shambani, lakini bado mafisadi yanaona aibu kutangaza mgao wa umeme kwa sababu wanaogopa watawaambia nini Watanzania kwa sababu wanajua bwawa lao la umeme walilojengewa na Rais wa wanyonge limekamilika na linauwezo wa kutoa megawati 2115.
Mafisadi kwa vikao vyao yanajiuliza sasa tutakula wapi? Na yanapofikia hiyo hatua humlaani Hayati Magufuli kwa kuanzisha ujenzi wa bwawa hilo na yakimaliza yanamlaani pia Rais Samia kwa kukubali kumalizia miradi yote iliyoachwa na Magufuli ikiwemo hilo bwawa la umeme.
Matarajio ya mafisadi ilikuwa ni kwamba pale tu Magufuli alipofariki na ujenzi wa bwawa ungeishia hapo.
Wewe kamfuate huko kaburini
 
Mke wa huyu jamaa na mke wa yule sijui Mwijaku, huwa nawaonea HURUMA SANA!
 
Back
Top Bottom