Makonda kufyatua Jezi mpya zenye nembo ya Mama?

Makonda kufyatua Jezi mpya zenye nembo ya Mama?

Fifa haitaki kabisa mambo ya siasa. Kuweka nembo ya picha ya Rais ni kukiuka muongozo huo. Kama hii taarifa ni ya kweli, naona tunatafuta kufungiwa au kulazimishwa kutumia jezi za awali.

Amandla...
Mbona mama anapotoa pesa za magoli hiyo FIFA haisemi kitu mkuu? Acha upotoshaji.
 
Kama watafanya hivyo moja kwa moja watahalibu hayo mashindano na kufanya zitangazwe siku za maandamano ndani ya hixo tarehe ..hivyo kihalibu kabisa ushiriki wa tanzania ...wazanzibari ni washenzi sana.
Kwani ikiwekwa nembo ya mama ambaye ni mzanzibar wazanzibar kinawauma nini mkuu? Mama si ni mwenzao?
 
Mbona mama anapotoa pesa za magoli hiyo FIFA haisemi kitu mkuu? Acha upotoshaji.
FIFA haikatazi timu kuzawadiwa. Inakataa mchezo wa mpira kutumika kisiasa. Kuweka nembo ni kumtangaza yule ambae picha yake inatumika. TFF haiwezi kumchangia mwanasiasa. Kuweka nembo yake inaweza kuchukuliwa kama ni kumchangia.

Kwani mama anaponunua magoli ile sio siasa mkuu?
 
FIFA haikatazi timu kuzawadiwa. Inakataa mchezo wa mpira kutumika kisiasa. Kuweka nembo ni kumtangaza yule ambae picha yake inatumika. TFF haiwezi kumchangia mwanasiasa. Kuweka nembo yake inaweza kuchukuliwa kama ni kumchangia.

Amandla...
Mkuu FIFA wanakataza jambo lolote ambalo lipo connected na siasa kama mama anavyonunua magoli ili kutafuta kiki za kisiasa.
 
Uongo. Mbona siku zote nchi na klabu zinatoa ahadi kubwa kwa timu zao kama wakishinda? Hiyo sio siasa, ni ushabiki.

Amandla..
Kwa hiyo wewe kwa ufahamu wako unadhani magoli ya mama sio ya kisiasa?
 
Hizo ni porojo tu hakuna uhalisia..

Chini ya Sheria ya 4 ya IFAB (Kifungu cha 4.5) na Kanuni za Vifaa za FIFA (FIFA Equipment Regulations), jezi za mpira wa miguu zinatakiwa kuwa huru na zisizo na upendeleo wowote wa kisiasa au kibinafsi.

Sheria zinasema wazi kuwa vifaa vya wachezaji, pamoja na jezi, kaptula, soksi, na nguo za ndani, havitakiwi kuwa na kauli mbiu, nembo, taarifa, au picha zozote za kisiasa, kidini, au za kibinafsi.
 
Makonda ameona pale sandaland hakuna upenyo wa ulaji akaona atafute wake ili apige pesa ndefu confusion man 😂 😂
Hio jezi katikati hapo wataweka picha ya samia 😂
Bajeti eti billion 523.3 hio yote ya nini kutuletea matumbo ya kina rickross na dj khaled ili
 
Rais wa DRC aliwaahidi wachezaji wake dola milioni moja kila mmoja kama wangevuka intercontinental play off stage ya world cup 2026.

Hakuchukuliwa hatua yeyote.

Amandla...
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Taarifa za kiintelejensia zilizopo ni kwamba Bwana Paulo Makonda ameazimia kutumia kila rasilimali aliyo nayo kuhakikisha kwamba anafyatua jezi mpya za timu ya taifa kwa gharama yoyote ile.

Wadau waliopo karibu na waziri huyo nguli wa michezo zinasema ndugu Makonda atafanya kila linalowezekana kusukuma agenda yake ya kufyatua jezi za timu ya taifa zenye nembo ya mama Samia. Ijapokuwa alipingwa vikali wakati anapromote jezi hiyo siku za nyuma, lakini inaonekana safari hii hataki kumsikiliza mtu yeyote yule awaye.
​
MAONI YANGU

Naungana na Bwana Makonda 💯% katika mpango wake huu kwani jezi za timu ya taifa za sasa hivi zenye rangi ya Yanga (njano) zinaogopwa na mashabiki wa klabu ya Simba pamoja na klabu nyingine za Ligu Kuu ambazo zinaichukia Yanga. Namuombea kila siku mpango wake huu ufanikiwe haraka iwezekanavyo. Amen.
Tutanunua kwa gharama yeyote!
 
Back
Top Bottom