Makonda kutoa mafuta lita 20,000 kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Maswali ya kujiuliza ni kuwa;

1. Makonda anatoa litahizi za mafuta kama mtu binafsi au serikali? Kama anatoa kama mtu binafsi vyanzo vya mapato haya ni nini? Mkuu wa Mkoa anatoa wapi pesa za kugharamia mafuta lita zote hizi?

2. Bajeti inayotengwa upande wa vyombo vya ulinzi ikijumuisha mambo yote ikiwemo hili la mafuta inafanya kazi gani? Au bajeti yao ilisitishwa? Lakini kama ilisitishwa na pesa hii inatoka serikalini, inatolewa wapi?

3. Tukumbuke hapa juzi Makonda alisema ofisi yake itakuwa inawajibika kulipa pesa za ukumbi kwa wote watakaofanya harusi Arusha. Pesa hizi zinatoka serikalini kutoka wapi? Nini kimepunguzwa ili kugharamia harusi hizi?

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ametangaza kutoa lita 20,000 za Mafuta ya Petroli na Dizeli kila mwezi kwa vikosi mbalimbali vya majeshi ya Ulinzi na usalama mkoani Arusha katika jitihada za kuongeza kasi na ufanisi katika kuimarisha ulinzi na usalama Mkoani Arusha.

Pia soma:
Mtume Mwamposa kutoa pikipiki 20 kwa Jeshi la polisi Arusha kurahisisha kazi zao

"Kwenye kampeni yetu ya pikipiki tumefikisha pikipiki 50, Leopard (Kampuni ya Utalii) ameahidi kuchangia pikiki 40 na Mwamposa pikipiki 20, kwahivyo jumla ndani ya mwezi huu tutakuwa na pikipiki 110 na tunaendelea na mchakato na tupo katika hatua nzuri ya kupata magari 50 yatakayowezesha jeshi letu la polisi kuanzia KIA mpaka Karatu na maeneo mengine ya Longido na mipaka yetu kuwe na uwepo wa vyombo vya ulinzi,

"Muonekanano wa magari tayari tunao wa jinsi yatakavyoonekana Mungu akituwezesha tutafanikiwa, tuongezee Jeshi letu magari hayo 50 lakini tutaiba magari 2 nataka tuwape Jeshi la Wananchi ili waweze kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi

"Kwahiyo, tunataka jeshi letu la polisi litupe matokeo mazuri, habari hii ya tatu mzuka tunataka iwe ni historia kwenye mkoa wetu.

"Kamanda wa Jeshi la Polisi tunakuongezea vitendea kazi, maana yake tumekupa pikipiki, na mwezi huu kwa mahitaji yako ameniambia ana upungufu wa mafuta, maana yake kwa mwezi huu tutakupa uwezo wa mafuta lita 12,000 na kwa Jeshi la Uhamiaji tunawapa lita 2,000, Jeshi la Zimamoto watapata lita 1,000, Magereza watapa lita 1,000 kwasababu Magereza pia wanafanya kazi ya kubeba wafungwa kuwatoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine, Jeshi la Wananchi tutawapa lita 1,000 na Fire tutawapa lita 1,000."

Nikipata fursa ya kuwatumikia wananchi wenzangu wa Tanzania lazima Mheshimiwa awe one of my Mentors wa Muhimu sana.

Nitajifunza mema yake yote ila zaidi ni kuwa kiongozi wa mfano haswa kwenye nyanja ya uthubutu..

Hongereni sana Wakaazi wa Arusha
 
Kutoka kwenye fungu gani la bajeti? Ama atatoa kwenye mshahara wake? Kusaka kiki kwingine hadi inapelekea hata kuongea asiyoweza.
 
Kwakweli maana ukienda kituoni una shida uite askari, stori za changia hela ya mafuta zinakua nyingi
Screenshot_20231102_120808_Remix.png
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ametangaza kutoa lita 20,000 za Mafuta ya Petroli na Dizeli kila mwezi kwa vikosi mbalimbali vya majeshi ya Ulinzi na usalama mkoani Arusha katika jitihada za kuongeza kasi na ufanisi katika kuimarisha ulinzi na usalama Mkoani Arusha.
Mtu mwenye akili hatashangilia tangazo hili la Makonda, bali atajiuliza tunakwama wapi katika taratibu za kusimamia vyombo vya usalama, jukumu la serikali kuu?
 
Niliandika jana, vibaka wa Arusha wamemchokoza Makonda.

Mpaka katowa mafuta, oparesheni inayofatia vijana watakoma, bora waanze kutajana na kujisalimisha kabisa, kabla hawajaanza kufinywa.
 
Kutoka kwenye fungu gani la bajeti? Ama atatoa kwenye mshahara wake? Kusaka kiki kwingine hadi inapelekea hata kuongea asiyoweza.
Ukiacha kuchangia pumba .......jamii forum itapumzika kwa muda
 
Maswali ya kujiuliza ni kuwa;

1. Makonda anatoa litahizi za mafuta kama mtu binafsi au serikali? Kama anatoa kama mtu binafsi vyanzo vya mapato haya ni nini? Mkuu wa Mkoa anatoa wapi pesa za kugharamia mafuta lita zote hizi?

2. Bajeti inayotengwa upande wa vyombo vya ulinzi ikijumuisha mambo yote ikiwemo hili la mafuta inafanya kazi gani? Au bajeti yao ilisitishwa? Lakini kama ilisitishwa na pesa hii inatoka serikalini, inatolewa wapi?

3. Tukumbuke hapa juzi Makonda alisema ofisi yake itakuwa inawajibika kulipa pesa za ukumbi kwa wote watakaofanya harusi Arusha. Pesa hizi zinatoka serikalini kutoka wapi? Nini kimepunguzwa ili kugharamia harusi hizi?

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ametangaza kutoa lita 20,000 za Mafuta ya Petroli na Dizeli kila mwezi kwa vikosi mbalimbali vya majeshi ya Ulinzi na usalama mkoani Arusha katika jitihada za kuongeza kasi na ufanisi katika kuimarisha ulinzi na usalama Mkoani Arusha.

"Kwenye kampeni yetu ya pikipiki tumefikisha pikipiki 50, Leopard (Kampuni ya Utalii) ameahidi kuchangia pikiki 40 na Mwamposa pikipiki 20, kwahivyo jumla ndani ya mwezi huu tutakuwa na pikipiki 110 na tunaendelea na mchakato na tupo katika hatua nzuri ya kupata magari 50 yatakayowezesha jeshi letu la polisi kuanzia KIA mpaka Karatu na maeneo mengine ya Longido na mipaka yetu kuwe na uwepo wa vyombo vya ulinzi,

"Muonekanano wa magari tayari tunao wa jinsi yatakavyoonekana Mungu akituwezesha tutafanikiwa, tuongezee Jeshi letu magari hayo 50 lakini tutaiba magari 2 nataka tuwape Jeshi la Wananchi ili waweze kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi

"Kwahiyo, tunataka jeshi letu la polisi litupe matokeo mazuri, habari hii ya tatu mzuka tunataka iwe ni historia kwenye mkoa wetu.

"Kamanda wa Jeshi la Polisi tunakuongezea vitendea kazi, maana yake tumekupa pikipiki, na mwezi huu kwa mahitaji yako ameniambia ana upungufu wa mafuta, maana yake kwa mwezi huu tutakupa uwezo wa mafuta lita 12,000 na kwa Jeshi la Uhamiaji tunawapa lita 2,000, Jeshi la Zimamoto watapata lita 1,000, Magereza watapa lita 1,000 kwasababu Magereza pia wanafanya kazi ya kubeba wafungwa kuwatoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine, Jeshi la Wananchi tutawapa lita 1,000 na Fire tutawapa lita 1,000."

Yeye anatumika tu, kuna watu ndio wanazitoa,
 
Niliandika jana, vibaka wa Arusha wamemchokoza Makonda.

Mpaka katowa mafuta, oparesheni inayofatia vijana watakoma, bora waanze kutajana na kujisalimisha kabisa, kabla hawajaanza kufinywa.
Suluhisho la Vibaka ni Serikali ya CCM itoe ajira iache kuuza tu nchi kwa Waarabu.
Vibaka hawataisha kwa Makonda kutoa lita za mafuta, haya mawazo mgando mnayatoaga wapi?
 
Dah, mbona mimi hawajanichukuwa palipouzwa? Mwenzetu umechukuliwa kwa Waarabu nini?

Chenji ya mauzo ulibahatika kuipata?
 
Niliandika jana, vibaka wa Arusha wamemchokoza Makonda.

Mpaka katowa mafuta, oparesheni inayofatia vijana watakoma, bora waanze kutajana na kujisalimisha kabisa, kabla hawajaanza kufinywa.

Toka amefika hao vibaka wapo, au ni kwakuwa wananchi wenye hasira kali wamechukua hatua mkononi ndio anaamka?
 
Mtu akiwa Diwani tu, anarukhusa ya kuingia karibu ofis zote hata za mabalozi wa nchi mbalimbali kuomba eidha kuungwa mkono katika mambo kadha wa kadha ya maendeleo ya wananchi

Kama ndivyo, Je mkuu wa mkoa ana opportunity za kiwango gani?

Makonda anajuwa kutumia furusa, na huyu ndiye kiongozi wa kuigwa, na kwa nafasi aliyopo, bado ni ndogo sana, ili nchi ifaidi ubunifu wa Makonda, ni kuondoa mawazo ya wajinga wachache kutoka chadema eti mtu huyu hafai, Makonda anapaswa kupewa Uwaziri mkuu au zaidi na hapo ndipo tutamfahamu vizuri mtu huyu
 
Back
Top Bottom