Makonda kutoa mafuta lita 20,000 kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama

Makonda kutoa mafuta lita 20,000 kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama

Maswali ya kujiuliza ni kuwa;

1. Makonda anatoa litahizi za mafuta kama mtu binafsi au serikali? Kama anatoa kama mtu binafsi vyanzo vya mapato haya ni nini? Mkuu wa Mkoa anatoa wapi pesa za kugharamia mafuta lita zote hizi?

2. Bajeti inayotengwa upande wa vyombo vya ulinzi ikijumuisha mambo yote ikiwemo hili la mafuta inafanya kazi gani? Au bajeti yao ilisitishwa? Lakini kama ilisitishwa na pesa hii inatoka serikalini, inatolewa wapi?

3. Tukumbuke hapa juzi Makonda alisema ofisi yake itakuwa inawajibika kulipa pesa za ukumbi kwa wote watakaofanya harusi Arusha. Pesa hizi zinatoka serikalini kutoka wapi? Nini kimepunguzwa ili kugharamia harusi hizi?

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda ametangaza kutoa lita 20,000 za Mafuta ya Petroli na Dizeli kila mwezi kwa vikosi mbalimbali vya majeshi ya Ulinzi na usalama mkoani Arusha katika jitihada za kuongeza kasi na ufanisi katika kuimarisha ulinzi na usalama Mkoani Arusha.

"Kwenye kampeni yetu ya pikipiki tumefikisha pikipiki 50, Leopard (Kampuni ya Utalii) ameahidi kuchangia pikiki 40 na Mwamposa pikipiki 20, kwahivyo jumla ndani ya mwezi huu tutakuwa na pikipiki 110 na tunaendelea na mchakato na tupo katika hatua nzuri ya kupata magari 50 yatakayowezesha jeshi letu la polisi kuanzia KIA mpaka Karatu na maeneo mengine ya Longido na mipaka yetu kuwe na uwepo wa vyombo vya ulinzi,

"Muonekanano wa magari tayari tunao wa jinsi yatakavyoonekana Mungu akituwezesha tutafanikiwa, tuongezee Jeshi letu magari hayo 50 lakini tutaiba magari 2 nataka tuwape Jeshi la Wananchi ili waweze kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi

"Kwahiyo, tunataka jeshi letu la polisi litupe matokeo mazuri, habari hii ya tatu mzuka tunataka iwe ni historia kwenye mkoa wetu.

"Kamanda wa Jeshi la Polisi tunakuongezea vitendea kazi, maana yake tumekupa pikipiki, na mwezi huu kwa mahitaji yako ameniambia ana upungufu wa mafuta, maana yake kwa mwezi huu tutakupa uwezo wa mafuta lita 12,000 na kwa Jeshi la Uhamiaji tunawapa lita 2,000, Jeshi la Zimamoto watapata lita 1,000, Magereza watapa lita 1,000 kwasababu Magereza pia wanafanya kazi ya kubeba wafungwa kuwatoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine, Jeshi la Wananchi tutawapa lita 1,000 na Fire tutawapa lita 1,000."

Makonda hela anatoa wapi msimkweze
 
Pablo Escobar alijenga hospital, mechi za mtaani na timu ya mtaani aliidhamini vizuri tu alitoa misaada ila yote ni wachache walijua nyuma ya hiyo misaada maana yake nini.

US Department of State huwa hawabahatishi kazi kwenu sasa.
 
Si anaongea na wamiliki wa vituo tu wanampa lita kadhaa, ni kama alivyokarabati magari ya polisi aliongea na watu wa garages tu. Ni CSR fulani kwa wenye makampuni ya mafuta.
Alafu hizo lita kwa mwezi ni ndogo sana kwa watu wa vituo vya mafuto makonda ni genius sema wenzake wanamuonea wivu sana..
Ila anachofanya ndio kinatakiwa kufanya na kila kiongozi.
 
Biashara ya ruzuku? Labda siyo mchaga.
Ajuza CCM inapata zaidi ya 3B za ruzuku, wamepora viwanja vya umma, bado wanapewa pesa na DEDs, wanachukua kwa wafanyabiashara n.k, wamefanya nini? report ya CAG ambaye ni mali ya CCM huwa anawapa hati safi CHADEMA, sijui kwanini huna akili.
 
Back
Top Bottom