Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, amepuuza taarifa na uvumi unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa maandamano ya kuzuia michezo kuelekea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), akisisitiza kuwa hakuna maandamano yoyote na kwamba wananchi wanajikita katika kutafuta riziki zao halali.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari leo, Septemba 24, 2026, jijini Dar es Salaam, Waziri Makonda ameeleza kuwa kauli hizo za maandamano ni maneno ya kimitandao yanayochangiwa na bei nafuu ya vifurushi vya intaneti. Amesisitiza kuwa mtazamo na lengo kuu la Mtanzania ni kufanya kazi kwa amani ili kujipatia kipato halali cha kuhudumia familia yake
"Nafikiri tu ni mabando tu haya yamezidi kuwa na bei nafuu wakati sisi wengine tunaona mabando ya gharama kubwa lakini wenzetu wanaona bei nafuu. Lakini Mtanzania anataka kupata kipato chake halali, anataka kutoka nyumbani asubuhi akahemea arudi nyumbani watoto wake wafanye nini? Wale", ameeleza Makonda.