Makonda: Maandamano kuzuia AFCON? Hayatakuwepo, Mtanzania anataka Amani!

Leta jina… sisi ni wazuri wa kukosoa
Samiah ana machawa wake wengi wakuchukua hiyo nafasi. Kama Nchimbi kaondolewa na watu wamesahau sembuse makonda ambaye akiwa nje ya system Hana lolote.
 
Hii promosi code tulis tulisikia hivi hivi before October 29 viongozi watumie busara hata kidogo wasidhihaki wananchi na Amani ya uongo ile hali haipo
Hawajifunzi kabisa. Angekaa kimya ingesaidia sana
 
Inawekanaje wizara ikose taarifa kuhusu jezi za timu ya taifa? Anataka kutwambia ndunguru damasi hakuwa anaelewa anachokifanya?

Ukimsikiliza Ndunguru, anasema kwenye utiaji ule wa saini yeye alikuwepo kama mwalikwa tu na wala hakuwa sehemu ya mchakato mzima...

Isipokuwa aliweza kuusoma mkataba na hakuona shida yeyote kwa sababu TFF/Serikali haikuwa ikiingia gharama ya namna yeyote...

Ijulikane kwamba Sandaland kwenye huo mkataba si kwamba alikuwa ni mzabuni bali ni mfadhili, kwamba nawapa TFF vifaa vyote vya timu za taifa lakini pia mkataba unampa idhini ya kusambaza jezi hizo kwenye maduka ya michezo...
 
Si kwamba walitakiwa watangaze tenda ya kutafuta mzabuni?
 
Very correct, promo ndio hizo.
Jibu zuri angesema hilo swala ni mambo ya ndani sio yeye! na huyu aminini kuwa hajasoma kabisa aligushi vyeti sasa ili kuziba pengo hilo huwa anadhani kujibu kila kitu ndio akili! mwache hajui siku yaja
 
Ndiyo wanaanzaga hivi hivi kuyapromote mdogo mdogo. Hadi ukifika huo muda unakuta mambo yamepamba moto.
Hawa Wanajichanganya Muda Wote Wanapoonywa
Hawaonyeki Kabisa Tayari Wameanza Kuingia Mtego Kujadili Maandamano
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, amepuuza taarifa na uvumi unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa maandamano ya kuzuia michezo kuelekea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), akisisitiza kuwa hakuna maandamano yoyote na kwamba wananchi wanajikita katika kutafuta riziki zao halali.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari leo, Septemba 24, 2026, jijini Dar es Salaam, Waziri Makonda ameeleza kuwa kauli hizo za maandamano ni maneno ya kimitandao yanayochangiwa na bei nafuu ya vifurushi vya intaneti. Amesisitiza kuwa mtazamo na lengo kuu la Mtanzania ni kufanya kazi kwa amani ili kujipatia kipato halali cha kuhudumia familia yake

"Nafikiri tu ni mabando tu haya yamezidi kuwa na bei nafuu wakati sisi wengine tunaona mabando ya gharama kubwa lakini wenzetu wanaona bei nafuu. Lakini Mtanzania anataka kupata kipato chake halali, anataka kutoka nyumbani asubuhi akahemea arudi nyumbani watoto wake wafanye nini? Wale", ameeleza Makonda.

Sasa anayapromote hayo maandano au anayazuia.

Anyway, MO29 ya mwaka huu itaamua mwelekeo.
 
Eti yeye huwa anaona mabando ni gharama
 
Back
Top Bottom