Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Pia soma: Makonda, Lukuvi pamoja na Kabudi walekea ziarani Ngorongoro
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesisitiza kuwa hatashiriki kukandamiza haki ya mtu mahala popote pale atakapokuwa, huku akikumbusha kuwa nafasi wanazopata viongozi ni upendeleo wa Mungu.
Pia soma: Rais Samia Aagiza urejeshwaji wa huduma za kijamii Ngorongoro
“Mimi mtoto wenu na mtumishi wenu lakini nina sifa nyingi mojawapo ni sifa ya kusimamia haki na ukweli, hiyo nilikula kiapo kwamba popote nitakapokuwepo kwenye nafasi yoyote sitashiriki kukandamiza haki ya mtu na sikuishia hapo nikasema nafasi hizi tunazopata ni za upendeleo wa Mungu.
Pia soma: Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe
“Lakini Mungu anapotupa nafasi anataka tufanye kazi kwa watu wake aliowaumba kwa mfano wake, furaha niliyonayo chama changu cha mapinduzi (Chama Cha Mapinduzi-CCM) ambacho mimi nilikitumikia kama mwenezi,” amesema Makonda.