Makonda: Moja ya sifa niliyonayo ni kusimamia haki na ukweli, sitashiriki kukandamiza haki ya mtu

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Your browser is not able to display this video.

Pia soma: Makonda, Lukuvi pamoja na Kabudi walekea ziarani Ngorongoro

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesisitiza kuwa hatashiriki kukandamiza haki ya mtu mahala popote pale atakapokuwa, huku akikumbusha kuwa nafasi wanazopata viongozi ni upendeleo wa Mungu.

Pia soma: Rais Samia Aagiza urejeshwaji wa huduma za kijamii Ngorongoro

“Mimi mtoto wenu na mtumishi wenu lakini nina sifa nyingi mojawapo ni sifa ya kusimamia haki na ukweli, hiyo nilikula kiapo kwamba popote nitakapokuwepo kwenye nafasi yoyote sitashiriki kukandamiza haki ya mtu na sikuishia hapo nikasema nafasi hizi tunazopata ni za upendeleo wa Mungu.

Pia soma: Wamasai Ngorongoro wamechoka kunyang’anywa ardhi yao na kupewa Mwarabu, Wameamua liwalo na liwe

“Lakini Mungu anapotupa nafasi anataka tufanye kazi kwa watu wake aliowaumba kwa mfano wake, furaha niliyonayo chama changu cha mapinduzi (Chama Cha Mapinduzi-CCM) ambacho mimi nilikitumikia kama mwenezi,” amesema Makonda.
 
[emoji7][emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono hoja.
P
 
Makonda yupi? Huyu huyu aliyepigwa ban na USA kukanyaga kwenye nchi hiyo kwa kuwa ni mtoa roho za watu?
 
Mungu ni mwema wakati Wote

Gabriel, Mikael, Raphael na Lucifer aliyetupwa kuzimu

Wengi Duniani wanafanya Kazi za Lucifer badala ya kufanya Kazi za Gabriel Mikael na Raphael

Mungu wa mbinguni mbariki Makonda
 
Mi nasimama na Anthony Blinken: 'Huyu amedhulumu haki za watu kuishi'
 
Makonda anajua maana ya Haki lakini?
 
Shida ni je, mnatenda kama ambavyo Mungu anavyotaka au ambavyo angetaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…