Makonda na Ndugai wako chimbo gani?

Makonda na Ndugai wako chimbo gani?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Viongozi waandamizi hawa katika Mihimili ya Utendaji na Bunge id est Makonda na Ndugai wako Oldonyo gani kusikoweza kufika mkono wa serikali?

Tundu alikwepa Mahakama hadi Wakili akajiondoa na hadi Mahakama ikafuta shauri je, Makonda naye anaweza kufanikiwa kukwepa Mahakama kwa njia hiyo ya Tundu?

Ndugai anaaminika kuwa nje ya mipaka ya JMT bila taarifa kwa umma, alizuia mishahara ya Tundu kwa kigezo cha utoro je, Bunge nalo leo litatumia vigezo vile vile alivyotumia Ndugai kuzuia mishahara ya Tundu; kuzuia mishahara ya Ndugai ilhali anaonekana kufuata njia ile ile aliyofuata Tundu kisiasa na kufika huko aliko kusikojulikana na anachokifanya ni kwa faida ya nani Bunge au jimbo lake?

Viongozi wote hawa watatu wamewahi kuwa na nyakati ngumu za kukabiliana wao kwa wao katika mambo kadha wa kadha.

Kweli nyota ya alfajiri haikeshi.

1645692392521.png
1645692512562.png

Taswira zote kwa hisani ya Google.
 
Unafuga jibwa then linakuja kujun'gata kigimbi, poleni sana wazee wa legacy, maisha haya yanakwenda kwa kasi saana hakuna aliyetegemea pea hii yaani bashite na Jobo waishi kama digidigi mwituni.
 
Nyota ya alfajiri haikeshi.
 
Watarudi tu ni kwamba aibu kwa sasa, ila makonda ana kesi ya kujibu mahakamanj
Ila kila mmoja wao ametengeneza legacy yake positive or negative na historia itawakumbuka kwa hayo.

Woooote watatu wana ufanano wa haiba na misimamo ya kihafidhina, hivyo wanaweza kwa wakati mwingine kukutana na kuishi kwenye standard ideology. Hivyo kwa kuwa kwenye siasa hakunaga adui wa kudumu ni rahisi siku moja wakaungana kwenye jambo moja la kisiasa.

Case Studies:
Nelson Mandela, Walter Sisulu, Oliver Tambo na Mangosuthu Buthelezi walikuja kukutana kwenye ideology moja kwa sababu wote kule nyuma walifanana kwenye uhafidhina.

Ni vivyo hivyo kwa Obote (Waziri Mkuu) na Mutesa II (Rais wa kwanza).

Ni vivyo hivyo kwa Mugabe na Banana.

Ni vivyo hivyo kwa Karume, Nyerere, Babu na Kombo.

Ni vivyo hivyo kwa Raila na Kenyatta.
 
Viongozi waandamizi hawa katika Mihimili ya Utendaji na Bunge id est Makonda na Ndugai wako Oldonyo gani kusikoweza kufika mkono wa serikali?

Tundu alikwepa Mahakama hadi Wakili akajiondoa na hadi Mahakama ikafuta shauri je, Makonda naye anaweza kufanikiwa kukwepa Mahakama kwa njia hiyo ya Tundu?

Ndugai anaaminika kuwa nje ya mipaka ya JMT bila taarifa kwa umma, alizuia mishahara ya Tundu kwa kigezo cha utoro je, Bunge nalo leo litatumia vigezo vile vile alivyotumia Ndugai kuzuia mishahara ya Tundu; kuzuia mishahara ya Ndugai ilhali anaonekana kufuata njia ile ile aliyofuata Tundu kisiasa na kufika huko aliko kusikojulikana na anachokifanya ni kwa faida ya nani Bunge au jimbo lake?

Viongozi wote hawa watatu wamewahi kuwa na nyakati ngumu za kukabiliana wao kwa wao katika mambo kadha wa kadha.

Kweli nyota ya alfajiri haikeshi.

View attachment 2129451 View attachment 2129453
Taswira zote kwa hisani ya google.
Wakati fulani siasa bhana... bora ukawa mfugaji wa kuhamahama...
 
Unafuga jibwa then linakuja kujun'gata kigimbi, poleni sana wazee wa legacy, maisha haya yanakwenda kwa kasi saana hakuna aliyetegemea pea hii yaani bashite na Jobo waishi kama digidigi mwituni.
Dini tulizoletewa na wakoloni zinatuonya kuishi na kutenda kwa kiasi.
 
Unafuga jibwa then linakuja kujun'gata kigimbi, poleni sana wazee wa legacy, maisha haya yanakwenda kwa kasi saana hakuna aliyetegemea pea hii yaani bashite na Jobo waishi kama digidigi mwituni.
Wamekuwa kama hayawani.
 
Back
Top Bottom