Viongozi waandamizi hawa katika Mihimili ya Utendaji na Bunge
id est Makonda na Ndugai wako Oldonyo gani kusikoweza kufika mkono wa serikali?
Tundu alikwepa Mahakama hadi Wakili akajiondoa na hadi Mahakama ikafuta shauri je, Makonda naye anaweza kufanikiwa kukwepa Mahakama kwa njia hiyo ya Tundu?
Ndugai anaaminika kuwa nje ya mipaka ya JMT bila taarifa kwa umma, alizuia mishahara ya Tundu kwa kigezo cha utoro je, Bunge nalo leo litatumia vigezo vile vile alivyotumia Ndugai kuzuia mishahara ya Tundu; kuzuia mishahara ya Ndugai ilhali anaonekana kufuata njia ile ile aliyofuata Tundu kisiasa na kufika huko aliko kusikojulikana na anachokifanya ni kwa faida ya nani Bunge au jimbo lake?
Viongozi wote hawa watatu wamewahi kuwa na nyakati ngumu za kukabiliana wao kwa wao katika mambo kadha wa kadha.
Kweli nyota ya alfajiri haikeshi.