Makonda: Ndaro anaingiza milioni 17 kwa mwezi, kaajiri vijana 20

Makonda: Ndaro anaingiza milioni 17 kwa mwezi, kaajiri vijana 20

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Paul Makonda amesema Serikali ipo kwaajili ya kuwawezesha Vijana wenye ndoto yakuwa mamilionea kupitia maudhui ya kazi zao huku akimtaja mchekeshaji na mtengeneza maudhui kupitia mitandao ya Kijamii Ndaro kuingiza milioni 17 na kutoa fursa za ajira kwa watu 20 kupitia kazi hiyo.

Kwa upande wa Ndaro ametoa shukrani zake baada ya kutaja na Makonda
Sisi kama vijana au content creator nifuraha kubwa kuona tunaungwa mkono na serikali katika tasnia yetu na kutoa fursa mbalimbali kwa vijana kwa lengo la kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana. Mimi kama content creator natoa shukrani za dhati kwa serikali na wizara ya sanaa utamaduni na michezo ikiongozwa na Mh Paul Makonda na naibu mh @mwanafa ni muda sasa wakujiandaa kuingia china kushusha vifaa vya kisasa zaid kwa lengo la kukuza tasnia yetu

 
Kuingiza kiasi fulani kwa mwezi ni kauli inayowapoteza wengi.
Kunamwezi fulani mtu ndio aliingiza kiasi fulani. Ila inavyozungumzwa ni kwamba as if iyo pesa anaingiza kila mwezi.
 
Shida ya elimu ya kuunga unga waga haijifichi. 😊
Huyu mkali ana ngekewa ila elimu ilimpiga chenga. Mungu hakupi vyote.
 
Mkubwa fela alituambia kupitia kinywa chake anaingiza mi 47+

Lakn leo.ananiomba mimi naye ingiza lak 2 kwa mwez

Muda n mwalimu mzuri atunze kipato chake vizuri
 
Back
Top Bottom