Makonda: Nitasimamia harusi za Lemutuz, Lulu na Meya wa Kinondoni

Makonda: Nitasimamia harusi za Lemutuz, Lulu na Meya wa Kinondoni

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Kwa kipindi kirefu kumekuwa na stori za hapa na pale kuwa muigizaji wa filamu Bongo, Elizabeth Machael 'Lulu' anaolewa na Majey.

Sasa basi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana August 18, 2018 akiongea na waandishi wa habari alipohudhuria Komaa Concert aliulizwa kuhusu uwepo wa harusi hiyo.

RC Makonda amesema Harusi ya Lulu na Majey ni miongoni mwa harusi tatu ambazo ni lazima azisimamie.

"Majizo tayari yupo kwenye mipango na binti yangu Lulu na wameshakuja nyumbani na wameshafanya vikao vingi vya kupanga kwa ajili ya Harusi," alisema RC Makonda.

RC Makonda ametaja harusi nyingine mbili ambazo lazima azisimamie ni ile ya Meya wa Kinondoni, na ya Lemutuz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Babu le mutuz anaoa???huyo mke mtarajiwa ajiandae ajue kuwa mume wake bado kuna mambo ya ujana hajayapitia
 
Mwaka 2012 wakati wa kugombea ubunge wa Africa Mashariki, Le Mutuz akiwa anaomba kura kwa wabunge kupitia wasifu wake, ilionekana alikuwa ana umri zaidi ya miaka 50, kwa sasa huenda anakaribia kufikisha miaka 60.

Sasa hii ya kuozeshwa au sijui kusimamiwa harusi na Makonda ni aibu kubwa sana. Babu mzima ambaye bado hajaacha utoto ili kuingia rika la ujana, eti anataka kuozeshwa!!!
 
Amekosa kazi za kufanya.

Sent from my SM-G950F using Tapatalk
 
tapatalk_1495798435070.jpeg

Kwani huyu dogo keshafikisha umri wa kuoa ?
 
Back
Top Bottom