Makonda: Nyama tuliyochoma Arusha haina uhusiano wowote na mafundisho ya Dkt. Janabi

Makonda: Nyama tuliyochoma Arusha haina uhusiano wowote na mafundisho ya Dkt. Janabi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ametania kuwa nyama choma ya Arusha haina uhusiano wowote na mafundisho ya Dkt. Janabi kuhusu masuala ya afya.

"Mhe. Rais, sherehe zetu zilihitimishwa jana na ulaji wa nyama... Nyama ya Mkoa wa Arusha haina uhusiano na mafundisho ya Dkt. Janabi. Sisi Wamaasi tunaendelea kula nyama miaka yote kwa kweli, nyama ni sehemu ya utamaduni wetu, nyama ni sehemu ya tiba yetu. Na tunakuomba Mheshimiwa Rais, baada ya futari basi ile nyama tuliyoionja jana, swala pamoja na wanyama wengine, tukukaribishe na wewe,” amesema Makonda.

Makonda ameyasema hayo wakati akitoa salamu za mkoa kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yanayofanyika kitaifa leo Machi 8, 2025, katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, Arusha.
 
Kumbe skuizi salam za siku ya wanawake zinawakilishwa na mwanaume...😳
 
Kumbe wamechinja Wanyama Pori wetu bila kutushirikisha?
 
Bali ina mahusiano na rushwa na kafara za damu
 
Back
Top Bottom