Makonda: Rais Samia alilibeba jina langu na kuingia nalo Kamati Kuu bila kujali kelele za chura akiamini nitamsaidia kazi. Viongozi wa Dini mniombee!

Huyuhuyu aliyekuwa anavania ofisi za watu usiku akiwa na wale mabakamabaka ndiye aombewe?
 
Hili ndo tatizo kubwa la huyu mtu, akibebwa anachana mbeleko. Akijua nyuma kuna mbuyu huwa hajali yeyote aliyembele yake. Hii tabia huwa inawaaribia waliombeba au waliomkingia kifua(Mibuyu).

Alipokingiwa kifua na JK aliwashambulia akina Mzee Warioba na Lowasa bila haya yaani kwasababu tu mtu mkubwa alikuwa nyuma yake akanyanyua mabega kupita masikio bila kujua anamuharibia aliyembeba.

Alipobebwa na JPM alichafua hali ya hewa kiasi cha kutosha, alichamba, alisweka ndani watu hovyo, yaani hakujali cha mkubwa wala mdogo yaani ninapoandika hapa nimekumbuka ile speech yake aliyosema "Tunaweza kuwa tulicheza pamoja, au tulisoma pamoja lakini kwasasa hatufanani hata kidogo. Wakubwa zako wananitambua" [emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23] nukuu sio ya usahihi moja kwa moja ila content ipo sahihi. Kwa kiongozi anayetumia busara haya maneno hawezi kusema.

Mimi nina amini alikosa ubunge Kigamboni sio kwasababu ya kupata kura chache, ila ni kwasababu JPM alitaka kujivua gamba tu kimtindo, aliona jamaa anamuaibisha anamuharibia, anamchafua katika jamii. Hakutaka kumtema live alikuwa anamuonea aibu kumtema direct kama alivyokuwa anawatema wengine. Kwasababu JPM alikuwa na uwezo wa kurudisha jina lake hata kama alikupita kama alivyofanya kwa wabunge wengine.

Sasa kipindi hiki anataka kurudia tena yale yake kumuharibia Mama, kuna haja gani ya kusema hivyo eti "alilibeba jina langu bila kujali kelele za chura?" Yeye alijuaje, alikuwepo katika kikao? Au waliongea na Rais kabla kwamba napeleka jina lako hata kama watasema potelea mbali, au alimwambia baada ya kuteuliwa kuwa nililibeba jina lako bila kujali kelele zako, wanamahusiano gani mpaka amwambie yote hayo?. Haoni kwa hili anamfanya Mwenyekiti wake aonekane hajali maamuzi au maoni ya vikao na kwamba anatumia udikteta?

Makonda hajui kuhifadhi wafadhiri wake, ni kweli ni mtu jasiri akitumwa kazi anafanya vizuri ila sometimes anapitiliza kiasi cha kuharibu. Mimi maoni yangu kwake ni kwamba UKIBEBWA BEBEKA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…