Uchaguzi 2020 Makonda: Rais wa kwanza CHADEMA bado yuko shule ya msingi, hawa wa sasa wanarukaruka

Uchaguzi 2020 Makonda: Rais wa kwanza CHADEMA bado yuko shule ya msingi, hawa wa sasa wanarukaruka

Nimefurahi kusikia na yeye anaamini CHADEMA itachukua nchi siku moja kuhusu muda kila mtu anahaki ya kutoa utabiri wake.
 
Eti lissu kwenda pale big brother ndio anajifanya anazijua shida za wananchi
 
Maisha yanakwenda Kasi Sana leo bashite na gwaji ni maswaiba bashite kawa mhubiri gwaji kawa mwanasiasa
 
Hapana Makonda, unayo maono lakini ni ya karibu mno.Mimi naona hata Mama yake rais atakayetoka CHADEMA bado hajazaliwa.
 
Kadri siku zinavyokwenda mchuano wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 unazidi kunoga. Kila silaha imefunguliwa kutoka stoo kuhakikisha ushindi unapatikana kwa kila upande.

Lakini bado CCM hawajatumia silaha yao moja hatari sana ambayo ni Paul Christian Makonda.

Inajulikana wazi kwamba Makonda ni mfuasi na anampenda sana Magufuli na huwa hapendi hata kidogo Magufuli kusemwa vibaya ama kushmbuliwa kwenye mitandao. Lakini mara hii Makonda katulia kabisa na haonekani kijihisisha na kampeni za CCM sijui kwanini.

Makonda ana wafuasi wengi sana kwenye kurasa zake za mitandao lakini sioni akijihisisha na kupost kampeni za mgombea wa CCM. Kazi wanaifanya akina Polepole za kujibu mashmbulizi kutoka upande wa upinzani.

Ningependa kumwona Makonda akimwaga sera za kuitetea serikali na kuorodhesha mafanikio ya awamu ya tano lakini yupo kimya. Sijui ni mkakati wa CCM ama vipi.

Ngoja tusubiri mpaka mwisho pengone anaweza kujitokeza muda wowote
 
Makonda ana hoja, Ajibiwe kwa hoja asibezwee Wala kutukanwa.
 
Leo alipokuwa anatoka kanisani aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alifanya mahojiano na channel ya mtandaoni inayoitwa Sauti za watu maarufu na kuulizwa anaona "Je ni kweli Lissu anaweza kuwa rais 2020?"

Makonda: Hawa wanarukaruka tu, CHADEMA bado sana kuchukua nchi, rais wa kwanza kama yupo basi atakuwa darasa la tatu au la nne anajiandaa na mtihani wa taifa, sio hawa wanaokaa miaka minne nje halafu wiki mbili kabla ya uchaguzi wananunua mitumba Manzese na kudai tayari wanajua shida za wananchi"

Wadau yapi maoni yako.
Tangu akataliwe VISA na USA akili yake haijatulia.
 
Back
Top Bottom