Uchaguzi 2020 Makonda: Rais wa kwanza CHADEMA bado yuko shule ya msingi, hawa wa sasa wanarukaruka

Uchaguzi 2020 Makonda: Rais wa kwanza CHADEMA bado yuko shule ya msingi, hawa wa sasa wanarukaruka

Lissu anawachosha akili ccm.
Novemba Lissu anapokea nchi
 
Leo alipokuwa anatoka kanisani aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alifanya mahojiano na channel ya mtandaoni inayoitwa Sauti za watu maarufu na kuulizwa anaona "Je ni kweli Lissu anaweza kuwa rais 2020?"

Makonda: Hawa wanarukaruka tu, CHADEMA bado sana kuchukua nchi, rais wa kwanza kama yupo basi atakuwa darasa la tatu au la nne anajiandaa na mtihani wa taifa, sio hawa wanaokaa miaka minne nje halafu wiki mbili kabla ya uchaguzi wananunua mitumba Manzese na kudai tayari wanajua shida za wananchi"

Wadau yapi maoni yako.
Hiyo miaka 4 huko nje alikaa tu kwa kupenda? Si alikwenda baada ya yeye kuongoza GENGE la wasiojulikana na kumchapa zile mvua za risasi mchana kweupe, mwambie bashite asijaribu kutonesha vidonda. HATUJASAHAU
 
Lissu anadai na kumtaja hadharani Huyu mkuu wa mkoa mstaafu kuwa ni moja kati ya vijana waliotumwa kufanikisha shambulizi la Mauaji ya Lissu.

Lissu huwa ni mkweli siku zote, sijawahi kumuona akiwa mnafiki na Muongo.

Mungu anashughulika na watesi wote wa Lissu.
Labda ndio sababu alienda kutafuta 'Toba' kwa Mungu kupitia mtumishi wake Cardinal Pengo.!

Maana si Jambo la kawaida mtu prominent wa dhehebu tofauti kumpigia magoti mtumishi (Askofu) wa dhehebu lingine.
Screenshot_20201011-120511.jpg
 
Kwanza yeye mwenyewe tu angejihoji kwanza anahojiwa na chombo gan? Tayari angejipatia jibu kuwa hana jipya lolote.
 
Huyuhuyu Albert Bashite Pimbi wa kutupa, mungu wa Dar nae anaenda kanisani .
IMG_20200914_140316.jpg
Screenshot_20201011-153057.png
Screenshot_20201011-153202.png
 
Ni aibu kumhoji aliyepuuzwa na wajumbe wa chama chake maana hata wao walijua fika Bashite hawezi fanya lolote la maana kwa wanakigamboni
 
Leo alipokuwa anatoka kanisani aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alifanya mahojiano na channel ya mtandaoni inayoitwa Sauti za watu maarufu na kuulizwa anaona "Je ni kweli Lissu anaweza kuwa rais 2020?"

Makonda: Hawa wanarukaruka tu, CHADEMA bado sana kuchukua nchi, rais wa kwanza kama yupo basi atakuwa darasa la tatu au la nne anajiandaa na mtihani wa taifa, sio hawa wanaokaa miaka minne nje halafu wiki mbili kabla ya uchaguzi wananunua mitumba Manzese na kudai tayari wanajua shida za wananchi"

Wadau yapi maoni yako.
Amenena ukweli kabisa ila mimi naongeza kuwa upinzani wa kweli labda utapatikana baada ya miaka 50 ijayo!
 
Unakaa nje miaka 4 then wiki mbili kabla ya uchaguzi unarudi nchini kununua mitumba manzese..

Lissu tapeli wa siasa
 
Makonda yupo sahihi, huyu kibaraka wakala wa beberu Mbeligiji hawezi kuwa Rais. Mbowe kamwingiza chaka huyu jamaa, anamuulia chama huyu.
 
Hebu achana na hicho alichosema. Naomba urudie jina la hiyo idhaa ya kimataifa iliyomhoji, inaitwaje vileeeee? Hahahahaaaaa maisha yanaenda kasi sana, kutoka BBC Dira ya dunia mpaka Upupu Online, hahahahaaa binadamu tuache kiburi, Mungu hapendi.
 
Polisi, Msajili, NEC, TISS, wote wanahangaika na mtu mmoja(LISSU), halafu huyu anaongea ujinga gani sijui!
Wiki mbili kabla ya uchaguzi wananunua nyanya Kariakoo afu eti wanajua matatizo ya watanzania!!!!

Tutampigia Magufuli 2020
 
Back
Top Bottom