Makonda: Serikali imeanza Mchakato wa Uraia Kwa Clatous Chama

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema serikali imeanza kuona taratibu za kumpatia uraia kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama baada ya kuonyesha kiwango kikubwa katika soka la Tanzania.

Akizungumza katika usiku wa Tuzo za BMT 2025, Makonda alisema kiwango alichoonyesha Chama, ikiwemo bao lake la hivi karibuni, kimeongeza hoja ya kumtaka achezee Taifa Stars.

“Kwa lile goli la juzi, wizara imeanza mchakato wa kuona taratibu za kumpatia uraia Chama ili kuongeza uwezo wa timu yetu ya taifa,” alisema Makonda.

Alisema Chama ameonyesha uwezo mkubwa wa kubadilika kulingana na mahitaji ya timu na kufanikiwa kucheza kwa ushindani katika vilabu vikubwa vya Tanzania.
 
Shida sio wao.. ni sisi watanzania
Muafrika anajikutaka anajua kila kitu ndio maana wanapigana kila mahali..congo,uganda,rwanda,south Afrika n.k ujuaji wa ujinga na upumbavu na niwapingaji wa kila kitu...jamii yenye laana hivi
 
Halafu uraia hautolewi kwa vigezo vya kujua mpira

Tuseme angekuwa mchezaji kibonde, angeenda kuomba uraia wa Tanzania angeambiwa we hujui mpira, hupati uraia ?

Na pia Waziri ame assume kwamba Mzambia anautolea udenda uraia wa Tanzania just because anacheza mpira wa kulipwa Tanzania. Chama amekwambia anataka kuutema uraia wa kwao ????

Uchambuzi wa Waziri ni hafifu.
 
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema serikali imeanza kuona taratibu za kumpatia uraia kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama baada ya kuonyesha kiwango kikubwa katika soka la Tanzania.

Akizungumza katika usiku wa Tuzo za BMT 2025, Makonda alisema kiwango alichoonyesha Chama, ikiwemo bao lake la hivi karibuni, kimeongeza hoja ya kumtaka achezee Taifa Stars.

“Kwa lile goli la juzi, wizara imeanza mchakato wa kuona taratibu za kumpatia uraia Chama ili kuongeza uwezo wa timu yetu ya taifa,” alisema Makonda.

Alisema Chama ameonyesha uwezo mkubwa wa kubadilika kulingana na mahitaji ya timu na kufanikiwa kucheza kwa ushindani katika vilabu vikubwa vya Tanzania.
SOURCE?
 
Back
Top Bottom