WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema serikali imeanza kuona taratibu za kumpatia uraia kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama baada ya kuonyesha kiwango kikubwa katika soka la Tanzania.
Akizungumza katika usiku wa Tuzo za BMT 2025, Makonda alisema kiwango alichoonyesha Chama, ikiwemo bao lake la hivi karibuni, kimeongeza hoja ya kumtaka achezee Taifa Stars.
“Kwa lile goli la juzi, wizara imeanza mchakato wa kuona taratibu za kumpatia uraia Chama ili kuongeza uwezo wa timu yetu ya taifa,” alisema Makonda.
Alisema Chama ameonyesha uwezo mkubwa wa kubadilika kulingana na mahitaji ya timu na kufanikiwa kucheza kwa ushindani katika vilabu vikubwa vya Tanzania.